East Africa Radio, mnakwama wapi?

Gini

JF-Expert Member
Oct 11, 2018
398
385
East Africa Radio
Tatizo ni nini, mnakwama wapi?
Na Mwl Sylvester, George Wambura (PG)

East Africa Radio, ikiwa ni miongoni mwa stesheni ya Radio iliyopata kuwa na watangazaji wenye vipaji pamoja na DJs wakali sana na kujizolea umaarufu na kusikilizwa sana na vijana pamoja na wasikilizaji wa rika zote. Vipindi vya rika zote vilitaradadi, muda ulipangwa ukapangika, radha ikasikika masikioni mwa wasikilizaji. Jingles zikapikwa zikapikika, kale ka-jingle ka East Africa Radio ALL HITS STATION, kutokea Mbezi Beach sauti ya mdada mwenye kuitwa Yeranda ikinakishi katika tangazo akisema My name is Yeranda from (kutokea) Mbezi Beach nasikiliza East Africa Radio East Africa Radio huku tangazo hilo likiwa limesukwa kiufundi kiasi cha kutamani kila wakati wapige jingle ilimradi tu uisikie sauti ya Yeranda. Ilikuwa ni All Hits Station kweli, zilipigwa kopo to kopo, ngoma kali si kitoto, vipindi kama #Saturday HotMix siku za Jmosi mishale ya saa 4-7 usiku, show ikisimamiwa na Bahati Abdul, kijana mwenye utangazaji smart hivi huku kwenye 1&2 yupo DJ Mackay baadae anaingia DJ 45 King, kwa mtaa vijana wa Social Media Team nao hawakuwa nyuma, wako kwenge meseji, watapiga simu kutoa shout out zao kwa wana.

Achana na akina Salama Jabir, DJ Bush baby, Jimmy Kabwe, Sister dread (baby kabae), Ssebo mzee wa Homa TVE, Maimatha wa Jesse n.k, East Africa News ikisomwa na akina Magreth Richard, Prudencia Gerald Mosha kama nitakuwa sijakosea jina na watangazaji wengine, walitangaza kwa uzuri wake. Pindi kama PB Planet Bongo kila Jmosi mida ya 4-6 mchana, hapa Dullah Mjukuu wa Ambua kwenye mashine DJ Mafuvu beiibyy, noma ikawa noma, hakuna mwana alikosa pindi mida hiyo, fuvu beiby Master wa Turntable kisanga kisangani, saa ya kwanza ya ngoma laini kisha inafuatiwa na ngumu nyeusi (Hip Hop). The Request show, PowerJams, The late night, The Cruise chini ya Steve kafire nani alikuwa anaikosa hii.

Je, shida ni nini? Watangazaji wakasepa na kujiunga na radio nyingine kama CloudsFM huku wakiiacha EARadio ina mapengo mapengo yaani kibogoyo, Sister dread (Babbie Kabae), Musa Hussein, George Bantu, Joshua Edmund, Mina Ally, Mamii beiby, Kenedy The Remedy, Michael Lukindo, DJ Sinyorita n.k. Raia wanajiuliza, shida ni masilahi duni, au uongozi?

Wakati DJ Mafuvu anafanya yake, zile kelele katika kipindi cha PowerJames nasikia Nasa Kingu anampiga marufuku, nilishangaa sana, yaani dj asiweke mbwembwe wakati anasugua santuri eti kelele wakati hizo fujo ndo raia wanapagawa nazo, yaani bila kelele pindi linakuwa doro, venye Fuvu beiby akisema "yeeeeeh fuvu beibyy" ndo mizuka kwa wana inapanda na huwaambii kitu, mwishowe kipindi kikakosa radha baadae fuvu baby akasepa. Kuna wakati watangazaji walizuiwa hata kutaja account zao za mitandao ya kijamii hewani, yaani SamMisago kwa mfano haruhusiwi kuitaja account yake ya Facebook, twitter au Instagram hewani akiwa kwenye kipindi, wakati radio nyingine wanafanya. Unajiuliza uongozi una shida gani..

Sina hakika sana kama East Africa Radio wana account ya Instagram. Muda si mrefu Zembwela amesepa, moja ya watangazaji alikimudu kipindi cha Super Mix, nani alikuwa hasikilizi SuperMix, kipindi kilichozifufua kero za jamii na kufanyiwa kazi, leo hayupo na kipindi wamekibadilisha jina na kukiita Mama Mia ila sidhani kama kinafanya vyema, David Rwenyagira, mmoja wa watu alikuwa anaendesha ndinga ya East Africa Drive (EA Drive) sambamba na Ian Dialo nae amesepea Wasafi na nasikia sababu ni uongozi na mambo kadhaa.

Changamoto nyingine ni transmission, hili ni tatizo kubwa, yamkini linafanyiwa kazi lakini kiushindani ni tatizo. Usikivu wa East Africa Radio hususani kwa Dar es Salaam na mikoani ni shida tena kubwa, uko kariakoo, ukiwa Pugu au Majohe huko radio inakata, au uko Banana usikivu mbovu. Katika dunia ya ushindani ni lazima kuendana na kasi ya ubora ili ku maintain soko (wasikilizaji). Badilisheni mitambo ikiwezekana kama ku repair inashindikana. Soko liko Dar usipoishika Dar umefeli. Ukitokea Ubungo unaenda Kibaha ukifika Mbezi kwa mbele kidogo kama ulikuwa unaisikiliza East Africa Radio ndo basi unaiacha, ila ukiwa unasikiliza CloudsFM, kutokea Dar utafika nayo Kibaha with the same frequency, unajiuliza EARadio wanakwama wapi?

Inawezekana nguvu ya pesa ikakutoa kwenye reli, mfano Wasafi FM kuchukua watangazaji wazuri, ila kwa East Africa Radio nadhani kuna tatizo zaidi, uongozi uliangalie hili. Uongozi ujiulize, kwa nini watangazaji wa Clouds FM hawaondoki pale, unaweza kukuta mishahara haipishani sana lakini kuna vitu uongozi unawafanyia, kuanzia kuwa brand watangazaji na wafanyakazi kiujumla. Wanawa promote kiaina mathalani kuwaongezea visenti hivi kila awamu au hata kuwapa mikopo nafuu kumudu na kuweza kupambana na maisha, katika mazingira kama haya mfanyakazi hawezi ondoka kirahisi, maana unakuwa umemuinua kiasi fulani. Je, uongozi wa East Africa uko serious kubeba na kiyafanyia kazi maoni ya watangazaji, wanapopeleka mawazo chanya aidha juu ya nini kiboreshwe katika muktadha wa kuhuisha maenedeleo ya mafanikio, je uongozi unafanyia kazi?

#Studio, sitaki kuamini kuwa uongozi umeshindwa kuona hata umuhimu wa kuwawekea watangazaji wake na wageni TV ya kisasa Studio ukiacha studio isiyotosha kukaa hata watu watatu. Tv kichogo inchi 14 ndiyo mmeanza nayo miaka ya marehemu Rodney Mutie Mengi, hamshindwi ku install hata TV ya inchi 100 ila kwa sasa hata ya inchi 40 au 32 basi itatosha. East Africa ni brand kubwa, naamini mna uwezo wa kuwa na studio kubwa na ya kisasa yenye muonekana bomba na wa kuvutia sana. Clouds FM & Wasafi FM wana Studio za kisasa mno, igeni kitu kizuri, sio dhambi. Mazingira ya kazi ndiyo kichocheo namba moja cha kuipenda kazi mbali na masilahi.

Mbali na vipindi vinafanya vizuri kama Kipenga, niseme tu Ibra Kasuga, Tigana na George David Kampista wanafanya vizuri, sitegemei kumuona Ibra Kasuga akiondoka maana dogo anajua, yaani akiwa anatangaza na kuchambua michezo una feel lile vibe la kispoti yaani. King Smash, Dullah Mjukuu wa Ambua, Jr, Frida Amani, Ian Dialo wako vizuri, sitegemei kusikia wamesepa.

MWISHO kabisa, malizaneni na Diamond Platinumz, aliyependekeza kutopiga ngoma za Diamond aliwaingiza chaka sana, Mond ni brand, kwa sasa hamuwezi kushindana nae hata kidogo zaidi yeye ndiye anauza media yako. Yaani Diamond hahitaji promo na media tena zaidi media ndiyo zinatakiwa kuwa karibu nae ili azipeleke mbali kimauzo au kibiashara zaidi. Babu Tale aliwahi kusema kuwa shida ilianzia kwenye tuzo mlizoziandaa, bahati mbaya tuzo hazipo tena, kukubali kushindwa sio udhaifu bali kuonesha uungwana. Malizaneni mfanye kazi. Andaeni matamasha, muifanye Radio kuwa ya vijana, matamasha yatawaletea pesa maana makampuni yatakuja kudhamini, kama ni wataalamu wa kutengeneza ideas za namna gani ya ku run radio muajiri, waandike proposal za namna gani mtafanya matamasha, yawe ya kiburudani na msibague wasanii. Yako mengi sana ila nitapata kuyaandika na kuwashauri zaidi katika andiko langu kuhusu EAST Africa TV,tchao until next time!
 
Wewe unaonekana Ni mdau mkubwa Sana atamimi hiyo la diamond wananishangaa Sana pia wanastudio low quality ingawa ni media inayozalisha vijana wengi potential.
 
ila EA me naona wamefeli sana kwenye TV kuliko radio, hawana ubunifu kabisa kwenye vpind vyao...mavipind ni yale yale, muonekano uleule miaka nenda rudi.inshort wanaboa.
 
Bro unechambua vizuri Sana.Shida ni management na ukoloni ndani Yake.Mfano late Ruge na Clouds FM wamewajenga staff Kuwa na viproject vyao na uongoz una support.Clouds ukiwa na tangazo na ni staff kuna discount nenda EA radio hakuna hayo mambo.EA ndio ilikua radio ya vijana back in the days walikua wanaandaa Matamasha Leo jii.Mafuvu kilichomtoa ni bureaucracy za kijinga.EA radio Madj wanapewa playlist,Kama wimbo Haupo kwenye playlist hutakiwi kuupiga,Yeye akawa anapiga baada akaon a ujinga aka resign
 
Bro unechambua vizuri Sana.Shida ni management na ukoloni ndani Yake.Mfano late Ruge na Clouds FM wamewajenga staff Kuwa na viproject vyao na uongoz una support.Clouds ukiwa na tangazo na ni staff kuna discount nenda EA radio hakuna hayo mambo.EA ndio ilikua radio ya vijana back in the days walikua wanaandaa Matamasha Leo jii.Mafuvu kilichomtoa ni bureaucracy za kijinga.EA radio Madj wanapewa playlist,Kama wimbo Haupo kwenye playlist hutakiwi kuupiga,James akawa anapiga baada akaon a ujinga aka resign
Ni wao kuona umuhimu wa ku deal na changamoto hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ea radio walikuwa vizuri sana..i wish warudi kama zamani..Zinapigwa hits hatari,vipindi vina watangazi best kabisa

Wanajua sana kuspot talent halisi za utangazaji..no wonder watangazaji wengi wa Clouds ambao hawajawa raised na Clouds wametoka Ea radio.
 
Ea radio walikuwa vizuri sana..i wish warudi kama zamani..Zinapigwa hits hatari,vipindi vina watangazi best kabisa

Wanajua sana kuspot talent halisi za utangazaji..no wonder watangazaji wengi wa Clouds ambao hawajawa raised na Clouds wametoka Ea radio.
Wajitafakali shida ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom