Ewe mzazi kama unaishi na mwanao au jamaa ambaye ni Jobless, basi zingatia haya

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
30,554
62,390
Salam wakuu, andiko hili ni kwa ajili ya kuelimisha jinsi jamii inavyo paswa kuishi na ma jobless pro max.

Jamii yetu ina watu mbali mbali, wapo wenye ajira, ma jobless pro max, watu wa daraja la kati na hata wakishua. Shida inaanza baadhi ya wanajamii wanakosa utu na akili, na kupelekea kuwa ona ma jobless Kama midoli.

Haya ewe mzazi, mlezi, rafiki, zingatia haya pindi unapo kaa na jobless yoyote.

1. Usiingilie ratiba ya jobless pasipo kumtaarifu. Kama ame lala, usijifanye kumuamsha asubuhi asubuhi as if yeye ni toy lako la kuchezea.

2. Usimseme seme jobless, wakati wa chakula. Kama kuna mambo hayako sawa tafuta wakati mzuri myazungumze.

3. Usimtukane jobless kisa kukosa kazi au shughuli ya kuendesha maisha yake. Amini nakwambia kuna watu wanajifanya ni mabingwa wa kuhukumu watu, kisa tu kakosa shughuli usi muone mvivu, au mzigo, hizi kejeli zinamuathiri kisaikolojia.

4. Usimtume tume jobless kila mara, kumbuka hata punda ana mapumziko. Kukosa kwake shughuli haku kupi wewe nafasi ya kujiona mfalme. Kumbuka Kuwa utazeeka.
Sasa sijui akijipata itakuwaje.

5. Mtaarifu ikiwa hutopenda kuendelea kumpa hifadhi. Kama unaona hauna mipango ya kuendelea kukaa naye, basi mpe habari ili ajipange, haitopendeza ukimuimbia taarab hovyo.

6. Usimtolee kauli ya mfano wa kushindwa mbele ya wengine. Riziki haitoki mikononi mwako, siku Moja akichoka anaweza kukupasua huo mdomo.

Raisi wa chama Cha ma jobless pro max Intelligent businessman. Kidumu chama Cha ma jobless pro max.

Hakuna ubaguzi, umoja, upendo na amani. Sikiliza na tatua changamoto za ma jobless pro max.

OIG2.uG.jpeg
 
Back
Top Bottom