Washington. Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kusaini sheria kuhusu wahamiaji na Waafrika wanaoingia nchini humo.
Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani zilisema, ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapotembelea makao makuu ya Wizara ya Usalama wa Ndani.
Pia, anatarajiwa kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika.
Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani zilisema, ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapotembelea makao makuu ya Wizara ya Usalama wa Ndani.
Trump aliandika kwenye Twitter kwamba, itakuwa siku muhimu kwa usalama wa taifa la Marekani.Wakati wa kampeni zake ya urais, Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.
Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi.
Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba Waislamu watakaguliwa kwa kina kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.
Chanzo: Mwananchi