KWELI Dunia ni Duara na siyo diski tambarale

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kumekuwa na maswali Mengi kuhusu safari za Ndege kwanini hazisafiri kufuata straight line kutoka bara moja kwenda jingine?
Na hivyo wataalamu wa mambo kuja na theory ya dunia ni flat( kama sarafu ya mia mbili inapokuwa chini)
Naomba mnisaidie kwenye uhakiki.


 
Tunachokijua
Dunia ni sayari ya tatu kutoka kwenye jua, sayari hii inashika namba tano kwa ukubwa katika sayari zinazopatikana katika mfumo wa jua (solar system), na ni sayari ambayo ina viumbe hai tofautitofauti ikiwemo binadamu, mimea na wanyama wengine. Dunia imezungukwa na maji kwa asilimia 71 na nchi kavu kwa aslimia 29.

Mvutano kuhusu umbo la dunia
Kumekuwepo na mvutano mkubwa kuhusu umbo la dunia, madai mbalimbali yamekuwa yakiibuliwa mathalani kuna kundi linalodai dunia ina umbo la yai, wapo wanaodai kuwa dunia ina umbo la tufe na wapo wanaoamini kuwa dunia ni duara lililo tambarale (flat disk). Makundi yote haya yanayoibua madai haya wamekuwa na sababu za kuyatetea madai yao.

Mfano wa dunia kama ingekuwa diski tambarale. credit: Space.com

Tovuti ya Geography wanaeleza kuwa kwa hivi sasa hoja ya wazee wa kale kuwa dunia ni tambarale imekosa mashiko. Mabaharia wa zamani waliamini kuwa dunia ni diski tambarale (flat disk) kwani walipokuwa baharini mbali na nchi kavu, hawakuweza kuona nchi kavu badala yake waliona anga linagusana na bahari na hivyo kuwafanya waamini kuna ukingo hivyo wakawa hawaendi mbali zaidi kuhofia meli zao zisianguke kwenye ukingo wa dunia kama wangeenda mbali.

Ramani ya dunia ikiwa katika umbo la tambarale iliyochorwa na Orlando Ferguson 1893.
Credit: Wikipedia


Baada ya madai hayo kuwepo kwa muda mrefu baadaye wakaja watafitii wengine waliobainisha kuwa dunia si diski tambarale bali ni duara, kwa mara ya kwanza katika karne ya 6 Kabla ya Kristo (KK) mwanafalsafa wa kigiriki Pythagoras aliona sayari nyingine ipo katika muundo wa duara kupitia hadubini yake aliyokuwa amevumbua na hivyo akaamini kuwa dunia pia itakuwa duara.

Katika karne ya 5 KK, Anaxagoras alibainisha kuwa wakati wa kupatwa kwa mwezi kivuli kilichopinda cha dunia kilikuwa kikisogea kwenye uso wa mwezi na hivyo ikamfanya afikirie kuwa dunia ni duara.

Tovuti ya Geography wanaendelea kueleza kuwa dunia ni duara lakini si duara kamili bali ni duara ambalo limebonyea kidogo kwa juu (kaskazini) na kwa chini (kusini) na limetanuka kwa pembeni (kwenye mstari wa Ikweta). Kipenyo cha pola cha dunia (kutoka juu hadi chini) ni kilomita 12,714 na kipenyo cha ikweta ni kilomita 12,756 hali inayopelekea dunia kutokuwa duara kamili. Dunia inapozunguka nguvu ya nje huifanya kutanuka kidogo kwenye ikweta na kuwa na hali ya bapa juu na chini.

Attachments

Hebu tueleze hio gravity maana yake na kwanini maji bahari ambayo yana nafasi kubwa kuliko ardhi haya dondoki kama yanavyoonyeshwa kwenye huu mfano wako kama ingekuwa tambarare...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…