GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,812
- 9,643
Kwamba, kwa kuwa Dr. Sulle kagundua kuwa Wamasai walioandamana Ngorongoro si Watanzania bali ni Wakenya wenye nia mbaya dhidi ya Tanganyika, inaonesha ya kwamba yeye yupo makini zaidi kuzidi vyombo vyetu vya dola.
Kama ndivyo, ni vizuri akakabidhiwa Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na ukuu wa usalama wa Taifa na TAMISEMI pia.
Soma Pia: Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
Yeye akiwa "bosi" wa TAMISEMI, UHAMIAJI, POLISI, na USALAMA WA TAIFA, hayo makosa ya wageni kuingia nchini kwetu kinyemela na kuhudumiwa kwa kodi za Watanganyika kwa miaka mingi bila kujulikana kuwa ni raia wa kigeni wenye nia mbaya na nchi yetu hayatajirudia!
Dr. Sulle akabidhiwe hizo idara haraka sana!