Pre GE2025 DSM Dorothy Semu achukua fomu ys kugombea Urais ndani ya ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
2,093
5,590
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu leo tarehe 22 Aprili, 2015 amefika Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dar es Salaam kuchukua fomu ya kuomba kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akidokeza kuwa yupo tayari kuchuana na Mgombea wa CCM Samia Suluhu Hassan ikiwa Chama chake cha ACT Wazalendo kitamuidhinisha kuwania nafasi hiyo.

Soma pia:

"Leo nimechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia Chama cha Ishara kuwa nipo tayari kumkabili Rais Samia na CCM ambao wameshindwa kumkomboa mtanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii.Hii ni ishara ya utayari wangu wa kuongoza mapambano ya kulinda thamani ya kura na kutetea demokrasia"

photo_2025-04-22_16-24-07.jpg

photo_2025-04-22_16-24-03.jpg
 
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorthy Semu leo tarehe 22 Aprili, 2015 amefika Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dar es Salaam kuchukua fomu ya kuomba kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akidokeza kuwa yupo tayari kuchuana na Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Samia Suluhu Hassan ikiwa Chama chake cha ACT Wazalendo kitamuidhinisha kuwania nafasi hiyo.

Katika andiko lake la Aprili mwanzoni, Kiongozi mstaafu wa Chama hicho Zitto Zubeir Kabwe alionesha matarajio makubwa kwa Mwanamama huyo, akieleza kuwa ana matumaini makubwa kuwa anaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Leo nimechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia Chama cha Ishara kuwa nipo tayari kumkabili Rais Samia na CCM ambao wameshindwa kumkomboa mtanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii.Hii ni ishara ya utayari wangu wa kuongoza mapambano ya kulinda thamani ya kura na kutetea demokrasia"
Nilikua naangalia saa kumbe ni saa kumi za jioni,
Nadhani wamesahau au wamepitiwa kupata chai ya asubuhi na lunch, hivi vitu ukivikosa kwa kufuatana lazima utaota ndoto za mchana ukiwa unatembea.
 
Baada ya kutangaza nia ya kugombea Urais, leo Mei 22, 2025 Dorothy Semu amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa Mipango na Uchaguzi Taifa Ndugu, Shaweji Mketo katika Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar Es Salaam.
FB_IMG_1745329996857.jpg

Mara baada ya kukabidhiwa fomu, Ndugu Dorothy Semu akasema, "leo nimechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na niko tayari kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan na chama chake CCM—chama ambacho kimeshindwa kutimiza wajibu wake wa msingi wa kuongoza na kuwahudumia Watanzania."
FB_IMG_1745329987129.jpg
 
Baada ya kutangaza nia ya kugombea Urais, leo Mei 22, 2025 Dorothy Semu amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa Mipango na Uchaguzi Taifa Ndugu, Shaweji Mketo katika Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar Es Salaam.
View attachment 3312238
Mara baada ya kukabidhiwa fomu, Ndugu Dorothy Semu akasema, "leo nimechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na niko tayari kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan na chama chake CCM—chama ambacho kimeshindwa kutimiza wajibu wake wa msingi wa kuongoza na kuwahudumia Watanzania."
View attachment 3312239
Haongelei reform au yeye anachojali ni kuchukua tu form.
 
Kwa hiyo anaamini kabisa anaweza kushindana na Dr. Samia Suluhu Hassan na kushinda ?
Kwa kutumia nini labda maana Tume ya kwake sa100, Katiba inambeba yeye sa100 ni mbovu mbovu mbovu yeye mwenyewe anaiita kijitabu fulani tu hivi ambacho hakina maana kwake kwa maana haimtishi haina meno mbele yake na hizo Kanuni ndio kabisa km alikaa akazitunga mwenyewe sasa hapo unaenda kushindana na mtu ambae tayari kashashinda kabla ya kushindana nae?
 
Baada ya uchaguzi anataka ateuliwe ukuu wa mkoa...kama dada yetu wa twende kilioni kichwani. Hawa hawana Nia ya uongozi Hawa tunawajua, sisi tunataka wale wenye sauti kubwa ndio wagombee kupambana na yule bibi
 
Kwa kutumia nini labda maana Tume ya kwake sa100, Katiba inambeba yeye sa100 ni mbovu mbovu mbovu yeye mwenyewe anaiita kijitabu fulani tu hivi ambacho hakina maana kwake kwa maana haimtishi haina meno mbele yake na hizo Kanuni ndio kabisa km alikaa akazitunga mwenyewe sasa hapo unaenda kushindana na mtu ambae tayari kashashinda kabla ya kushindana nae?
Ndio maana nimeuliza, huyu ikitokea imetangazwa kashinda nafikiri atagoma kuapishwa maana alikuwa hajajiandaa...
 
Kila chama kina mtizamo wake ndio maana ya kuwa na vyama vingi

Wote hawawezi kuwaza kama CHADEMA Vinginevyo wasingekuwa na vyama vyao wote wangekuwa CHADEMA
Ili kuwa na upinzani wenye nguvu inatakiwa kuwe na vyama viwili tu.mfano chama tawala na vyama vyote vya upinzani vikaungana kuunda chama chenye nguvu
 
Back
Top Bottom