Fagio la chuma, wahujumu uchumi na hapa kazi tu ni lugha moja

Oct 7, 2015
86
108
Ikiwa ni miezi sita imepita sasa tangu serikali mpya ya HAPA KAZI TU chini ya rais John Magufuli ianze kazi.

Jana viongozi wa umoja wa UKAWA wakiongozwa na mstahiki meya wa kinondoni walifanya mkutano wa hadhara eneo la manzese bakhresa.

Katika mkutano huo mwanasiasa nguli na mkongwe upande wa upinzani Tambwe Hiza aliwakumbusha watanzania lugha na kauli ambazo miaka yote serikali CCM huja nazo kuwahadaa wananchi lakini pasipo kuwa tija yoyote akisitiza hilo anasema rais Mwinyi alikuja na 'fagio la chuma' na kila mwanachi akaimba wimbo huo lakini hatimaye aliicha nchi katika umaskini mkubwa, vivyo hivyo Mh Mkapa alituambia serikali yake ni ya uwazi na ukweli lakini ambapo nchi iliingia mikataba mingi ya hovyo isiyo na manufaa kwa taifa na ndio stahili hiyo hiyo wamekuja nayo tena sasa huku ikionekana dhahiri serikali haijajipanga vyema na kwenda kwa sera za kuunga unga

Akitolea mfano sera ya elimu bure ambayo sasa imekua mtihani mkubwa na kilio kwenye shule kwakuwa fedha haziendi kwa wakati hivyo inashusha hadi morali lakini pia serikali hiyo inayojinasibu kwa viwanda imeanza njia kwa kukurupuka kwenye ishu ya sukari matokeo yake rais anaingia kwenye vita na wafanyabiashara na kuwaita wahujumu uchumi.

Akaitaka serikali na CCM wajipange vyema ili wawe wanadili na chanzo cha tatizo na sio matokeo yake.
 

Attachments

  • IMG-20160507-WA0148.jpg
    124.2 KB · Views: 32
  • IMG-20160507-WA0160.jpg
    186 KB · Views: 34
  • IMG-20160507-WA0207.jpg
    56.9 KB · Views: 42
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…