Double standards: Polepole ziara na mikutano anayofanya ni mbunge? Mbona upinzani wanazuiliwa?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,886
Naomba kufaham hizi ziara za Mwenezi wa CCM kuzunguka nchi kwa ziara ya kuimarisha chama mikoani ni mbunge wa Tanganyika? Anavyozunguka huko na huko yeye anaruhusiwa kama nani?

Si mlisema siasa mapaka 2020 huko kuimarisha chama ni kwa CCM pekee na upinzani wao marufuku?

Hizi ndio siasa safii?
 

Kwa vyama vingine ni siasa kwa CCM ni Maendeleo.
 
Polepole ni kinyonga asiejuwa rangi yake halisi ni ipi na policy yake ni ipi....ndumilakuwili.

Wakati wa rasim ya katiba mpya ya Warioba alikuwa tofauti sana na ccm....kila mmoja wetu alimpenda kwa kusimamia tija ma maslahi ya Taifa......

- Serikali tatu

-kupunguzwa madaraka ya rais

-Demokrasia yakweli na uhuru halisi na usawa kwa vyama vya siasa na watu wote

-Uhuru wa kupashana habari

Nk

LEO HII POLEPOLE AMEGEUKA NAKUSALITI YOTE......VERY SAD.
 
Huna usichokijua hapo. CCM inazo ofisi,mali na wanachama nchi nzima. Kutembelea maeneo hayo na kuangalia uhai wa chama na kubadilishana uzoefu. Ungewashauri viongozi wajaribu kuiga mpango huu.
 
Ili Nchi Iendelee Inahitaji:-
1.Watu
2.Uongozi Bora
3.Siasa Safi
4.Ardhi

Ccm Mungu Anawaona Hamtakuwa Salama
Mnawazuia Wenzenu Kufanya Lolote Halafu
Huyo Pole Pole Sana Anajidai Na Hicho Chama Cha Kijani Kama Nzi
 
Ni kweli huyu jamaa anazunguka yeye kama nani?si wamesema siasa ni mpk 2020?
 
Sishiriki sana siasa ila nawaona viongozi wa CCM na CHADEMA wakifanya ziara kwenye maeneo yao hasa mikutano ya ndani.
Zuio nakumbuka lilizungumzia mikutano ya hadhara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…