KWELI Elia Mpanzu kuanza kucheza hatua za Makundi inategemea na kufunguliwa kwa dirisha la usajili na ratiba ya kuanza makundi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna hili suala la Kuwa Mpanzu amesajaliwa Simba tayari japo bado haijaw wazi ila jambo linalonipa utata ni tarifa z kuwa atacheza kuanzia hatua ya makundi kwa kuwa dirisha dogo litakuwa limeshafunguliwa huku wengine wakisema haruhusiwi kucheza hatua ya makundi.

Msaada wenu wakuu mtupe ukweli wake

1727257294515.png
 
Tunachokijua
Elie Mpanzu Kibisawala ni mchezaji wa mpira wa miguu, anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, alizaliwa 1 Januari 2002 huko Kinshasa.

Siku kadhaa zilizopita ilidaiwa Clbu ya Simba SC ilikuwa kwenye mpango wa kumsajili kutoka kutoka kwenye klabu aliyokuwa akiichezea ya AS Vita kabla ya kusikika taarifa nyingine kuwa Menejimenti na timu ya Mpanzu wameamua aende Ulaya, Kwenye timu ya KRC Genk iliyoko Uholanzi kufanya majaribio ili akifanikiwa aweze kusajiliwa huko. Mara baada ya taarifa hizo, ilisikika tena kuwa Mpanzu hakuwa amefanikiwa kwenye majaribio aliyokuwa amekwenda kuyafanya huku sababu rasmi zikiwa hazikutajwa.

Baadaye tetesi za kumhusisha na Simba zilianza tena huku zikidai Simba imemsajili, tetesi hizo ziliongezwa kasi na nguvu mara baada ya Mpanzu kuonekana uwanjani, Benjamini Mkapa, ambapo Simba ilikuwa ikicheza na Al Ahly Tripoli Mechi ya mtoano kutafuta nafasi ya kuingia makundi kwenye kombe la Shirikisho mechi iliyochezwa Septemba 22, 2024.

Tetesi za Usajili wa Mpanzu kwenye klabu ya Simba Sc zikiwa zimepamba moto, Kumeibuka hoja kuwa iwapo ikawa kweli Simba imemsajili Mpanzu basi Simba itaruhusiwa kumtumia kwenye mechi za makundi huku wanaodai ivyo wakiwa na sababu kuwa Mpanzu hajacheza mechi yoyote ya CAF na pia kutakuwa na dirisha la usajili ambalo litamuwezesha kusajiliwa.

Wengine wakisema haiwezekani kwa sababu hakuna dirisha la usajili hivi karibuni, dirisha la usajili litakuta mechi za makundi zilishaanza kuchezwa.

Ukweli ni Upi?

JamiiCheck imepitia kanuni za CAF na kubaini kuwa ili mchezaji aweze kuichezea klabu husika anatakiwa kuwa sehemu ya kikosi kinachoshiriki Ligi Kuu ya Nchi husika. Aidha, Awali taarifa zilizokuwepo ni kuwa Hatua ya Makundi ya CAF 2024/25 ilipangwa kuanza Oktoba mpaka Desemba, 2024.

• Hatua za Kikundi: Oktoba – Desemba 2024
• Hatua ya Mtoano: Machi – Mei 2025

Ikiwa itakuwa hivyo inamaanisha Elia Mpanzu hata kama amesajiliwa na Simba hataweza kuichezea timu hiyo hadi atakapopitishwa rasmi kuwa mchezaji wa Simba katika dirisha Dogo la Desemba.

Kwa kipengele hiki ni dhahiri kinaibana Simba kumtumia Elie Mpanzu kwenye mechi za CAF hata kama wangekuwa wameinasa saini yake kama ambavyo taarifa zinadai, kwani dirisha la usajili kwa timu za ligi Kuu haliko wazi kwa sasa.

Hata hivyo kuna dalili huenda kwa msimu huu kunaweza kuwa na mabadiliko ya ratiba kwani, Ukitazama Wikipedia inaonesha kuwa Hatua ya Makundi imepangwa kufanyika Novemba 28, 2024 hadi Januari 19, 2025

Ikiwa ratiba itakuwa hivyo inamaanisha Mpanzu akisajiliwa Simba rasmi anaweza kukosa mechi mbili au tatu za mwanzoni, kisha akaendelea kucheza mechi zinazofuata.

Aidha, kwa upande wa CAF, Vyanzo rasmi vya CAF vinaishia kusema Droo ya Makundi itafanyika Oktoba 7, 2024 bila kufafanua ratiba kama ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu huu ambapo walisema Hatua YA Makundi ni Oktoba – Desemba

JamiiCheck iliwasiliana na Klabu ya Simba SC kupitia kwa Msemaji wake Ahmed Ally, ambaye amesema

“Kuhusu mchezaji mpya kwenye usajili wa Simba kucheza Hatua ya Makundi inategemea na Hatua ya Makundi itaanza lini, msimu uliopita Hatua ya Makundi ilianza Desemba na Dirisha la Usajili lilikuwa limeshafunguliwa, msimu huu Hatua ya Makundi inaweza kuanza Oktoba 2024"

"Ikiwa itaanza Oktoba Dirisha la Usajili litakuwa bado halipo wazi, hivyo automatic uwezekano wa kuongeza mchezaji hapo haupo, ikiwa Hatua ya Makundi itaanza Desemba na tukasajili mchezaji wakati wa dirisha dogo basi ataungana na kikosi kikiwa tayari kwenye michezo".
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom