GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,841
- 118,702
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifanya GENTAMYCINE niwe najua Kujichanganya na kila aina ya Watu, Kukubalika na kujenga nao Urafiki hivyo kusaidia Kazi yangu ya 'Kufukunyuwa' Mambo kuwa rahisi.
Wadau wa Soka ( Mpira ) tukiwa tunasema kuwa kuna Rushwa Kubwa inayopelekea Timu Shiriki za Ligi Kuu Tanzania (VPL) Kupanga matokeo huwa tunamaanisha na wala hatutanii ila tunasikitika tu kuona Wahusika TAKUKURU (PCCB) wakiwa hawafanyi Kazi yao.
Leo GENTAMYCINE nimeweza kukutana na Wachezaji Waandamizi wa Timu Mbili zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania (VPL) ya Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC (sitowataja ili Kuwalinda kama nilivyowaahidi) ambapo walinieleza Kaka yao Mimi jinsi Rushwa ilivyokomaa katika Soka la Tanzania.
Bila Kunificha Mchezaji Mwandamizi wa Mtibwa Sugar FC na wa Dodoma Jiji FC wameniambia kuwa Mecbi Mbili Mtibwa Sugar FC ilizocheza na Kushinda zote iliwalazimu Kuhonga na wanaofanikisha hili ni Wachezaji wao Wastaafu ambao hupeleka Pesa kwa Timu Pinzani.
Mchezaji huyo aliniambia kuwa kwa miaka ya nyuma Mtibwa Sugar FC walikuwa ndiyo Wakihongwa na Timu Pinzani baada ya wao kuwa wameshajihakikishia kubaki Ligi Kuu ila kwa sasa baada ya wao kuwa na mwenendo ndiyo Wanahonga ili wabakie Ligi Kuu ya VPL.
Nae Mchezaji Mwandamizi (tena Tegemeo kabisa) wa Dodoma FC amenihakikishia kuwa kabla ya Mechi yao na Ihefu walishapewa Rushwa ili wakubali Kipigo walichokipata na kwamba angeshangaa kama wasingefungwa leo.
Sababu Kubwa ya Klabu ya Dodoma FC kuchukua Rushwa sasa ni kwamba wameshajihakikishia Kubakia katika Ligi Kuu ya Vodacom nchini Tanzania na hawatoacha Pesa zozote ambazo watapewa (watahongwa) na Timu Pinzani.
Kwa Nyakati tofauti kabisa Marafiki zangu hawa ambao ni Wachezaji Waandamizi wa Timu za Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC walinitajia Timu Vinara ( kwa Kipindi Ligi ikielekea Ukingoni) kwa Utoaji na Upokeaji wa Rushwa katika VPL ni Ihefu FC , Mtibwa Sugar FC, Dodoma Jiji FC, Prisons FC, KMC FC, Kagera Sugar, Gwambina FC, Ruvu Shooting, Namungo FC na Mbeya City FC.
Sijaziongelea hapa Timu Mbili Kongwe nchini Simba SC na Yanga SC pamoja ya ile Tajiri kwa Mbagala Azam FC kwakuwa wameniambia hawa Wababe Wakubwa si tu wameshawapa Hongo (Rushwa) bali ndiyo wanaongoza Kuharibu Mpira wa Bongo ( Tanzania ) kwa Kupenda Michezo hii Michafu ya Kuhonga Wachezaji au Waamuzi ili washinde Mechi zao husika.
Haya PCCB nimewatafunia nyie mezeni.