ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,834
- 69,521
Botto Biteko mesema TANESCO ina wadaiwa sugu ambao wanadaiwa takribani Bilioni 224 za matumizi ya umeme na hawajalipa.
Naunga mkono hoja, ila hapo utakuta 99% ni Taasisi za Serikali kama Hospital, Mamlaka za Maji na Ofisi za Umma.
Swali je, agizo lake litatekelwzeka? Maana TANESCO sio shirika la kibiashara, ni la huduma.
====
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameiagiza TANESCO kukata umeme kwa wadaiwa wote wasiolipa gharama za kutumia umeme ambapo Shirika hilo linadai jumla ya Shilingi Bilioni 224 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Binafsi na waliohama na madeni.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amekemea vikali watu wote wanaohujumu miundombinu ya umeme akitolea mfano wizi wa shaba na mafuta ambapo kati ya tarehe 25 Novemba, 2023 na 26 Novemba, 2024 kuna matukio 14 katika Ukanda wa Pwani ya kuharibu au kuhujumu miundombinu ya umeme.
Dkt. Biteko ametaka Watanzania kulinda vyanzo vya maji ambavyo vinazalisha umeme, amesema vyanzo hivyo visipolindwa vitapelekea athari mbalimbali zikiwemo kwenye uzalishaji umeme, pia ameitaka TANESCO kutokukaa nyuma katika masuala ya utunzaji wa mazingira.