masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 16,179
- 14,252
Nikikumbuka mpaka nilipost uzi humu nyie
Aiseee siamini kama sasa hivi moyo wangu umekua na ganzi kiasi hiki.
Nitajaribu kuhadithia kwa mafungu mafungu
Ili kwa yoyote anaepitia changamoto ya kuumiza moyo sana kiasi cha kuhisi dunia sio yako,amini katika muda.
Muda huponya mioyo iliyopondeka….
Mwenzenu wakati nakutana na mpenzi wangu ambae ndo mume wangu as we speak,
Nikiri tu alinivutia kwa kila kitu lakini kikubwa sana kutoka kwake
Ni mkimya sanaaa,ni mtulivu ila mpaka akuzoee ndo mnaweza mkapoga story za ndani (na hii ni moja wapo ya silaha zake za mateso)
Mkikosana mkasema muite mtu…mimi ndo nitaonekana na kosa sababu yeye mkimya
Fast forward week mbili kabla ya harusi, yeye alikua masomoni so akarudi kwa ajili ya maandalizi
Akaacha simu yake kwa kochi pale nakumbuka nilikua naishika mara nyingi tu na Pasword nazijua
Yaani kila kitu kilikua sawa tu,,,
On that faithful day nakuta msg za watu wanaojiuza wale mtandaoni anachat nao sio wawili wala sio watatu….wa kutosha
Nilimuuliza kwa kupanik(sikupata shinikizo la moyo ile siku basi sitaugua tena moyo)
Akasema anafanya research kuoana kama hao wadada ni wa kweli ila hajawah kukutana nao😁😁😁 later on nilikuja kujua yupo addicted na porn as we speak
Like a fool, sikuamini ila nilisema nikiingia kwa ndoa nitamsusia a.k.a kutoa yote
(HILI NDO KOSA KUBWA SANA NILILIFANYA)
Sidhani kama kwa miaka 7 hii yote aliwahi kua na msichana mmoja tu huko nje,ni wengi ni wengi
Kutokana na ile incidence ya kabla ya ndoa nilikua naiba simu yake(kwa hapa ni bora uibe ufe na presha au usiibe ufe na ukimwi😂) kila ukiichek ni baby,mume wangu ni picha za utupu ni balaa
Na kwasababu anajua nitasamehee basi hajali na alikua hajali haswaa
Fast forward,,,
Nikabeba mimba ya mwanangu wa kwanza,
Alikua anatoka asubuh sanaaa anarudi usiku sanaaa
Anasema wee lea mimba mimi nitalea mtoto
Nilikua nalia usiku na mchana mpka nakuja kujifungua kwa kisu maana mpaka nakuja kujifungua sijiwezi hata kupush huyo mtoto.
Wakati yote hayo yanaendelea nilikua najiuliza mimi nina kasoro gani,nimekosea wapi,ki ukweli nilikua tu naomba msamaha kila siku na kumlilia mume wangu
Wakati nakuja kuandika uzi huku,nilishapanga hadi kuacha kazi kurudi nyumbani nikaishi tu na mwanangu.
Sikua na nguvu hata ya kupumua,mito ilikua inaloa maji,sio machozi maana ni maji,
(MTU AKIJA KUOMBA USHAURI HUMU KAMA HUWEZI MSHAURI KAA KIMYA)
Pamoja na yote hayo,baba huyu alikua ana jambo moja gumu sana kuliko yote
Ukimuuliza kuhusu hayo mambo ndo kama umemfukuza nyumbani anaondoka na akirudi hazungumzi lolote,na hata ukimuomba tuzungumze jambo lolote hataki hata kukutazama,
Nyie nilikua najiona mchafu sana,dah nilijiuliza mambo mengi sana kwa nyakati zile
Maisha yakaenda hivyo hivyo unamfuma na msg za mwanamke anakunyamazia na kuondoka nyumbani
Inabidi uanze kuomba msamaha arudi
Linatokea jambo umekosea au kakosea yeye,wewe ndo uombe msamaha arudi lasivyo anakutelekeza wewe na mtoto wako hata mwezi,
Wakati hayo yanatokea nikamcheki mzaa chema
Nikamsanua story yote kwamba mwanao sielewi asije akaniletea hechiaviii….
Akasema akisafiri mfungie condom
Kwa kipengele hichi nadhani unaelewa mtu pekee aliyekua ananifariji ni mama yangu
Kwamba vumilia ipo siku atabadilika
Maisha yakaendelea ups and down zikiwa zimetawala,
Kuna ndugu zake walikuja kuishi mmoja mlevi hswa wa kupigwa ngeu mwingine sistaduu haswa wa kubandika kucha
Aisee nyie acheni hiyo naireserve kwa leo
Nikiwa na mimba ya pili na ilikua changa na wala sikujua kama ninayo kwa kipindi kile
Siku moja tunatoka kanisani tupo kwa gari akashuka kwenda buchani kama sikosei
Akaacha simu pale screen ikapop msg juu “naona leo umeenda na mkeo kanisani””
Which means ata hapa kitaa jamaa anavisugua
Nikaona isiwe maneno mengi leo kama mwisho na uwe mwisho
Ile siku niliongea mpaka koo likakauka
Alisema hana upendo tena na mimi kama vipi niendelee na maisha yangu…
Stor ilikua ndefu hapo kati
Ila i tried to date a guy ila sikuweza tulibak tu kuwa marafiki kama miezi mitatu baadae nikajua nina mimba
Na sikumwambia,nikasema nikisema hapa shuhuli itazidi kuwa ndefu sana.
Sasa nikamwambia Mungu(na hapa ndo namini Mungu yupo)
Nikasema nimaplay part yangu ila mapenzi hayanitaki sasa nifanyeje??
Nilikua bado nimeajiriwa na nikasema ili niweze kufocus na watoto wangu na kuwaandalia future kwa sababu ni wazi ndo nishakua single mama hivyo ndani ya ndoa (ukweli ni kwamba am doing 90% ya mambo yote ya watoto wangu kama kuwatairi,sherehe mabalimbali,afya zao ) na kwa hili wala sijutii.
Basi katika kuwaza na kumsihi Mungu na kulia usiku na mchana.nikapata ufunuo wa biashara
Nilikua na msemo wangu wa kimoyoni kama siinjoy mapenzi basi ni enjoy hata pesa basi Mungu🥹.
Basi mzigo wangu wa kwanza nafikiri ulikuja nikiwa na mimba kama around 7 hivi
Nakumbuka nikapost magroup ya shule nilizosoma
Nikapataga delivery ya makumbusho mizigo yangu yoote ilikua naweka nyumbani,
Pesa ya mzigo wnagu wa kwanza nilitoa katika mshahara wangu
Nakumbuka nafanya delivery nikiwa mjamzito hizi delivery mbili sitazisahau makumbusho na goldstar k.koo
Makumbusho nimeshuka pale bus stand dah mteja ambae ni clasmate akanielekeza nishukee tena niende nikaweke sehemu aisee ni mbali na tumbo langu natamani kulia machozi hayatoki.basi nikarudi kupanda gari wakati nasubiri jamaa mmoja nae anasubir gari akawa ananiangalia kama anajua yaliyopo moyoni sitasahu .
Ya pili goldstar naenda kudeliver nimeshuka gerezani huku naambiwa njoo goldstar weee
Na ilikua ni free delivery..
Maisha yakasogea mpaka naingia wodini kujifungua napokea oda tu aisee
Nilikua jasiri ila machungu ya mapenzi ndo yamenifikisha hapa nilipo
Biashara yangu yooote nilianza nikiwa na machungu sana na nilikua najisapoti mwenyewe
Nimeanza kupona maumivu ya mapenzi na huyu bwana ndo akaanza sasa kunisapoti
Alinichukulia ela nyingi tu nikazizungusha nikalipa zote
Alinipa ela ya gari nikaizungusha nikanunua gari kwa jina langu
Yaani kwa kifupi nimeshapona
Na sina feeling hata kidogo na yeye ndo anarudi sasa kimtindo
Watoto wakubwa kiasi namshukuru Mungu
Sasa ile hali yake ya kununa kukitokea changamoto hajaacha kabisa ila nilisema asije sema nimejipata
Huwa namuuliza shida nini
Akiongea tunasolve asipozungumza nampa time yake akiwa sawa karibu tena(simpi attention hata dakika 1)simfikirii wala simuwazii kwa chochote
Sasa bwana huyu hajajua kiwango cha mimi kupona kimenifikisha sehemu mbaya sana
Hajajua
Maisha yalienda akahamishwa kikazi japo sio mbali lakini kule alikoenda kukawa na nyumba nyingine
Ila huwa anarudi
So alikua home kama miezi miwili hivi
Kuna siku nilipata mambo mazito sana kwenye biashara nikaja nikamueleza jamaa,hakuonesha kunipa sapoti kimawazo ila alinilaumu tu….kuna pesa flani ilipotea
Sikushtuka sana kwa sababu sikutegemea sana sapoti yake
Nikaingia kulala tu
Japo nilimuambia nilitegemea utanisaidia hili swala
Nikawaza nikasema sio kesi tukaendele na maisha kama 3 days ghafla akarudi home amenuna sana kila nachomsemesha hazungumzi kabisa
Yaani
Mimi kama kuna kitu nimekifanya hivi
Akitaka kitu. Anamtuma mtoto wangu huyo mkubwa
Sasa kuna mtu alikua anataka gari yangu akaitumie kwenye sherehe mimi nina gari ndefu kama noah
Yule jamaa akamwambia mume wangu,mume akamtuma mtoto aje aniambie wakati natoka na gari asubuhi
Kwamba kuna watu wanakuja kuchukua hiyo gari…
Nikasema kimoyoni huyu jamaa ana tatizo kubwa kuliko nilivyokua nawaza….nilikua ndani kwanini asiseme??
So guys nikamwambia dogo amwambie nafata mazaga hapo sokoni nageuka chap
Nikatoka nikarudi
Nafikir hilo ndo lilichochea zaidi….jamaa akaendelea na mnuno lakini kuongezea hilo AKAONDOKA
akijua nitalia na kusaga meno na kuomboleza na kumpigia
Now almost 2 months mwili unakuja kwa speed nafanya tu mazoezi hapa
Maana sijawahi kufeel FREEE kwa muda mrefu kama hivi
Yaani aisee hata sms tu sijamtumia
Jamani mpaka nafika hapa sio kwamba nimejipata ,,,ki ukweli nikiri sijawahi kutegemea kama nitashika pesa nyingi namna hii
Ila pia sijawahi kutegemea kama nitapata ganzi kiasi
Hii pesa haina uhusiano wowote na kuwa hivi
Ila nilimuomba Mungu walau niwe na kitu kimoja cha kunifariji…..
Guys amini katika muda …
It took me 7yrs