Exposure katika kazi ni muhimu. Je, Watanzania wana wivu, chuki na ushamba?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,873
11,121
Niliwahi kuandika uzi kuhusu uelewa wa watanzania wengi upo chini ya kiwango kinachotakiwa kimataifa, na uzi wenyewe ni huu Uelewa wa mambo kwa Watanzania ni mdogo sana, Ujinga na upumbavu unaongezeka kila mwaka

Mjadala wa kujadili mtu badala ya uwezo wake binafsi ni matokeo ya watu waliokosa Lishe bora utotoni.

Badala ya kujadili uwezo wa Zuhura Yunus kama Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Dar es Salaam, Watu wanajadili Unzazibar na Pasaport, Hii yote ni Madhara ya Lishe bora utotoni.

Mambo yanayochangia watu kuwa na wivu, chuki na ushamba yanaanzia toka utotoni, Tafiti nyingi zinaonyesha makuzi ya watoto wa kitanzania ni magumu sana hasa kwenye Lishe yaani shibe ya mlo kamili.

Lishe duni ndio Chanzo cha watu kuwa na uelewa mdogo wa mambo, Mtu dhaifu hutumia nguvu nyingi kuweza kuelewa mambo madogo na ya kawaida.

Lishe bora sio jambo la utani na la kulifanyia mizaha hata kidogo, Bungeni Dodoma wakati wa Jakaya Kikwete tumewahi kulijadili jambo hili kwa mapana yake na ulikuwa mtifuano kati ya wazalishaji wa ndani na sisi tuliokuwa tunaunga mkono upande wa serikali iagize virutubisho nje ya nchi kwa ajili ya kupeleka maeneo yenye watu wengi wenye udumavu wa akili kwa watoto kama mikoa ya Kilimanjaro, Arusha Iringa na Mbeya.

Lishe duni wakati wa utoto ndio matokeo ya watu kufikiria maisha ndio haya haya tunayoishi Tanzania, Wanawaza hakuna maisha zaidi ya haya huko duniani.

Usishangae mkoa kama Kilimanjaro na Mbeya wana kila kitu shambani lakini kuna udumavu mkubwa wa akili kwa watoto, Tatizo wazazi wamekosa elimu ya lishe kwa watoto, Kipi wanatakiwa kumpa mtoto na kuacha kumpa na kwa mchanganyiko wa kiasi gani yaani Ratios anatakiwa kupewa mtoto awe na afya bora ya akili nyumbani na darasani.

Utamkuta mtoto wa Kinyakyusa na Kichaga anakula ndizi tu wiki nzima au wale wa Iringa ni hayo hayo tu ugali wakati wote, wakati shambani wana kila aina ya mboga na matunda.

Exposure nimekosa kiswahili chake fasaha lakini kwa ufupi naweza tumia msemo wa tembea uone, Soma uelimike.

Exposure ya Zuhura Yunus huwezi iweka mizania moja na ile ya Gerson Msigwa au Jaffer Haniu.

Zuhura anatambua umuhimu wa taarifa kuwafikia walaji Wengine waliobaki waliamini taarifa ni siri na hata upatikanaji wao kukanusha jambo ulikuwa ni mgumu sana.

Zimejitokeza lawama nyingi sana kuwa mbona kuna mambo kama yanapotoshwa na hakuna mtu wa kuliweka sawa, Hii yote ni kutokana watu waliokuwa kwenye hiyo nafasi waliamini Katika kuficha siri kuwafikia walengwa.

Ulaya hata nchi nyingi za mashariki ya kati ukiondoa zile zenye misimamo mikali, Lishe bora kwa watoto ni jukumu la Baba na Mama, Baba na Mama hushiriki malezi ya mtoto kwa pamoja kwa asilimia 100. Hali hii hupelekea Taifa lenye watu wa kuhoji mambo ya msingi na sio kujadili Passport, Utaifa wa Mtu au jinsia ya mtu.

Kama tumeshindwa kuwapa watoto Lishe bora utotoni basi tujitahidi wapate exposure ili kuondokana na watu wenye wivu, chuki na ushamba.
 
Mtu kama Makene alikuwa mwana kitengo cha habari wa chadema, siku hizi kawa chawa wa mama

Sasa mtu kama huyo utamteua awe pale ikulu atafanya nini zaidi ya kutumikia tumbo lake tu?
 
Mkuu kuhusu suala la lishe bora, umepita kunako. Tusipo badili vyakula fake na junkie upumbavu utakithiri!!
 
Mtu kama Makene alikuwa mwana kitengo cha habari wa chadema, siku hizi kawa chawa wa mama,

Sasa mtu kama huyo utamteua awe pale ikulu atafanya nini zaidi ya kutumikia tumbo lake tu?
Jitahidi sana umpe mwanao lishe bora ili kujenga makuzi bora, vinginevyo ndo wanakuja kuwa ma sadist kama JIWE
 
Mtu kama Makene alikuwa mwana kitengo cha habari wa chadema, siku hizi kawa chawa wa mama

Sasa mtu kama huyo utamteua awe pale ikulu atafanya nini zaidi ya kutumikia tumbo lake tu?
Sijamsikia siku nyingi sana, Zamani niliona maneno yake ni kama Mbwa abwakaye huku akifuata chakula
 
Hili swala la uraia wake ni vyema likawa cleared.
Kwani hapa Tanzania wahindi hawaruhusiwi kuwa wana ccm

Lini waliwakana ndugu zao wa India ambako wanapewa document inayoitwa Overseas citizen
 
Yaani heading tu imetosha kuandika hii reply hata kabla sijasoma article.

Watanzania asilimia kubwa tuna roho mbaya, ubinafsi, chuki, wivu na kutopenda mwingine asifanikiwe lipo wazi hili na alihitaji kuoneshwa.

Kuhusu huyo binti zuhura siwezi kufaham kwa undani kuhusu uraia wake ila, kama ana uraia wa Uingereza nadhani serikali itakuwa imefanya kosa kubwa sana, ukizingatia taifa letu halina uraia pacha, but if not binti apige kazi.

Tuendelee sasa, kwenye real life from JF tunapambana sana na roho hizi chafu za watu wanaofanya kwa wengine na hizi roho chafu nyingi zipo kwenye nyumba za ibada ambapo ndiko kuna sugu au kidonda ndugu kwa waumini wenzao.

Usione humu jukwaani watu wanawaponda wenzao ni kwa sababu ile afrikan illusion inatembea na watu na kuwapa mzimu kutembea nao.

👉🏾 Binafsi naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
 
Hamna cha maana mkuu wivu kwanza wanamchukulia mtu mwenye pesa na anaendelea kula neema eti kisa mwanamke ni namkubali na sisi wa pwani tunayo elimu kubwa sema hatukuwa na nafasi sasa ni zamu yetu mtuache kwanza ona tulivyo wastaarabu kujisitiri hatuna kik wala ukabila na ushamba

Roho safi kabis
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom