Tunashukuru kwa kutupatia makusanyo ya na matumizi ya serikali kila mwezi, kweli ni wazo zuri ila mbona tunaona makusanyo ya TRA pekee, maduhuri mengine ambayo hayapiti TRA yenyewe yanakusanywaje? kuna mirabaha ya madini huingia moja kwa moja wizara ya nishati na madini, yakowapi? tozo na ada za mamlaka mbalimbali kama ewura tcra sumatra hayo maduhuri yako wapi? unapotuletea mapato ya TRA pekee huo ni usanii wa mchana na kutaka kutupumbaza watanzania na vikodi kidogo, tunataka kuona bakuli lote.
Yapo mapato yatokanayo na bomba la gesi pamoja na bomba la mafuta la Tazama, magawio ya hisa za mashirika ya umma kama NMB, CRDB BP NHC nayo yakowapi? Ada za bandarini ziko wapi? Mapato ya vivuko vya magogoni na busisi nayo yako wapi?