Epuka porojo, zijue takwimu za Yanga na Ihefu. Yanga iko juu!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,284
25,866
Tafadhali mfuatiliaji na mpenzi wa soka, epuka porojo. Puuza upuuzi unaoenezwa kuwa Yanga, bingwa mtetezi wa Tanzania, ni kibonde wa Ihefu FC ya kule Mbarali Mbeya.

Tangu Ihefu ipande Ligi Kuu, imecheza na Yanga mara tano. Kati ya hizo, Yanga imeshinda mara tatu. Ihefu imeshinda mara mbili. Timu hizi hazikuwahi kutoa sare. Mechi zao ni zifuatazo:

1. Tarehe 23/12/2020 Yanga ilishinda ugenini 3-0.
2. Tarehe 15/7/2021 Yanga ilishinda nyumbani 2-0.
3. Tarehe 29/11/2022 Yanga alifungwa ugenini 2-1.
4. Tarehe 16/1/2023 Yanga ilishinda nyumbani 1-0.
5. Tarehe 4/10/2023 Yanga ilifungwa ugenini 2-1.

Hadi hapo, katika mechi hizo, Yanga wamepachika magoli 8 na kufungwa magoli 4. Yanga imewahi kushinda ugenini kule Mbarali lakini Ihefu haijawahi kushinda Dar es Salaam. Na marudio ya msimu huu yatapigwa Dar es Salaam.

Puuzeni porojo za Makolo kuwa Yanga ni kibonde wa Ihefu. Yanga kwa Ihefu iko juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom