Doyo Hassani Doyo achukua fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha ADC

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
WhatsApp Image 2024-06-11 at 17.24.16_dd4097cf.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Allience for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho kumrithi Hamad Rashid ambaye amekiongoza kwa miaka 10 na kumaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba.

Doyo amechukua fomu hiyo leo Juni 11, 2024 Makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam ambapo aliambatana na mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Scolastica Kahana, aliyewahi kuwania Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini Mwaka 2020.

Mapema akizungumza mara baada ya kumkabidhi fomu, katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho bwana Innocent Siliwa ametoa wito kwa wanachama wote wanaochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho kufuata kanuni za uchaguzi ili kuepuka malalamiko na hatua kali zitachukuliwa kwa kila atakayekiuka.

"Zoezi la kuchukua fomu limeanza rasmi nitoe rai kwa wanachama mnaochukua fomu Kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama katika kuhakikisha kuwa mnafuata taratibu zote za chama zinazosimamia uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mnajaza fomu ipasavyo,". Alisema Siliwa.

Nae Mwenyekiti wa Vijana wa chama hicho, Ibrahimu Pogora, amesema vijana wana imani kubwa na Doyo kwa kutambua utendaji wake katika kipindi akitumikia nafasi mbalimbali katika chama hivyo ikiwa atafanikiwa kushika uongozi tunaamini anao uwezo wa kuboresha chama na kukifikisha katika kilele cha mafanikio ikiwa pamoja na kuwa chama Kikuu cha upinzani na zaidi kushika dola.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu Doyo Hassan Doyo ameanza kwa kuwashukuru wanachama wote waliojitokeza kumsindikiza katika ofisi hizo ili kuanza mchakato wa kukamilisha adhma ya kukalia kiti cha uongozi wa chama hicho.


"Napenda kuwashukuru wanachama wenzangu ambao mmeacha shughuli zenu ma majukumu yenu na kuja kujuika nami kuniunga mkono katika jambo hili, nawashukuru sana,". Alisema Doyo

Katika hatua nyingine chama hicho pia kimefanikiwa kupokea wanachama wapya kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wameamua kujiunga na chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kadi ya chama cha ADC, kwa niaba ya wenzake Bi. Sabra Masanza amesema anarejea kundini na ameahidi kusaidia chama katika kufikia malengo yake

Alisema alikuwa mwanachama wa ADC na baadaye akajiunga na Chadema ambako alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Uenezi Kanda ya Pwani na sasa amerejea nyumbani ili kuhakikisha ADC inafanya vema katika mikakati yake kwenye siasa za vyama vingi.

WhatsApp Image 2024-06-11 at 17.24.21_c2c34770.jpg

WhatsApp Image 2024-06-11 at 17.24.19_a3ef15b9.jpg
 
Back
Top Bottom