A-town
JF-Expert Member
- Oct 25, 2011
- 494
- 169
Akiendelea na ziara yake nchini Marekani ya kujifunza inayoItwa Vision Tanzania. inayolenga kutafuta ufumbuzi wa tatizo sugu la, Katibu mkuu wa Chadema Dr. wilibrod Slaa, jana ametembelea maeneo mbali mbali yanayoendana na Nishati. Moja ya maeneo hayo ni eneo kubwa la kutengeneza umeme wa upepo wind firm huko Indiana, linalotengeneza zaidi ya MW 550, pamoja na solar farm linatogengeneza kiasi cha MW 20. 

Vile vile Dr. Slaa ametembelea Chuo kikuu cha utafiti cha Purdue, kitivo cha Engineering ambako alijionea ubunifu na utafiti wa hali ya juu unaofanywa na wanafunzi pamoja na walimu wa chuo hicho. Kwa masikitiko makubwa, Dr. Slaa amesema kwamba, CHADEMA haina jinsi zaidi ya kutafuta mbinu mpya ya kuweza kuwaokoa watanzania kutoka kwenye shimo la umasikini na minyonyororo ya CCM. 

Rais Kikwete mwenyewe ameshakiri wazi kwamba hajui ni kwa nini watanzania ni masikini. Kwa hiyo kama hajui kwa nini Watanzania ni masikini, basi yeye na CCM, ni bora wakawarudishia watanzania nchi yao. Hii ndio sababu kubwa CHADEMA inahangaika kutafuta ufumbunzi

Tatizo la umeme ni mradi wa mafisadi ndani ya CCM. Tanesco linafirisika kutokana na mapato yake kulipia mafuta mazito na makampuni kama Symbion.

Ziara hiyo ya Dr. Slaa ambayo imeratibiwa na Umoja wa vyuo vikuu vikubwa marekani, imelenga zaidi kutafuta ufumbuzi wa matatizo sugu yanayomkabili mtanzania.
Dr. Slaa na CHADEMA wamedhamiria kuliokoa Tanzania kushirikiana na mataifa pamoja na mashirika ambayo yatafanya biashara ya usawa na Tanzania. Hatutaki rasilimali zetu kupelekwa kuendelea mataifa mengine wakati tunarudishiwa bidhaa bandia. 

Inafika muda binadamu anayenyanyaswa anasema basi. Watanzania wamechoka !