Strictly Syrup
JF-Expert Member
- Aug 4, 2013
- 1,220
- 1,793
Rapper kutoka Toronto, Canada, Drake, pamoja na rapper kutoka Atlanta, Georgia, 21 Savage wameshirikiana kuandaa album inayoenda kwa jina la "Her Loss." Album hii ilitarajiwa kuachiwa hewani mnamo 28-11-2022, lakini kutokana na maandalizi yaliokuwa wakiendelea, iliwalazimu kusogeza muda wa kutoa album hiyo, na kuiachia siku ya jana tarehe 04-11-2022, ikiwa ni wiki moja mbele tangu tarehe ya awali ya release.
Album hii ilitangazwa kwa mara ya kwanza katika video ya Jimmy Cooks, nyimbo ambayo Drake alimshirikisha 21 Savage (kutoka album ya Drake "Honestly, Nevermind") siku ya jumapili ya tarehe 23 Oktoba 2022, ikionyesha Jina la Album na tarehe ya kuingia mtaani.
FIRST IMPRESSIONS
Album hii imepokelewa vizuri, ingawa baadhi ya mistari katika wimbo wa "Circo Loco" imezua gumzo mitandaoni. Katika wimbo huo Drake amezunguamzia madai ya Megan thee Stallion kuwa "alipigwa risasi" mguuni na Tory Lanez mnamo August 20, 2020 na kuelezea kuwa Megan the Stallion alidanganya kuhusu kupigwa risasi na Tory Lanez, (This bitch lied bout gettin shot but she still a Stallion, She don't even get the jokes but she still smiling.)
Megan katika account yake ya Twitter, ikiwa ni masaa machache baada ya kuachiwa kwa album hiyo, aliandika katika jumbe mbalimbali (Tweets) zikionyesha majibu yake yaliyoashiria "Hasira, mfadhaiko na kusononeka" na kumtuhumu Drake kuwa ameonyesha tabia isiyo ya kiume, na kudai kuwa Tory Lanez alimu"abuse" na kusema wanawake wenye ngozi nyeusi wanapitia manyanyaso mengi.
Drake siyo msanii wa kwanza kumtuhumu Megan thee Stallion kuwa ni mwongo. Mapema mwaka huu rapper 50 Cent kupitia account yake ya Instagram alipost video ikionyesha mahojiano ya Megan thee Stallion ambapo Megan alikuwa analia na akisimulia jinsi alivyopigwa risasi na Tory Lanez huku akilia.
Mashabiki wengi wameifurahia album hii.
Kwa sasa inapatikana katika Streaming Platforms zote (Apple Music, Spotify, Amazon etc.)