Mnyama huyu duma (Acynonimus jabatus) anatufurahisha kwa mbio zake anapokimbiza mawindo yake. Anamkimbiza mnyama spidi kali na kumpiga kofi na akianguka humbana mdomoni au shingoni kumnyima pumzi hadi afe. Udhaifu wa duma ni woga. Akiua mnyama lazima amle haraka kabla ya wengine kama simba, chui, fisi na mbweha hajaja kumnyanganya. Akitishiwa kidogo hukimbia na kuacha mawindo yake yaliwe na wavamizi hao. Kama hakuna mawindo ya kutosha ni wazi duma ataathirika kuliko wanyama wengine wanao winda kama simba, chui, mbweha, mmbwa mwitu na wengine