Elimu ni zaidi ya kutafuta pesa mataifa makubwa yameendelea na kuwa na matajiri wakubwa kwa kuwa kuna planners wazuri mfano hakuna tajiri au maamuma aliegundua kuwa mtwara kuna gesi na ina cubic feet ngapi ila ni wabobezi na watafiti waliofanya kazi hiyo na baadae matajiri au wenye mitaji ndio watawekeza na kuongezea utajiri wao, mfano mwingine ni kule Shinyanga ambako Dr. Williamson mtaalam wa Geology ndie alifanya utafiti wa kina juu ya madini yaliopo Mwadui, matajiri wengi wakubwa duniani wanajihusisha na mafuta, madini kama chuma au watengeneza machine mbali×2 wanatumia wasomi wabobez ktk uzalishaji wao, hata Bakhresa anatumia vijana wasomi kufanya utafiti kujua mahitaji ya customers hivyo matajir wakubwa wanaujua umuhim wa wasomi, hata Regnard Mengi pamoja na kuwa yeye ni msomi ila haachi kutumia bussness plan za wasomi wengine hivyo ikitokea elimu au wasomi wakafutika ktk hii dunia basi matajir watapungua ndo maana nchi zenye wasomi wengi kama Russia, USA, England ndizo zenye matajiri wa kutisha duniani na nchi zisizo na wasomi ndizo zenye mafukara wengi mfano mwingine hapa africa matajir wengi wanapatikana Nigeria, South africa, Misri, n.k na utagundua hizi ndo nchi zenye wasomi wengi, na kama kuna tajiri ambae hahusishi wasomi basi anafedha zakubadirishia mboga au ataishia kuwa tajir ktk kijji chake. Hitimisho; utajir na elimu ni Pete na chanda na penye utajir pana elimu na penye elimu pana utajir na kinyume chake