DP World, Ni Kweli Wana Uwezo Mkubwa. Lakini Ndiyo Sababu Ya Kuwapa Kila Kitu Bure?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,482
46,516
Hii nchi kuna wakati unawasikiliza watu wanaotoa sababu kwa nini mkataba wa bandari yetu, kati ya Tanzania na DP World, ni mzuri wakati umekaa hovyo kabisa, majibu wanayotoa, unajiuliza na kushangaa. Unashangaa zaidi ukiambiwa nafasi ya huyo mtu huko serikalini. Unashangaa alipewa nafasi hiyo kwa vigezo gani! Labda nafasi hiyo ama ilihitaji mtu mjinga, mwongo na mnafiki. Ndiyo alipewa huyo mtu.

Mtu anasema eti DP World wapewe bandari zote za Tanganyika kwa sababu DP World wana uwezo mkubwa, wanafanya biashara hiyo kwenye mataifa mengi! Alah! Una akili wewe kweli? Yaani tukubali DP World apewe bandari zetu:

1) kwa muda asiojulikana
2) tusiwe na uwezo wa kumkaribisha mwekezaji mwingine hata kwenye bandari nyingine
3) tuwahamishe watu na taasisi zetu kwa gharama zetu, alimradi tu DP amelihitaji eneo ambalo watu au taasisi zetu zipo kwa sasa
4) tusiwe na gawio lolote kwenye faida atakayopata DP licha ya kwamba na sisi tayari tumewekeza matrilioni ya pesa kwenye bandari hizo hizo, wala siyo kwamba DP anakuja kujenga bandari mpya
5) tusimtoze kodi zilizopo kwa mujibu wa sheria, eti yeye awekewe zilizo ndogo na chache;

halafu mtu katika kuyajibu haya anasema, wapewe tu kwa sababu wana uwezo na ufanisi.

Hata katika maisha ya kawaida, wewe unaweza kuwa na familia yako, umezungukwa na familia nyingine, na uwezo wa hizo familia, aghalabu hutofautiana. Kuna familia zenye uwezo mdogo, familia zenye uwezo wa kati na familia zenye uwezo mkubwa. Kwa fikra za hawa wenzetu, ambao mimi nawaita wajinga na mafukara wa nafsi, wanaona ni halali yule mwenye familia yenye uwezo mdogo kukabidhi kila kitu alicho nacho ikiwa ni pamoja na ardhi au nyumba yake bure kwa familia tajiri kwa maelezo tu kuwa ile familia tayari itaboresha maisha ya ile familia maskini.

Kama.ni uwezo wa kifedha au tekinolojia ilio nao DP World, ndiyo kigezo cha kutoa bandari zetu bure, na sisi kupoteza hata ule uwezo wetu kama Taifa huru, kulikuwa na sababu gani ya hata kuwaondoa wakoloni? Wajerumani na Waiingereza, walikuwa matajiri kuliko sisi, walikuwa na tekinolojia kubwa kuliko sisi, walikuwa na mifumo bora ya kiutawala kuliko sisi, walikuwa na uwezo wa kusimamia uchumi kuliko sisi. Si tungesema tu wabakie kwa muda usiojulikana kwa sababu wana pesa na tekinolojia kubwa kuliko yetu, na hivyo wataboresha maisha yetu?

Watu wanahoji, kwa nini mkataba wetu na DP ni wa hovyo. Mtu mjinga, anajibu tena kwa kujiamini, eti mbona DP wamewekeza hata UK. Loh! Hivi huyu ana akili timamu? UK na DP wana mkataba wa kijinga kama huu wa kwetu?

Mtu anauliza kwa nini mkataba hauna ukomo. Mwehu anajibu, hii ni framework tu, ukomo utawekwa kwenye mikataba ya utekelezaji! Uwendawazimu wa hali ya juu. Yaani hajui hata maana ya framework agreement. Hajui mkataba huu ndio unaotoa uongozi kwa mikataba mingine, na siyo kinyume chake.

Watu wanauliza, bandari.ni suala la Muungano, kwa nini bandari za Zanzibar zimeondolewa? Kwa nini mkataba huu unakiuka articles of union? Wajinga wanakuambia, unajua DP itaajiri watu wengi!! Kwa hiyo huko Zanzibar hawahitaji ajira? Ama tuseme kuanzia sasa tumeamua kitu chochote kile hata kama kinakiuka sheria na katiba, ni ruksa, kwa sababu kitatoa ajira au kuleta pesa?

Watu wanahoji, kwa nini maamuzi ya kuwapa DP World bandari za Tanganyika, mchakato na maamuzi yake yamefanywa na Wizara ambayo inaongozwa na Wazanzibari pekee, licha ya ukweli kuwa wizara hiyo siyo ya Muungano. Wajinga hawa wanasema, mmeanza ubaguzi!!. Unajiuliza, mbona hawajampa mtanganyika yeyote uwaziri kule Zanzibar? Kwa hiyo tuseme kuwa Zanzibar ni wabaguzi sana kwa vile hakuna mtanganyika ambaye ni waziri au katibu mkuu kwenye wizara mojawapo ya Serikali ya mapinduzi Zanzibar?

Hivi hawa watetezi wa DP, tuamini ni wajinga, hawana akili, hawana uelewa, ni wanafiki au wamepofushwa na rushwa?

Watu wanaongelea ubaya wa mkataba, jibu, wanawapeleka akina Kitenge kuwahoji wafanyakazi wa DP Dubai kuhusu ufanisi na utendaji wa DP! Hivi tangu mjadala huu uanze kuna mtu amehoji au kulalamika kuwa DP hawana uwezo au hawana ufanisi katika biashara ya bandari? Wanatoa majibu ya kitu ambacho hakijaulizwa wala kuhojiwa na yeyote. Au wanayafanya haya kwa sababu hawana majibu kwa maswali ya msingj wanayouliza wananchi?
 
No sense and fabrications
 
No sense and fabrications

Mada haijaletwa kwaajili ya watu wa aina yako. Ni kwaajili ya wale wenye uwezo wa kutoa hoja/arguments tu.

Sehemu ambayo inahitaji hoja, ukiona huna uwezo wa kutoa hoja, ziwe za kupinga, kukosoa au kuipa nguvu, achana nayo. Sio lazima utumbukize vioja. JF siyo jukwaa la vioja. Ni jukwaa kwaajili ya watu ambao ni mentally capable.
 
Mkuu unao orodhesha hayana ushahudi wowote zaidi ya fikra zako tu, ndo maana unakua mkali........toa ushahidi kwa kuonyesha mikataba hiyo.
 
Halafu kwanini wapewe bila ukomo? Yaani mkataba hausemi ni wa miaka mingapi, na unakataza kujitoa hata Yesu akirudi.

Na kwa mwendo huu, sio tu bandari imeuzwa, bali imegawiwa bure kabisa!!!

Saa100 ajiuzulu kulinda heshima na utu wake
 
We are mentally castrated wallahi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hili, saa100 ajiuzulu kulinda heshima na utu wake, hii aibu haivumiliki. Hii thread imeniumiza sana.

B7FE1762-BEC9-4046-B8FA-880CF3D78DBD.jpeg
D40FDE02-5E6A-4F7C-9820-A8DDEE3E2C92.jpeg
 
Mi nahisi Kuna watu wanataka wauze hii nchi halafu waihame..wakachukue uraia nchi zingine huko.
 
Hii nchi kuna wakati unawasikiliza watu wanaotoa sababu kwa nini mkataba wa bandari yetu, kati ya Tanzania na DP World, ni mzuri wakati umekaa hovyo kabisa, majibu wanayotoa, unajiuliza na kushangaa. Unashangaa zaidi ukiambiwa nafasi ya huyo mtu huko serikalini. Unashangaa alipewa nafasi hiyo kwa vigezo gani! Labda nafasi hiyo ama ilihitaji mtu mjinga, mwongo na mnafiki. Ndiyo alipewa huyo mtu.

Mtu anasema eti DP World wapewe bandari zote za Tanganyika kwa sababu DP World wana uwezo mkubwa, wanafanya biashara hiyo kwenye mataifa mengi! Alah! Una akili wewe kweli? Yaani tukubali DP World apewe bandari zetu:

1) kwa muda asiojulikana
2) tusiwe na uwezo wa kumkaribisha mwekezaji mwingine hata kwenye bandari nyingine
3) tuwahamishe watu na taasisi zetu kwa gharama zetu, alimradi tu DP amelihitaji eneo ambalo watu au taasisi zetu zipo kwa sasa
4) tusiwe na gawio lolote kwenye faida atakayopata DP licha ya kwamba na sisi tayari tumewekeza matrilioni ya pesa kwenye bandari hizo hizo, wala siyo kwamba DP anakuja kujenga bandari mpya
5) tusimtoze kodi zilizopo kwa mujibu wa sheria, eti yeye awekewe zilizo ndogo na chache;

halafu mtu katika kuyajibu haya anasema, wapewe tu kwa sababu wana uwezo na ufanisi.

Hata katika maisha ya kawaida, wewe unaweza kuwa na familia yako, umezungukwa na familia nyingine, na uwezo wa hizo familia, aghalabu hutofautiana. Kuna familia zenye uwezo mdogo, familia zenye uwezo wa kati na familia zenye uwezo mkubwa. Kwa fikra za hawa wenzetu, ambao mimi nawaita wajinga na mafukara wa nafsi, wanaona ni halali yule mwenye familia yenye uwezo mdogo kukabidhi kila kitu alicho nacho ikiwa ni pamoja na ardhi au nyumba yake bure kwa familia tajiri kwa maelezo tu kuwa ile familia tayari itaboresha maisha ya ile familia maskini.

Kama.ni uwezo wa kifedha au tekinolojia ilio nao DP World, ndiyo kigezo cha kutoa bandari zetu bure, na sisi kupoteza hata ule uwezo wetu kama Taifa huru, kulikuwa na sababu gani ya hata kuwaondoa wakoloni? Wajerumani na Waiingereza, walikuwa matajiri kuliko sisi, walikuwa na tekinolojia kubwa kuliko sisi, walikuwa na mifumo bora ya kiutawala kuliko sisi, walikuwa na uwezo wa kusimamia uchumi kuliko sisi. Si tungesema tu wabakie kwa muda usiojulikana kwa sababu wana pesa na tekinolojia kubwa kuliko yetu, na hivyo wataboresha maisha yetu?

Watu wanahoji, kwa nini mkataba wetu na DP ni wa hovyo. Mtu mjinga, anajibu tena kwa kujiamini, eti mbona DP wamewekeza hata UK. Loh! Hivi huyu ana akili timamu? UK na DP wana mkataba wa kijinga kama huu wa kwetu?

Mtu anauliza kwa nini mkataba hauna ukomo. Mwehu anajibu, hii ni framework tu, ukomo utawekwa kwenye mikataba ya utekelezaji! Uwendawazimu wa hali ya juu. Yaani hajui hata maana ya framework agreement. Hajui mkataba huu ndio unaotoa uongozi kwa mikataba mingine, na siyo kinyume chake.

Watu wanauliza, bandari.ni suala la Muungano, kwa nini bandari za Zanzibar zimeondolewa? Kwa nini mkataba huu unakiuka articles of union? Wajinga wanakuambia, unajua DP itaajiri watu wengi!! Kwa hiyo huko Zanzibar hawahitaji ajira? Ama tuseme kuanzia sasa tumeamua kitu chochote kile hata kama kinakiuka sheria na katiba, ni ruksa, kwa sababu kitatoa ajira au kuleta pesa?

Watu wanahoji, kwa nini maamuzi ya kuwapa DP World bandari za Tanganyika, mchakato na maamuzi yake yamefanywa na Wizara ambayo inaongozwa na Wazanzibari pekee, licha ya ukweli kuwa wizara hiyo siyo ya Muungano. Wajinga hawa wanasema, mmeanza ubaguzi!!. Unajiuliza, mbona hawajampa mtanganyika yeyote uwaziri kule Zanzibar? Kwa hiyo tuseme kuwa Zanzibar ni wabaguzi sana kwa vile hakuna mtanganyika ambaye ni waziri au katibu mkuu kwenye wizara mojawapo ya Serikali ya mapinduzi Zanzibar?

Hivi hawa watetezi wa DP, tuamini ni wajinga, hawana akili, hawana uelewa, ni wanafiki au wamepofushwa na rushwa?

Watu wanaongelea ubaya wa mkataba, jibu, wanawapeleka akina Kitenge kuwahoji wafanyakazi wa DP Dubai kuhusu ufanisi na utendaji wa DP! Hivi tangu mjadala huu uanze kuna mtu amehoji au kulalamika kuwa DP hawana uwezo au hawana ufanisi katika biashara ya bandari? Wanatoa majibu ya kitu ambacho hakijaulizwa wala kuhojiwa na yeyote. Au wanayafanya haya kwa sababu hawana majibu kwa maswali ya msingj wanayouliza wananchi?
Ni mageti machache tu wanakwenda kufanya uwekezaji wao. Hakuna tofauti yoyote ile na TICTS walipewa mkataba wa kufanya biashara na walipoharibu wamepigwa chini.
 
Mkuu unao orodhesha hayana ushahudi wowote zaidi ya fikra zako tu, ndo maana unakua mkali........toa ushahidi kwa kuonyesha mikataba hiyo.
Hjo ushahidi unataka uletewe nyumbani?

Nakala ya mkataba iliwekwa hapa. Ebu taja kile ambacho nimekiweka hapa ambacho siyo kweli.

Mimi nimeorodhesha yaliyopo kwenye mkataba na yale yanayotokana na tafsiri kutokana na mkataba.

Kwa mfano, mkataba hakuna mahali popote unaposema ni mkataba wa miaka mingapi.
 
Siyo kweli .
Acha Upotoshaji
Wanakodisha uendeshaji wa baadhi ya maeneo ya bandari na sio bandari nzima. Hawana tofauti na TICTS katika muundo wa kazi japo ni vitu viwili tofauti.

TICTS inao uswahili na ufisadi ndani yake wakati DPW kwetu sisi ni mteja mpya tunayejua wepesi wake wa kazi, mengi tutayajua mbele ya safari.
 
Kero za ngu kubwa ktk mkatba huu Ni Moja

Kokozekana mwisho wa mktbala

Pili rais na waziri na katibu mkuu wote Ni wanzanzibari inanitaatiza sna hili Jambo kwa ujumla.wake wanzanzibari wnanataka kumuweka muarabu kwa nguvu tanganyika
 
Hapana, haiwezi kuwa sababu ya kuwapa kila kitu bure, tena mbaya zaidi milele.

Kesi lazima zifunguliwe kupinga ule mkataba wa kihuni kulinda maslahi ya Tanganyika huru
 
Back
Top Bottom