Dr. Slaa: Serikali ya Magufuli inaelekea kubaya, adai kunasa nyaraka

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
"Ingawa tunapinga utegemezi kutokana na utajiri wa nchi yetu lakini ni lazima tuangalie kuwa tunapinga kutokana na sababu zipi hasa na tutaathirika kwa kiasi gani"

Aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Willbrod Slaa amedai kunasa nyaraka muhimu zinazoonyesha jinsi Tanzania ilivyotengwa na mashirika muhimu ya misaada ya kijamii duniani, imefahamika.

Akiongea na vyombo vya habari vya new habari corporations, Dr. Slaa ameongeza kuwa nchi ya Tanzania inaweza kujikuta ikitengwa na wadau muhimu wa maendeleo kutokana na uchaguzi wa Zanzibar, sheria ya makosa ya mitandao na vikwazo katika uwekezaji. Dr. Slaa amedai kuwa na nyaraka muhimu zinazoonyesha kuwa huenda serikali ya Magufuli ikajikuta katika wakati mgumu zaidi huko mbelelni.

Aidha uchunguzi unaonyesha kuwa tayari serikali ya Magufuli imetengwa kwa kiasi kikubwa na wadau wa misaada mbalimbali ya kimaendeleo duniani huku mashirika muhimu ya uwekezaji yakiipa kisogo Tanzania kutokana na kile kinachoonekana kama Tanzania kuweka vikwazo vingi katika sekta ya uwekezaji kwa sasa.
 
Tuweke chanzo cha taarifa yako kabla ya kuchangia
 
Kila mtu ashaongelea hili, watu hawageuzi shingo.........ni mfululizo wa matukio yasiyo na kichwa wala miguu.......Ukweli ni kwamba wazungu ndio wanaendesha hii dunia, hatuna uwezo wa kujitegemea hata siku tatu wakiamua......Muhabe alilazimisha,Zimbabwe is no where, nchi inatumia USD kama currency yao kwa sasa, ila ndio hivyo ngoja watupige vizuri pengine tutaelewa ,Nyerere na maakili yake yote aligota akaamua kungatuka, kumbuka tulikuwa na kila kitu, sijui hii ya sasa iliyoliwa ikabaki Mifupa, ila Magufuli angeshirikiana nao hata kinafiki kwa kas hii hii tungefika mbali sana,
Tusubiri tuone, Muda utasema yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…