Ethiopia: Kikosi cha zimamoto chatumika kumwaga dawa za kuua vijidudu vya corona nchi nzima

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,056
2,208
Ni Ukweli usiopingika kuwa Ethiopia chini ya uongozi wa Waziri mkuu abiy Ahmed Ali imekuwa ikifanya juhudi za dhati na za hali ya juu katika kupambana na Virusi vya corona

Juhudi hizi zinaonekana tangu Awali ni kubwa na za kupigiwa Mfano kwani walianza kusambaza vifaa vya korona vilivyokuja kwa msaada kutoka nchini China na kuvisambaza katika nchi 53 za Africa kwa kutumia shirika Lao la ndege la Ethiopian Airlines kwa gharama za serikali ya Ethiopia

Majuzi ijumaa waligeuza ukumbi jijini addis Ababa kuwa hospital ya muda kwa wagonjwa WA corona covid19 na Jana wametumia magari yao ya zimamoto kupulizia dawa mitaani katika majiji yote nchi nzima ili kuua VIJIDUDU vya CORONA covid19

Kama nchi ya makao makuu ya umoja wa afrika imekuwa mstari wa mbele kupambana katika janga hili la CORONA kwa. Kutumia kila rasilimali ilozonazo kwa sasa

My take
Nasi tujifunze kutumia rasilimali tulizonazo Kwa sasa kupambana na janga hili kwa sasa
Capture%2B_2020-04-20-10-35-30~2.jpeg
IMG_20200420_105128.jpeg
IMG_20200420_105124.jpeg
IMG_20200420_105121.jpeg
IMG_20200420_105119.jpeg
 
Back
Top Bottom