Fadhili Mpunji: Mipango hewa ya juhudi za Umoja wa Ulaya kudhoofisha nguvu ya ushawishi wa China barani Afrika zaonekana kugonga mwamba

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,091
1,094
VCG111399588701.jpg


Mkutano wa kilele kuhusu Afrika Kuzoea mabadiliko ya tabia nchi kuzoea mabadiliko ya tabia nchi “African Adaptation Summit” ulifanyika mwanzoni mwa mwezi Septemba mjini Rotterdam Uholanzi. Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za nchi za Ulaya kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, chini ya mpango wa mkubwa wa wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (COP).

Mkutano huo uliofanyika barani Ulaya uliitwa mkutano wa Kilele, ikiwa na maana kuwa viongozi wa nchi za Ulaya na wale wa upande wa Afrika walitakiwa kushiriki. Na lengo kubwa lilikuwa ni kuchangisha dola bilioni 25 za kimarekani kwa ajili ya kugharamia programu mbalimbali barani Afrika ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Undani wa mkutano huo hata hivyo, ni mkakati mpana wa nchi za Ulaya unaoitwa Global Gateway Initiative, ambao lengo lake ni kukabiliana na pendekezo la China la “Ukanda mmoja, Njia moja” (Belt and Road Initiative) ili kupunguza nguvu ya ushawishi ya China barani Afrika katika eneo la mabadiliko ya tabia nchi.

Ni wazi kuwa nchi za Ulaya zimetambua kuwa kupitia miradi inayotekelezwa nchini ya pendekezo la “Ukanda mmoja, njia moja” China imefanya juhudi kubwa kivitendo kuzisaidia nchi za Afrika kuendeleza matumizi ya nishati safi, kama vile umeme wa nishati ya maji, wa joto la ardhini, upepo na hata wa jua.

Hali hiyo unachukuliwa na baadhi ya nchi za magharibi kama daraja la China kujijengea ushawishi, kwa hiyo mpango Global Gateway Initiative na mkutano huo wa Rotterdam uliofanyika kabla ya mkutano wa COP27 unaotarajiwa kufanyika mjini Sharm el Sheikh mwezi Novemba, mbali na kuwa unataja mabadiliko ya tabia nchi, kimsingi vinailenga China.

Kinachoshangaza kuhusu mkutano huo ni kuwa nchi zilizoandaa mkutano huo, yaani nchi za Ulaya zimeupuuza na kutoupa umuhimu wowote. Mbali na Waziri Mkuu wa Uholanzi Bw. Mark Rutte kuhudhuria kwa kuwa ndio nchi mwenyeji, hakuna kiongozi mwingine wa nchi ya Ulaya aliyeshiriki, hali iliyomfanya Bw. Rute aseme wazi kuwa anaona aibu kuwa viongozi wenzake hawakushiriki kwenye mkutano huo. Hali hiyo pia ilikosolewa vikali na Rais Mack Sall na Rais Felix Tshisekedi.

Lengo lingine muhimu la mkutano huo, lilikuwa ni kuchangisha dola bilioni 25 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuzoea mabadiliko ya tabia nchi, ikiwa ni pamoja na kusafirisha teknolojia. Cha ajabu ni kuwa zilikusanya dola milioni 55 tu, kiasi ambacho ni kidogo sana ikilinganishwa na lengo lililopangwa. Rais Macky Sall amesema kilichofanywa na nchi za Ulaya kwenye mkutano huo, kimewaachia picha mbaya viongozi wa Afrika na hata wadau wengine wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kufanya wasiamini ahadi zinazotolewa na nchi za Ulaya.

Kilichotokea kwenye mkutano huo ni funzo lingine kwamba nchi zinazojaribu kuanzisha ushirikiano wa hila na nchi za Afrika kulenga upande wa tatu hazitafika popote, kwani ushirikiano huo hauna udhati wowote. China imekuwa ikifanya ushirikiano na nchi za Afrika ikilenga kutatua changamoto zilizopo, na sio kutumia changamoto zilizopo kuzilenga nchi nyingine. Hii ndio maana China inapoitisha mikutano na nchi za Afrika kujadili jambo si kama China yenyewe inashiriki kwenye mikutano hiyo kwa ufanisi, lakini pia inatekeleza kivitendo kila inachoahidi.

Kwenye mkutano wa COP 27 utakaofanyika Sharm el Sheikh, itakuwa vigumu kuamini kitakachosemwa na nchi za Ulaya, kwani undani wao kuhusu ushirikiano na nchi za Afrika kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, tayari umeonekana.
 
Hivi hawa watu bado wanaendelea na mipanga ya Scramble for Africa kwa mkono mwingine?

Tumesoma lkn bado elimu ya mwaafrika iko sawa na ile watu walisoma ili kuwa watumishi ktk serkali ya mkoloni.
Bado Afrika nchi moja moja hatujawa na ajenda ya pamoja kujitoa ktk makucha ya ukoloni wa kisasa.

Na huenda hatuoni tunagombewa na nchi za Ulaya, Marekani na China si kwa wema bali kwa ajili ya unyonyaji.
Hatujajiandaa kukabiliana na sera za nje ambazo zinalenga dominance in Africa.

Serkali zetu zinashangilia bila kuelewa, tukisafirisha viongozi kuhudhuria kwenda kupokea unyonyaji tena kwa gharama za kodi za maskini walioko vijijini.
 
Back
Top Bottom