Tatizo wengi hawajui maazimio ya Bunge yaliagiza nani afanye nini.Sehemu kubwa ya maazimio ya bunge yaliagiza vyombo husika vya uchunguzi vichunguze na hatua stahiki za kisheria zichukuliwe kwa wale watakaobainika beyond reasonable doubt kuwa ni wahalifu.Raisi sio usalama taifa,Takukuru,polisi,mwendesha mashtaka wala mahakama ambao ndio sehemu kubwa ya maazimio hayo ya bunge yanawagusa.
Nchi hii inatawaliwa na sheria.Azimio la Bunge halikuagiza raisi kuwa anza fukuza fukuza kienyeji.
Hatua iliyopo ni ya vyombo vya uchunguzi wa hizo tuhuma zilizotolewa na CAG,PAC na bunge.
Vikimaliza kazi zake wa kupelekwa mahakamani watapelekwa wa kutimuliwa na raisi watakaonekana wana hatia watatimuliwa na bunge litapewa taarifa sasa ni bunge lipi litapewa hizo taarifa ni lijalo au mabunge yatakayofuata baada ya uchaguzi hilo sijui sababu itategemea vyombo vilivyokabidhiwa hiyo kazi kama vitakuwa vimemaliza kazi walizopewa kutegemeana na utaalamu wao na uwepo wa nyenzo za kazi sababu kufuatilia hii kesi kutahitaji pesa za watu kusafiri ndani na nje na mambo mengine lukuki.Kwa hiyo hiyo deadline ambayo bunge lilitoa ni laymen deadline sababu bunge lilitoa deadline blindly bila kujua ukubwa wa hiyo kazi sababu wao si wataalamu wa hayo mambo.
Sasa hivi vyombo husika ambavyo bunge liliagiza vinayafanyia kazi.Na vikiwa vinayafanyia kazi huwa havishindi ukumbi wa habari maelezo kujieleza kuwa leo tumeamka asubuhi tuko kwenye daladala kwenda kumhoji mthumiwa wa Escrow.
Tulieni acheni mihemuko