Emmanuel Chengula achukua fomu ya Kugombea Uenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa, atapambana na William Mungai

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,782
239,459
Uchaguzi wa Chadema Mkoa wa Iringa umefika patamu, baada ya Emmanuel Chengula ambaye Ushawishi wake kwa wapiga kura unatisha, kuchukua fomu ya kuomba Uenyekiti wa Mkoa.

Chengula anatarajiwa kupambana na Mwenyekiti anayemaliza muda wake Bilionea William Mungai.

Screenshot_2024-04-05-14-14-55-1.png
 
Kila mwenye kutaka fomu zipo , chadema haichapishi fomu 1 tu
Mie nimeuliza tu, Nani atachukua fomu ya Uenyekiti Taifa?

Sasa kama unataka tuuliznae fomu, haya.

Miaka ishirini fomu imetoka ni moja tu ndani ya CHADEMA.?(Nipo tayari kusahahishwa)

Huko kwingine ni kila baada ya mihula inayoruhusiwa wanachukua fomu ACT n.k

Na pia kuna mfano, CCM ilikuwa na Fomu 38 2014, CHADEMA Ilikuwa na fomu ngapi? Ya Dkt Slaa, enhe....
 
Unatuletea habari za hao nyumbu wako tusiowafahamu ili iweje? Ana mchango nchi hii, nani anamfahamu, ataisaidia nini nchi yetu? Nyie nyumbu muendelee kuandamana.
 
Nani atachukua fomu ya Uenyekiti Taifa?
Nenda kamuulize Mwakipande,upumbavu mwingine unatia kinyaa,wewe unajua yatakayokutokea in the next few mins?sio lazima uchangie kila uzi,Chadema ni political party yenye katiba yake,wakati utakapofika katiba ipo wazi kwa wenye sifa ya kugombea uongozi
 
Unatuletea habari za hao nyumbu wako tusiowafahamu ili iweje? Ana mchango nchi hii, nani anamfahamu, ataisaidia nini nchi yetu? Nyie nyumbu muendelee kuandamana
Wewe nani kakupa usemaji wa hao?kama wewe huwafahamu mimi ninawafahamu,chama dola kipo madarakani for more than 60yrs mmeifanyia nini kodi yangu,nimepita juzi kati pale kitonga pass,yaani sikuelewa matengenezo yale yanalenga nini,wameshindwa hata kuweka alama za kuwaonya watumiaji wa barabara na hii ndio serikali ya ccm inavyofanya kazi yake,kama idara ya zimamoto.
 
Nenda kamuulize Mwakipande,upumbavu mwingine unatia kinyaa,wewe unajua yatakayokutokea in the next few mins?sio lazima uchangie kila uzi,Chadema ni political party yenye katiba yake,wakati utakapofika katiba ipo wazi kwa wenye sifa ya kugombea uongozi
Unateseka na mimi kuchangia Uzi? Wewe umefanya nini hapo, kwani ulikuwa una ulazima wa kuharisha hapa?

Ntamuuliza huyo Mwakinini sijui, ila wewe nenda uKajiharie huko uliko.

Usinishobokee kabisa sipendi miharo.
 
Mie nimeuliza tu, Nani atachukua fomu ya Uenyekiti Taifa?

Sasa kama unataka tuuliznae fomu, haya.

Miaka ishirini fomu imetoka ni moja tu ndani ya CHADEMA.?(Nipo tayari kusahahishwa)

Huko kwingine ni kila baada ya mihula inayoruhusiwa wanachukua fomu ACT n.k

Na pia kuna mfano, CCM ilikuwa na Fomu 38 2014, CHADEMA Ilikuwa na fomu ngapi? Ya Dkt Slaa, enhe....
Umeandika uongo duni sana ! Chaguzi zote za Chadema imetoa nafasi kwa kila atakaye , Uchaguzi uliopita , aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani , Fredrick Sumaye alichukua fomu ya kuomba uenyekiti wa Taifa , japo baadaye alijitoa mwenyewe , hakukataliwa kuchukua fomu , Mbunge wa Ndanda Bwana Mwambe alichukua fomu na kugombea ambapo alivuna kura 56 na kuangushwa na Mbowe.

Hoja yako ya uongo imekufa kibudu
 
Haikuwa hoja ile, ulikuwa ni mfano. Hata hivyo maoni yako yanapimika, Itoshe, Haujajibu swali langu, porojo ya nini?

Nauliza hivi, Ni nani atachukua fomu ya Uenyekiti wa Taifa?

Tatizo lipo wapi kutoa jibu? Manake una taarifa zote za Wagombea wa Juu wa CHAMA-Mabilionea na wasiokuwa Mabilionea. Where is the problem Bwashee?

Chunga majibu yako ya kupindisha pindisha.

NB:Hakuna kitu kama Uongo duni. Umejitungia tu maneno kukwepa swali langu.
 
Sasa Chadema imetoa nafasi , mimi nitawajuaje watakaochukua fomu ? sijawahi kuwa mpiga ramli , tusubiri wakati utakapofika tutawajua tu , ngoja tumalize hawa wa mikoa .

Najua mpaka sasa ccm ina mgombea uenyekiti na Mgombea Urais , lakini Chadema haina ni mpaka kipyenga kipulizwe
 
Back
Top Bottom