MoseeYM
Senior Member
- Jul 19, 2021
- 144
- 199
Habari wanaJF,
Ningependa kushiriki nanyi mambo machache kuhusu ujenzi kwa wale wanaoendelea na ujenzi, au wanaotarajia kufanya hivyo siku chache zijazo.
0679169532
Ningependa kushiriki nanyi mambo machache kuhusu ujenzi kwa wale wanaoendelea na ujenzi, au wanaotarajia kufanya hivyo siku chache zijazo.
1. YAPASWAYO KUFANYIKA KABLA YA KUANZA UJENZI
- Maandalizi ya Eneo: Hakikisha umefanya maandalizi ya eneo unalotarajia kujenga, mfano kusafisha eneo n.k.
- Utafiti wa Materials: Fanya utafiti kuhusu upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, gharama zake, na ubora wake. Hii itakusaidia kupanga namna bora ya kupata vifaa vyenye ubora na gharama zisizoumiza.
- Kusoshalize na Majirani: Socialize na majirani (kama wapo) kwenye eneo unalotarajia kujenga mara unapofika kwenye site yako. Hii itakusaidia kupata msaada kwa urahisi wakati wa ujenzi na kuokoa baadhi ya gharama (mfano: kuhifadhi vifaa, kusaidia kuangalia vitu visibiwe kwenye jengo lako wakati ujenzi ukiendelea, n.k.). Muhimu sana hii!
- Mipaka ya Kiwanja: Hakikisha suala la mipaka ya kiwanja chako umeliweka sawa na mipaka yako inatambulika.
- Kutafuta Ramani: Tafuta ramani unayoihitaji. Muhimu zaidi ni kutafuta mtaalamu wa kukusaidia kupata ramani itakayokidhi mahitaji yako kulingana na bajeti yako. Epuka kunakili au kuscreenshoot ramani zisizo na vipimo kamili kutoka mtandaoni. Ramani huwa ni seti ya michoro kadhaa ambayo iko katika mpangilio unaomsaidia fundi kujenga kile kilichodesigniwa. Michoro iliyosanifiwa ni muhimu kwa ufuatiliaji wa vibali vya ujenzi na hati. Hivi sasa, si ghali sana kupata ramani kutoka kwa wasanifu. Pia, wakati wa usanifu ni mzuri kupata ushauri wa kitaalamu wa ujenzi.
- Kutafuta Wataalamu: Tafuta wataalamu wa ujenzi/mafundi wa kukujengea jengo lako. Fahamu gharama zao pia. Epuka kuokoteza watu watakaokuja kujifunza kwenye jengo lako na kukuharibia.
2. HATUA YA UJENZI
- Uthibitisho wa Maandalizi: Wakati wa ujenzi, ni muhimu kuhakikisha kuwa unaweza kuanza kwa kuwa vitu vyote vya muhimu vipo tayari.
- Usafirishaji na Uhifadhi wa Materials: Jitahidi vifaa vifike kwa wakati site, na zinapofika zihifadhiwe vizuri na kutumika ipasavyo.
- Ununuzi wa Materials: Epuka kununua vifaa kidogo kidogo hasa vile vinavyohitajika kwa wingi site. Hii itakusaidia kuokoa gharama zisizo za lazima.
- Ushirikiano na Wataalamu: Shirikisha wataalamu husika kwenye eneo husika, mfano: kutegemea taarifa za fundi uashi kwenye kazi ya fundi umeme, kufanya mabadiliko ya design site pasipo kumshirikisha msanifu, n.k.
0679169532