Mbona mnakuwa wakali sana kila anayehoji haya mambo!!?
Lengo ni kujadiliana na pengine kuishauri serikali namna bora ya kutekeleza hii sera ambayo kwa vyovyote vile ni nzuri na hakuna anayeipinga.
Na tukunbuke pia kuwa utekelezaji wake ndo tu umeanza na ni kitu kilichokuwa nje ya utaratibu wa kibajeti. Kwa hiyo ni lazima tu kutakuwa na mapungufu ya hapa na pale ktk utekelezaji wake!!
Binafsi nimemuelewa mleta hoja na
wewe pia nimekuelewa.
Ni kwamba hizi 18.6bn ni kwa ajili ya
shule zote za msingi na sekondari kwa
mwezi desemba, 2015.
Kwa mujibu wa magawanyo wa fedha
hizo ni kwamba;
Kwa sekondari kidato cha I -IV kila mwanafunzi atalipiwa na serikali
Tshs. 45,000 kama fidia ya ada ambayo ilipaswa kulipwa na mzazi wa mwanafunzi.
Kwa shule za msingi kila mwanafunzi atalipiwa na serikali Tshs. 10,000= kwa mwaka.
Kwa utaratibu wa serikali ni kwamba hizo fedha zitakuwa zinatolewa kila mwezi kwa kutumwa moja kwa moja ktk shule husika, hazitalipwa kwa mkupuo mmoja!!
Sasa kwa mfano kama shule ya sekondari X ina wanafunzi 145 kidato cha I - IV (nyingi ya shule za vijijini zina idadi ya wanafunzi inayo range kati ya 90 - 350) maana yake shule hii shule ktk mgawa wa mwezi desemba imepata;
45,000 ÷ 12 × 145 = Tshs. 543,750/=
Maana yake haya ndiyo matumizi ya shule hii kwa mwezi January, 2016 mara shule zitakapofunguliwa!!
Hii ndiyo hoja nadhani nilivyomuelewa mleta mada. Swali lake ni kwamba, hizi pesa zinatosha kuendesha shule kwa mwezi??
Mimi binafsi sina jibu ktk swali hili kwa sababu kila shule ina mahitaji na bajeti yake ya mwezi, muhula na kwa mwaka mzima. Ninachoweza kusema ni kuwa inategemea na shule.
Kwa sababu kuna shule zina wafanyakazi (casual labours) ambao hawako ktk payroll la serikali na hulipwa na shule kama walinzi, wahudumu wa ofisi nk kulingana na vyanzo vya mapato ya shule husika iwe ni kutoka EK au michango ya wazazi kwa wakati ule kabla ya sera ya elimu bure kuanza. Pia kuna shule zingine vijijini hazina walimu wa kutosha especially wa sayansi na shule huajiri parttime teachers ambao hulipwa posho ya kati ya Tshs. 150,000 hadi 250,000 ili wanafunzi hawa wafundishwe
Hii kitu ni halisi wala si kuandika tu hapa. Mimi hapa naandika nikiwa Shinyanga na natembea sana vijijini. Kuna shule za sekondari ziko kwenye very remote areas na mazingira ni magumu sana to the extent kwamba walimu hupakimbia huko kila wanapopangiwa. Kuna shule moja iko wilaya ya Kishapu inaitwa Paji ina wanafunzi 123 wa kidato cha 1 - 4 na walimu 5 wote wa masomo ya Arts na language hasa Kiswahili ns History, Geography na Civics. Hakuna mwalimu wa Mathematics, physics, Biology na Chemistry.
Anachofanya mwalimu mkuu alikuwa anatafuta vijana wa walionaliza kidato cha sita na kusaidia kufundisha. Na huwezi amini kuwa kila mwaka mwalimu huyu hupeleka vijana wawili au watatu kidato cha tano (A'level). Sasa serikali ime consider hii kitu??
Na kuna shule zingine wala hazina watu wa namna hii kwa sababu kama ni walinzi au muhudumu wa ofisi ama mtunza bustani wote wanalipwa na serikali. Kwa hiyo ni wazi, shule kama hii pesa kama hii inaweza kutosha tu kwa mwezi japo kwa kubanana sana!
Kwa hiyo hii 18.6bn ni nyingi kwa kutamkwa kwa pamoja lakini zikishagawanywa mashuleni, picha halisi ya kitakachokwenda ktk kila shule ni kama nilivyoonesha hapo juu na kwa hakika kuna shule zinaweza kupata hata Tshs. 150,000 tu kwa mwezi!!!
Dah! Kuna watu wanakurupuka sana. Sijui huyu mleta mada kaandika wakati amepakatwa au ameinama! Yaani nawaza tu wadau.
mkuu hiyo hesabu yako umeipigaje, maana zimetolewa bilioni 18 na point, wewe hiyo laki mbili umegawanyaje hadi kuipata?