Elon Musk anaunga mkono sana mapinduzi ya kijeshi yatokee Venezuela. Kuna siri gani nyuma ya hili?

Xi Jinping

JF-Expert Member
Jun 14, 2023
1,815
5,754
Jana matokeo ya uchaguzi yalipotoka ilitangazwa kuwa Nicolás Maduro ameshinda tena kiti cha uraisi nchini Venezuela. Akimshinda mpinzani wake Edmundo González ambaye anaungwa mkono na Marekani.

Viongozi wa mataifa ya Magharibi wameonyesha kutofurahishwa na matokeo hayo. Huku vyombo vya habari vya mataifa hayo vikieneza propaganda na habari za uongo.

Lakini pia bilionea Elon Musk amekuwa mstari wa mbele kupitia tweets kwenye akaunti yake ya X akimkosoa vikali Maduro kuwa ni dictator na ameiba kura.
20240731_062725.jpg

Hizi ni baadhi ya tweets za Elon Musk dhidi ya Maduro.


Elon Musk amefikia hatua ya kutaka kutokee mapinduzi ya kijeshi ili Maduro apinduliwe!

Swali ni kwa nini Elon Musk amekuwa akipigania hilo?

Je, ni kwa sababu ya utajiri wa madini, mafuta na gas ulio katika nchi hiyo?


20240730_234243.jpg

Hazina ya utajiri wa madini, mafuta na gas wa taifa la Venezuela unakadiriwa kuwa ni $14 trillion.


Wakati wa utawala wa Hugo Chávez mwaka 2009 iligunduliwa utajiri wa madini ya coltan. Madini hayo pamoja na lithium yanatumika kwenye kutengeneza bidhaa nyingi za high tech kama vile:
  • Electric car batteries (EV batteries)​
  • Rockets​
  • Jet engines​
  • Electronic devices (computer, mobilephones etc)
Je, Elon Musk anataka mapinduzi hayo yatokee ili ashirikiane na taifa lake dhalimu Marekani kuiba madini ya coltan na lithium kwa ajili ya uwekezaji aliofanya kwenye EVs na SpaceX? We never know!



Inajulikana kuwa Elon Musk ni Pro-Israel mkubwa sana na ni rafiki wa karibu wa Netanyahu.

Na hivi karibuni wakati wa uchaguzi kauli za Maduro na moja ya mwanachama machachari mpinzani María Machado zilionyesha tofauti zao za kisera kati ya chama tawala na chama kikuu cha upinzani inapohusu Palestina na Israel.

"Long live free Palestine!"
Nicolás Maduro
"Our struggle is Israel's struggle"
María Machado

Je, huenda hii ni sababu nyingine inayofanya Elon awe na vita kali dhidi ya Maduro?


Ikumbukwe kuwa Marekani kwa kutumia CIA imeshagharamia majaribio kadhaa ya kimapinduzi nchini Venezuela lakini ikashindwa kwa aibu.

Hii ni historia fupi ya mapinduzi ya kijeshi yaliyowahi kufanywa Latin America kukiwa na mkono wa Marekani:


20240731_060126.jpg
  • Brazili: CIA iliunga mkono mapinduzi ya 1964 yaliyompindua Rais João Goulart na kuweka udikteta wa kijeshi wa mrengo wa kulia.​
  • Bolivia: CIA ilihusika katika mapinduzi mwaka 1971 ambayo yalimuondoa madarakani Rais Juan José Torres.​
  • Chile: CIA ilishiriki katika mapinduzi ya 1973 yaliyompindua Rais Salvador Allende.​
  • Argentina: CIA iliunga mkono mapinduzi ya 1976 ambayo yaliondoa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia na kuanzisha udikteta wa kikatili wa kijeshi.​
  • Ecuador: CIA ilifanya operesheni za siri nchini humo kati ya 1960 na 1963.​
  • Panama: CIA iliunga mkono uvamizi wa 1989 ambao ulimpindua Jenerali Manuel Noriega.​
  • Haiti: CIA iliunga mkono mapinduzi ya 1991 yaliyompindua Rais Jean-Bertrand Aristide.​
  • Venezuela: CIA ilihusika katika jaribio la mapinduzi ya 2002 dhidi ya Rais Hugo Chávez.​
Wavenezuela wenyewe ndio wana haki ya kuamua nani awe kiongozi wao na wala sio mataifa ya Magharibi.
 
Nchi za america ya kusini hazina tofauti na za ki Afrika kwenye udikiteta, na uhuni wa kwenye chaguzi!! Madulo wananchi wamemchoka hasa na siasa zako, ambazo zinqzidisha umaskini tu kwa raia wake!!
Tatizo demokrasia kwa nchi masikini haina maana angalia viongozi wa kidemokrasia wanasigni mikataba ya kimangungu na mabaperi.

Ukiona sehemu western wanapigania demokrasia ujue kuna jambo nyuma ya pazia ndo maana hawana habari na kagame na Museveni au kingi mswati
 
Ukiona sehemu western wanapigania demokrasia ujue kuna jambo nyuma ya pazia ndo maana hawana habari na kagame na Museveni au kingi mswati
Umesema vyema.

Popote pale ambapo wana kibaraka wao madarakani hata aibe kura au akae madarakani kwa miaka mingi hautawasikia wakisema kuna ukandamizaji wa Demokrasia au kiongozi huyo ni dictator

Nchi za Magharibi zimejaa unafiki sana
 
Madulo wananchi wamemchoka hasa na siasa zako, ambazo zinqzidisha umaskini tu kwa raia wake!!
Baada ya Marekani kushindwa kwenye majaribio ya mapinduzi nchini Venezuela, wakaiwekea vikwazo vikali sana vya kiuchumi Venezuela na hapo ndipo uchumi wa taifa hilo ukaanza kutetereka.

Sio sera ya Maduro wala mtangulizi wake Hugo Chávez ni ukandamizaji unaofanywa na Marekani.

Wanachotaka hawa Marekani wamweke mtu wao madarakani ndio maana wanamuunga mkono sana Edmundo González kama walivyofanya Argentina kumweka Javier Milei.

Marekani ndio baba wa michezo michafu kwenye siasa za dunia
 
Wasingekuwa na mafuta wangeishi kaa amani kama Mongolia. Kosa lao ni kuwa na mafuta na kuwa karibu na USA.
Poleni sana Venezuela
 
Baada ya Marekani kushindwa kwenye majaribio ya mapinduzi nchini Venezuela, wakaiwekea vikwazo vikali sana vya kiuchumi Venezuela na hapo ndipo uchumi wa taifa hilo ukaanza kutetereka.

Sio sera ya Maduro wala mtangulizi wake Hugo Chávez ni ukandamizaji unaofanywa na Marekani.

Wanachotaka hawa Marekani wamweke mtu wao madarakani ndio maana wanamuunga mkono sana Edmundo González kama walivyofanya Argentina kumweka Javier Milei.

Marekani ndio baba wa michezo michafu kwenye siasa za dunia
Hata hivyo hizo sera zao zimeshindwa kufanya kazi, cuba iko wapi? Hata huyo maduro ni suala la muda tu, kwani misimamo yake sio kama ile ya mwanzo anachukua madaraka,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom