Epuka kurudiwa mara kwa mara zoezi la uchukuaji wa alama za vidole wakati wa usajili wa laini ya simu, baadhi ya Mawakala si Waaminifu

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
684
1,117
Ni muhimu Mtumiaji wa Huduma za Mawasiliano ya simu kuhakikisha anachukua tahadhari wakati wa usajili wa laini yake ya simu kwa Wakala kwa kuhakikisha Mtoa huduma ya kusajili na kuhakiki, anasajili namba husika tu.

Miongoni mwa mambo ya kuzingatia wakati wa usajili wa laini ya simu kwa alama ya kidole ni kuepuka kurudiwa mara kwa mara zoezi la uchukuaji wa alama za vidole.

Hatua nyingine muhimu ni kuhakikisha Wakala anaesajili na kuhakiki laini za simu anacho kitambulisho kutoka kwa Kampuni anayoiwakilisha. Hatua hizi ni muhimu kuchukuliwa na Mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu wakati anaposajili na kuhakiki laini yake ya simu ili kuepuka ulaghai unaotendwa na baadhi ya Mawakala wasio waaminifu wakati wa zoezi la usajili na uhakiki.

Baadhi ya mawakala wasio waaminifu husajili laini nyingine za wateja kwa kutumia utambulisho wa namba yake ya kitambulisho cha utaifa mara ukomo wa idadi ya laini Tano kwa kila mtandao inapofikia wakala huanza kusajili laini za ziada kwa kutumia namba za wateja wasiotambua ulaghai huo ili aongeze wigo wa faida kupitia idadi kubwa ya wateja aliowasajili.

Ili kumfanya mteja asigundue kwa urahisi kuwa namba yake ya NIDA imesajili namba nyingi, huanza kwa kuihakiki na kuichagua namba hiyo kuwa namba kuu kisha nyingine zote kuzifanya kuwa namba za ziada.

Baadhi ya Mawakala hao hufanya kosa hilo licha ya kufahamu ni kutenda kinyume na Sheria, hivyo katika kudhibiti uhalifu huo ni muhimu kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi kuhakiki idadi ya laini za simu zilizosajiliwa kwa kutumia namba yake ya Kitambulisho cha Taifa inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Uhakiki wa laini za simu unaofanywa na Mtumiaji mara kwa mara huwezesha kubaini namba za simu ambazo zimefanana majina ya usajili na ambazo hazitambui hivyo kurahisisha hatua za kumbainisha wakala alietenda kosa hilo ili hatua zaidi za ki-nidhamu zichukuliwe dhidi ya mhusika.

Mbinu inayotumiwa zaidi na baadhi ya mawakala wasio waaminifu wakati wa usajili wa laini ya simu kwa njia ya bayometria ni kumtaka mteja kurudia mara kadhaa zoezi la kuweka alama ya kidole ili kuthibitisha usajili; mawakala hao hubainisha kuwa zoezi la kuchukua alama za vidole lirudiwe mara kadhaa kwa madai kuwa hatua ya awali haikufanikiwa, wakati huo alama hizo huhifadhiwa ili zitumike kusajili laini za ziada.

Ni muhimu kwa mtumiaji huduma anaehitaji kusajili laini yake kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha anaweka alama ya kidole mara moja tu na ikiwa ipo haja ya zoezi kurudiwa ni muhimu wakala akatoa hakikisho kwamba zoezi hilo halilengi kuchukua alama ya kidole mara mbili na inabidi kuthibitisha; ni muhimu mpatiwa huduma akajiridhisha.

Baadhi ya Mawakala mtaani huziuza laini za simu zilizosajiliwa kwa utambulisho wa watumiaji wengine wakiziita “take away”, ni muhimu mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuepuka kununua laini hizo kwani kufanya hivyo ni kutenda kosa.

Uhalifu wa aina hii, umekuwa ni mtaji kwa baadhi ya Mawakala ambao hutumia alama hizo kusajili laini za simu zaidi ya mara moja, ili baadae kuziuza kwa watu wenye uhitaji wa laini za simu zilizosajiliwa kwa matumizi binafsi; matokeo yake laini hizo hutumika kwa matumizi ya kawaida na matumizi yanayohusisha vitendo vya jinai kama vile wizi wa mtandaoni na uhalifu mwingine.

Hivyo kutokuhakiki laini ya simu kunaweza kumweka mtumiaji wa huduma za mawasiliano matatani ikiwa laini za simu zilizosajiliwa bila kufahamu zitatumika kutenda jinai kwa makossa mbalimbali kama vile utapeli wa mtandaoni, kubagaza, kutusi, kutishia nakadhalika.

Mtoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi, anawajibika kisheria kumlinda mtumiaji wa huduma hizo, dhidi ya uhalifu mtandaoni kama Wizi na Ulaghai.

Uhakiki wa namba za simu una madhumuni ya kumlinda mtumiaji dhidi ya vitendo visivyofaa vinavyofanywa na watumiaji wengine mfano kutuma ujumbe wa vitisho, matusi na matendo ya kihalifu.

Kwa kubofya namba *106# katika simu, yako utaweza kuhakiki usajili wa namba yako ya simu, pamoja na kutazama idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa namba yako ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Baada ya kupiga namba *106# utapewa chaguzi kadhaa namba 1 hadi 5, ukichagua namba 3 utaweza kutazama idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa namba yako ya Uraia iliotolewa na NIDA. Mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi akibaini namba za ziada, zaidi ya zilizosajiliwa kwa namba yake ya NIDA, atatakiwa kuchukua hatua.

Hatua za kuchukuliwa ni pamoja na kufika katika dawati la huduma kwa wateja ili kutoa taarifa itakayowezesha kufutwa kwa namba ambazo hakuzitambua; hatua hii ni muhimu kwa kuwa inamlinda mtumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya matumizi mabaya ya namba hizo yakiwemo matumizi yanayohusisha uhalifu.

Pamoja na hakikisho hili la usalama bado baadhi ya watu wasio waaminifu wanavumbua njia mbadala za utapeli ambazo mtumiaji wa huduma za simu anaweza kuzishinda na kuhakikisha huduma anayopata inakuwa salama kwa kuhakiki laini yake ya simu na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na watoa huduma pamoja na Mamlaka inayosimamia mawasiliano.

Chanzo: https://www.tcra.go.tz/index.php/tcra-news/tcra-issues-106-for-consumer-protection
 
Nikiangalia kwangu nakuta kuna namba ya Airtel nimeisajili kwa namba yangu ya nida lakini namba hiyo siitambui.
Sasa niliicopy nikapiga akapokea dada fulani yupo mkoa mwingine anaitwa Eliza, nilipompeleleza kuniambia laini hiyo aliuziwa na vijana wanaosajili laini mitaani na alikubali kuinunua kwakua hana namba ya nida ili aweze kusajili yakwake.
Nilimvungia sema siku naenda kuifunga nitamtaarifu kama ameweka humo hela akazitoe
 
Dawa ya hili fanya hivi.
Katika usajili wako uwe na tabia ya kukagua namba zilizosajiliwa kwa nida yako.

Nimewahi kugundua namba iliyosajiliwa kwa majina yanga na namba ya nida.

Nilichukua hatua ya kuiripoti na kuifuta
 
Una report wapi?
 
Ni muhimu Mtumiaji wa Huduma za Mawasiliano ya simu kuhakikisha anachukua tahadhari wakati wa usajili wa laini yake ya simu kwa Wakala kwa kuhakikisha Mtoa huduma ya kusajili na kuhakiki, anasajili namba husika tu.

Miongoni mwa mambo ya kuzingatia wakati wa usajili wa laini ya simu kwa alama ya kidole ni kuepuka kurudiwa mara kwa mara zoezi la uchukuaji wa alama za vidole.

Hatua nyingine muhimu ni kuhakikisha Wakala anaesajili na kuhakiki laini za simu anacho kitambulisho kutoka kwa Kampuni anayoiwakilisha. Hatua hizi ni muhimu kuchukuliwa na Mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu wakati anaposajili na kuhakiki laini yake ya simu ili kuepuka ulaghai unaotendwa na baadhi ya Mawakala wasio waaminifu wakati wa zoezi la usajili na uhakiki.

Baadhi ya mawakala wasio waaminifu husajili laini nyingine za wateja kwa kutumia utambulisho wa namba yake ya kitambulisho cha utaifa mara ukomo wa idadi ya laini Tano kwa kila mtandao inapofikia wakala huanza kusajili laini za ziada kwa kutumia namba za wateja wasiotambua ulaghai huo ili aongeze wigo wa faida kupitia idadi kubwa ya wateja aliowasajili.

Ili kumfanya mteja asigundue kwa urahisi kuwa namba yake ya NIDA imesajili namba nyingi, huanza kwa kuihakiki na kuichagua namba hiyo kuwa namba kuu kisha nyingine zote kuzifanya kuwa namba za ziada.

Baadhi ya Mawakala hao hufanya kosa hilo licha ya kufahamu ni kutenda kinyume na Sheria, hivyo katika kudhibiti uhalifu huo ni muhimu kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi kuhakiki idadi ya laini za simu zilizosajiliwa kwa kutumia namba yake ya Kitambulisho cha Taifa inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Uhakiki wa laini za simu unaofanywa na Mtumiaji mara kwa mara huwezesha kubaini namba za simu ambazo zimefanana majina ya usajili na ambazo hazitambui hivyo kurahisisha hatua za kumbainisha wakala alietenda kosa hilo ili hatua zaidi za ki-nidhamu zichukuliwe dhidi ya mhusika.

Mbinu inayotumiwa zaidi na baadhi ya mawakala wasio waaminifu wakati wa usajili wa laini ya simu kwa njia ya bayometria ni kumtaka mteja kurudia mara kadhaa zoezi la kuweka alama ya kidole ili kuthibitisha usajili; mawakala hao hubainisha kuwa zoezi la kuchukua alama za vidole lirudiwe mara kadhaa kwa madai kuwa hatua ya awali haikufanikiwa, wakati huo alama hizo huhifadhiwa ili zitumike kusajili laini za ziada.

Ni muhimu kwa mtumiaji huduma anaehitaji kusajili laini yake kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha anaweka alama ya kidole mara moja tu na ikiwa ipo haja ya zoezi kurudiwa ni muhimu wakala akatoa hakikisho kwamba zoezi hilo halilengi kuchukua alama ya kidole mara mbili na inabidi kuthibitisha; ni muhimu mpatiwa huduma akajiridhisha.

Baadhi ya Mawakala mtaani huziuza laini za simu zilizosajiliwa kwa utambulisho wa watumiaji wengine wakiziita “take away”, ni muhimu mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuepuka kununua laini hizo kwani kufanya hivyo ni kutenda kosa.

Uhalifu wa aina hii, umekuwa ni mtaji kwa baadhi ya Mawakala ambao hutumia alama hizo kusajili laini za simu zaidi ya mara moja, ili baadae kuziuza kwa watu wenye uhitaji wa laini za simu zilizosajiliwa kwa matumizi binafsi; matokeo yake laini hizo hutumika kwa matumizi ya kawaida na matumizi yanayohusisha vitendo vya jinai kama vile wizi wa mtandaoni na uhalifu mwingine.

Hivyo kutokuhakiki laini ya simu kunaweza kumweka mtumiaji wa huduma za mawasiliano matatani ikiwa laini za simu zilizosajiliwa bila kufahamu zitatumika kutenda jinai kwa makossa mbalimbali kama vile utapeli wa mtandaoni, kubagaza, kutusi, kutishia nakadhalika.

Mtoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi, anawajibika kisheria kumlinda mtumiaji wa huduma hizo, dhidi ya uhalifu mtandaoni kama Wizi na Ulaghai.

Uhakiki wa namba za simu una madhumuni ya kumlinda mtumiaji dhidi ya vitendo visivyofaa vinavyofanywa na watumiaji wengine mfano kutuma ujumbe wa vitisho, matusi na matendo ya kihalifu.

Kwa kubofya namba *106# katika simu, yako utaweza kuhakiki usajili wa namba yako ya simu, pamoja na kutazama idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa namba yako ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Baada ya kupiga namba *106# utapewa chaguzi kadhaa namba 1 hadi 5, ukichagua namba 3 utaweza kutazama idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa namba yako ya Uraia iliotolewa na NIDA. Mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi akibaini namba za ziada, zaidi ya zilizosajiliwa kwa namba yake ya NIDA, atatakiwa kuchukua hatua.

Hatua za kuchukuliwa ni pamoja na kufika katika dawati la huduma kwa wateja ili kutoa taarifa itakayowezesha kufutwa kwa namba ambazo hakuzitambua; hatua hii ni muhimu kwa kuwa inamlinda mtumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya matumizi mabaya ya namba hizo yakiwemo matumizi yanayohusisha uhalifu.

Pamoja na hakikisho hili la usalama bado baadhi ya watu wasio waaminifu wanavumbua njia mbadala za utapeli ambazo mtumiaji wa huduma za simu anaweza kuzishinda na kuhakikisha huduma anayopata inakuwa salama kwa kuhakiki laini yake ya simu na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na watoa huduma pamoja na Mamlaka inayosimamia mawasiliano.

Chanzo: https://www.tcra.go.tz/index.php/tcra-news/tcra-issues-106-for-consumer-protection
Hii ilimu imekaa pahala pake kabisa acha nihakiki sasa Mangupulelo asije kuwa kaniingiza cha kike
 
Nawezaje kujua kwamba wakala amenisajili kwenye namba nisizozijua?
 
Mimi ni wakala na nasajili laini, lakini kitu watu wengi hawatambui ni kwamba hauwezi kusajili laini mbili kwa wakati mmoja hasa kwa mtandao ule ule kwani inakudai usubiri dakika 30 ndo upate kusajili laini nyingine.

Kwa hoja ya kusema kwamba mteja kuweka kidole mara moja hiyo ni sawa lakini kwa upande mwingine haiwezekani sababu kuna wateja alama za vidole zinasumbua unakuta unajaribisha karibia vidole vyote ndipo kimojawapo kinakuja kukubali kuacha hilo unakuta kuna shida ya kimtandao na kutokana na hili ndiyo maana mimi huwa napenda sana kuwahudumia wateja ambao wanajua kusoma na waelewa mtu ukimwambia laini imekataa unamwonesha anakubali mnarudia tena.

Kwaiyo hii hoja ya kuweka kidole mara moja ni sawa lakini tusisahau kuwa kuna mtandao kusumbua, lakini pia kuna muda kidole kama kidole alama hazionekani vizuri adi urudie tena.

Tusisahau pia kuwa hauwezi ukasajiri laini mbili kwa wakati mmoja et mfano upige Tigo/Yas mbili mda huo huo no adi nusu saa ipite na zipo laini ambazo zinakataa inakubidi ubadili laini nyingine ndo inakubali.

Kuhusu lingine japo halijazungumziwa ni lile la kusema mawakala wa mtaani ni wezi,,,tusisahau wizi ni tabia ya mtu hata aloweka kibanda anakuibia fresh tu.

Labda tu niseme kwamba tuwe wadadisi wakati tunasajiliwa laini na mawakala na siyo kufokafoka kama wateja wengine,nimemaliza chuo hii ndo kazi inayoniweka mjini naipenda na natafuta namna ya kuifanya kwa ufasihi inipe matokeo ninayoyataka.

Ombi langu kwa TCRA wasijekaa wakazuia mawakala wa mtaani, watakua wameau ajira nyingi mno za vijana ikiwa ni pamoja na mimi.
 
Naona hii ishu watu hawaelewi ukweli ni kwamba sio kuweka kidole mara mbili ishu ni kuhakiki namba yako ya nida kuwa umesajili laini ngap kwa kupiga *106#

Kisha chagua kuangalia laini ulizo sajili mitandao yote au mtandao mmoja na watakuambia weka nida yako zeni utaona wanakutumia namba zako ulizo sajili zote hii itakusaidia kuona namba gani huitambui na utaenda kwenye mtandao usika na kuifuta lakini.

Masuala ya kusema usiweke kidole mara mbili siockweli maana kuna muda mtandao unasumbua kweli au wengine vidole vyao vina sumbua kutokana na kazi wanazo fanya kwani hata uko nida wakati unaenda kujiandikisha kuna watu wanarudia sana kuweka halama za vidole sembuse uku kwenye usajili lazima nyinyi kama chombo cha habari mnatakiwa kutoa taarifa zenye weledi.
 
Back
Top Bottom