Eti mliosomea uchumi, hivi Tanzania itaingizwa uchumi wa kati kupitia kilimo au viwanda?

Opuk Jater

Senior Member
Dec 25, 2018
145
131
Habari wanandugu,
Mimi sijasomea Uchumi ila nikitumia ufahamu wangu wa kawaida kupitia elimu niliyopewa na walimu wangu wengi wakiwa ni wa UPE ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ sioni kama Tanzania itaingia kwenye huo uchumi wa kati kwa kutumia VIWANDA badala ya KILIMO.

Nasema hivi kwasababu hivyo viwanda vingi vinavyofunguliwa na hata vinavyoendelea kufanya kazi ni kama MADARAJA ya KUSAFIRISHA HELA kwenda nchi ambazo hutupatia MALI GHAFI.. Karibia kila bidhaa inayopatikana Tanzania basi kuna kasehemu kake kamesafirishwa kutoka nje...

Kama leo mtu anafungua kiwanda cha viatu lakini anaagiza ngozi kutoka nje, kiwanda cha nguo lakini pamba/vitambaa anaagiza nje, samani inaagizwa kutoka nje... Ina maana kiwanda KINANUNUA MALIGHAFI kutoka nje halafu kinatuuzia sisi walaji, halafu bidhaa zetu nyingi nazo hata haziendi nje kwahiyo soko kubwa ni WATANZANIA, kwahiyo kila kukicha HELA YA TANZANIA ITASHUKA TU...

SASA KWANINI HII SERA YA VIWANDA ISIENDANE KWENYE MZANI MMOJA NA KILIMO... NI KWELI Tanzania haiwezi kutoa kila malighafi inayohitaji viwandani ila kama KILIMO kingekuwa ndo KIPAUMBELE chetu cha KWANZA ina maana tungepunguza MANUNUZI,,,, NA WAKULIMA WANGEPATA KIPATO CHA KUWAINUA KIUCHUMI NA TAIFA kweli lingeinuka...

Sasa tunajaza VIWANDA vingi lakini ile 80% ya WATANZANIA ambayo tunasema ipo KWENYE KILIMO hainufaiki na hivi VIWANDA zaidi ya KUCHUKULIWA HELA ZAO wanazopata kwa taabu kutoka kwa WALANGUZI (MIDDLEMEN) na kwenda kununua bidhaa ambazo malighafi zimetoka CHINA...

KWAHIYO KIUFUPI HIVI VIWANDA NAVYO NI AINA FLANI YA ULANGUZI TU...

Mfano mdogo Waziri aliizindua Duka la viatu vya Skechers ,,, SASA nikajiuliza kweli Waziri mzima anaenda kufungua Duka binafsi la kulangua na kusafirisha HELA YA TANZANIA kwenda nje badala ya kiwanda cha Skechers hapa Tanzania ambacho kingekuwa kinatumia ngozi na pamba kutoka kwa wakulima na wafugaji wa Tanzania?????๐Ÿค” Pengine hizi SOLI ndo ingeaagizwa?????

KWAHIYO kwakuwa KILIMO hapa TANZANIA ni kama imefanywa kuwa ANASA inawabidi watu wawe na SHORTCUT ambazo mwisho wa siku haziingizii chochote TAIFA zaidi kushusha dhamani ya PESA yetu...
 
Kilimo na viwanda ni sekta zinazotegemeana sana maana moja hutoa malighafi nyingine hutoa nyenzo za kazi nk kwa ajili ya urahisishaji wa shughuli

Mfano kilimo hutoa malighafi kama pamba, miwa, nk ambazo hutumiwa na viwanda kwa ajili ya kutengenezea nguo, mafuta, sukari nk lakini pia viwanda hutengeneza majembe, dawa za kuulia wadudu nk ambazo hutumiwa na wakulima katika shughuli zao

Kwa hiyo kuna link baina ya hizi sekta mbili moja ikikua husababisha nyingine pia kukua kwa kiasi kikubwa ili kuleta matokeo mazuri ni vyema sana zikienda sambamba utakua umeua ndege wawili kwa jiwe moja
 
uzi mzur nitarudi
 
Inawezekana kabisa sema watanzania wanaona imposible, kwa mtazamo wangu 2027 naexpect boom kwenye uchumi wetu Magufuli anaweka foundation tu๐Ÿ’ช
 
Uchumi wa Kati tumeingia toka mwaka Jana na kifikia 2025 tutakua katika uchumi mzur zaidi wa kati kutoka kwa mwanauchumi chuo kikuu cha mzumbe
 
Unajua serikali inaposema kuhusu Uchumi wa viwanda sio kwamba ๐Ÿ’ฏ% serikali ndo itakuwa inajenga viwanda hivyo la! Serikali inakuwepo kuratibu au kuweka platform nzuri kwa ajili ya makampuni ndani ya nchi kuchangamkia fursa ya kuanzisha Viwanda.
Consumer force of demand inayopelekea super normal profit kwa wazalishaji ndio inayopelekea uanzishwaji wa viwanda kwa wauzaji ili waendelee kupata iyo super profit.
Hivyo viwanda Tanzania vinanafasi kubwa ya kuongezeka kutokana na uongezekaji wa idadi ya watu ambao kutokana na nature mwanadamu lazima anunue ili kukamilisha maitaji yake hivyo force of demand kwa bidhaa za wanadamu itakuwepo tu na daima inaongezeka.
Kwa hiyo hata serikali isiseme " hii Ni nchi ya Viwanda" automatically itafikia hatua Kila mwekezaji mkubwa ndani ya nchi anawaza kuanzisha kiwanda chake ili kufaidi hiyo super profit iliyoko kwenye Uchumi.
Kinachotakiwa kufanywa na serikali Ni kupitia Sera yake ya Viwanda Kama inamwezesha mzalishaji mzawa kufungua na kuendeleza kiwanda chake, bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani lazima zizuiliwe kuingia nchini, Sera ya Viwanda iende sawa na Sera ya kilimo hasa kuweka miundombinu hasa ya maji kwenye mapori na kuruhusu wazawa kuchangamkia mapori na mashamba hayo kwa ajili ya kufanya kilimo Cha umwagiliaji hata mvua ziziponyesha viwanda vya ndani vina uhakika was kupata malighafi bila kuathiriwa na ukame.
Kwa hiyo acha serikali isisitize kuhusu nchi ya Viwanda ila tuikumbushe na Sera ya kilimo Ni muhimu ili kupata viwanda vya uhakika.
FN Mchumi kutoka SAUT
 
Kilimo na viwanda ni sekta zinazotegemeana sana maana moja hutoa malighafi nyingine hutoa nyenzo za kazi nk kwa ajili ya urahisishaji wa shughuli

Mfano kilimo hutoa malighafi kama pamba, miwa, nk ambazo hutumiwa na viwanda kwa ajili ya kutengenezea nguo, mafuta, sukari nk lakini pia viwanda hutengeneza majembe, dawa za kuulia wadudu nk ambazo hutumiwa na wakulima katika shughuli zao

Kwa hiyo kuna link baina ya hizi sekta mbili moja ikikua husababisha nyingine pia kukua kwa kiasi kikubwa ili kuleta matokeo mazuri ni vyema sana zikienda sambamba utakua umeua ndege wawili kwa jiwe moja

Nakubaliana na were kuhusu kushabihiana kati ya Kilimo na viwanda. Swali langu, je Nchi ya Tanzania itafanikiwa kujenga huo uchumi wa kati na sera hizi za kukandamiza PRIVATE sector?

Bila kuwa na vibrant private sector haiwezekani hiyo ndoto kutimia ; huko nyuma tulijaribu kujenga uchumi kwa kutumia public secto[ Magufuli anataka kuturudisha huko] lakini tulishindwa because most if not all of the state enterprises were loss making hence a burden to the state.

These are historical lessons the Magufuli administration should learn! They don't have to invent the wheel!!!
 
Back
Top Bottom