Dola ya Marekani inavyonyanyasa sarafu mbalimbali duniani kwa mwaka 2025 na kufanya ndoto ya Brics kufifia kabisa

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
14,635
17,744
Muungano wa BRICS ambao ulianzisha ajenda ya kuondoa dola ya kimarekani sasa uko chini ya rehema ya dola ya Marekani mwaka wa 2025.

Dola ya Marekani ilisalia katika kijani kibichi kwa siku tisa mfululizo katika faharasa ya DXY na kukanyaga sarafu nyingine za ndani. Rupia ya India imeshuka hadi kiwango cha chini cha 85.93 na iko kwenye ukingo wa kushuka hadi kiwango cha 86. Yuan ya China na Yen ya Japan zinakabiliwa na hali ya chini sawa na haziwezi kutamba kwa dola ya Marekani inayopanda.

Dola ya Marekani ilifanya kazi vizuri zaidi kuliko sarafu zote za ndani mwaka wa 2025 na kuchukua nafasi ya kwanza katika masoko ya sarafu. USD sasa imefikia kiwango cha juu cha 109.30 katika faharasa ya DXY na inaweza kupindukia kiwango chake cha juu cha 109.53. Sarafu za wanachama wa BRICS ndizo zilizoathirika zaidi licha ya muungano huo kusukuma ajenda yao ya kuondoa dola ya Marekani ili kuishusha thamani.

Nchi kama India na China sarafu zao kuwa chini ya dollar huoni kwamba ni advantages kwa hizo nchi?

Hivi nyie wenzetu mna ABC za uchumi?

Ungesema mwamba GDP ya India au China imeshuka hapo ningekuelewa. Au export zao zimeshuka hapo ningekuelewa.

Hivi unakumbuka kipindi kile Trump ni president alikuwa analalamika kwa kitendo cha China kushusha curency yake na kusema inaondoa trade competitiveness.. unakumbuka?

Embu jifunze kwanza elementary economics.
 
Kwa hiyo tuna advantage kwa TZS kuwa very far weaker than USD? Hebu dadavua mchumi first class!
 
Muungano wa BRICS ambao ulianzisha ajenda ya kuondoa dola ya kimarekani sasa uko chini ya rehema ya dola ya Marekani mwaka wa 2025.

Dola ya Marekani ilisalia katika kijani kibichi kwa siku tisa mfululizo katika faharasa ya DXY na kukanyaga sarafu nyingine za ndani. Rupia ya India imeshuka hadi kiwango cha chini cha 85.93 na iko kwenye ukingo wa kushuka hadi kiwango cha 86. Yuan ya China na Yen ya Japan zinakabiliwa na hali ya chini sawa na haziwezi kutamba kwa dola ya Marekani inayopanda.

Dola ya Marekani ilifanya kazi vizuri zaidi kuliko sarafu zote za ndani mwaka wa 2025 na kuchukua nafasi ya kwanza katika masoko ya sarafu. USD sasa imefikia kiwango cha juu cha 109.30 katika faharasa ya DXY na inaweza kupindukia kiwango chake cha juu cha 109.53. Sarafu za wanachama wa BRICS ndizo zilizoathirika zaidi licha ya muungano huo kusukuma ajenda yao ya kuondoa dola ya Marekani ili kuishusha thamani.

BRICS HAIPO KWA LENGO LA KUIANGUSHA DOLA.

History ya dola mpaka kuja kuwa world reserve currency itafanya ujumbe huu kuwa mrefu na wa kuchosha.

Baada ya dola kuwa reserve currency ya dunia, Marekani ikawa inaitumia dola kama chombo cha kisiasa katika kuziwekea nchi vikwazo. Nchi ambazo zinapingana au hazikubaliani na sera za kimataifa za marekani na Nato. Na hili liliwezekana kwa kupitia mfumo wa kimataifa wa kibenki wa SWIFT.

Nadhani mwaka 2017 kabla ya vita ya Ukraine Urusi alianzisha mfumo wake unaoitwa Mir na nadhani unatumika katika nchi takriban 10 au 11. Huu uliziwezesha nchi hizo kufanya biashara na Urusi bila ya kutumia mfumo wa swift. Nadhani Urusi ilishajua vikwazo vitakavyokuja mbeleni na wakaandaa alternative yake.

Baada ya wanachi wanachama wa brics kukubaliana, Sasa umekuja mfumo wao wa malipo wa BRICS PAY na watalipana kwa kutumia sarafu za nchi zao badala ya dola mpaka sarafu ya brics ambayo italindwa na dhahabu itakapokuwa tayari.

Sasa lengo kuu la brics pay ni kwa nchi wanachama kuweza kufanya malipo baina yao na kuikimbia dola ambayo baadae inageuka kuwa silaha dhidi yao. Na zaidi ya hapo kuwa na taasisi yao ya kifedha kwa ajili ya kukopeshana ambayo itakuwa na masharti yenye uafadhali kuliko IMF au world bank.

Baada ya Japan, China ndiye mmiliki mkubwa wa bond za dola ya Marekani hivyo dola ikishuka kwa kasi sana Mchina naye atakuwa kala hasara. Kushuka kwa nguvu ya dola hakuepukiki kwa sababu ile ile ya demand and supply, kwa hilo tunakubaliana. Na kwa kulijua hilo, China sasa hivi inauza bond za marekani kwa kasi kubwa na badala yake inaongeza hifadhi ya dhahabu.

Dola itashuka, dominance yake itapungua au kwisha kabisa. lakini haya mambo sio ya kutokea ndani ya m
iaka 5 au 10.
 
Nchi kama India na China sarafu zao kuwa chini ya dollar huoni kwamba ni advantages kwa hizo nchi?

Hivi nyie wenzetu mna ABC za uchumi?

Ungesema mwamba GDP ya India au China imeshuka hapo ningekuelewa. Au export zao zimeshuka hapo ningekuelewa.

Hivi unakumbuka kipindi kile Trump ni president alikuwa analalamika kwa kitendo cha China kushusha curency yake na kusema inaondoa trade competitiveness.. unakumbuka?

Embu jifunze kwanza elementary economics.
Pole ndugu kwa kumjibu huyo popoma wa uchumi yeye anajua tu kuimba usa .. usa mamtoni hajui watu huko wanateseka na infarion ya kama matikeo ya pesa yao
 
Mimi nimeleta taarifa iliyoandikwa na jarida hilo hapo sasa kunikosoa kwamba sijui ABC ya uchumi ni kuonyesha jinsi watu mlivyo na upeo mdogo na hii yote ni kwa sababu kuna watu humu wakiona habari yoyote wanayoona inaelekea kuifagilia Marekani basi wenyewe huchangia kwa misingi ya kidini wakilenga kuiponda hiyo taarifa.

Hizi imani za kidini zinakuwa na mwitikio mbovu sana kwa jamii ya kitanzania kwani huwafanya wasidadavue mambo kwa uhalisia wake.
 
Western propaganda hazijawahi kuwa na mazuri . Ni hao hao waliokuwa wanadai eti ukrain inashinda
 
Unadhani kuwa na strong currency ni faida kwa nchi ? Pound ilikuwa strong kwa muda mrefu sana lakini matokeo yake bidhaa zake zinakwa zinaonekana expensive kuliko za wengine..., China always amekuwa akimanipulate currency yake iwe chini ya Dollar. Ukiwa muuzaji wa bidhaa ni faida kwako sarafu yako ikiwa na thamani ndogo kuliko wengine hivyo bidhaa zako kwa soko la dunia kuwa bei nafuu...

Threat ya BRICS au Dollar kutokuendelea kuwa world currency ni kwa USA kuacha kupata faida wanayopata sasa kwa kuweza kuandaa bajeti kubwa kuliko makusanyo yao (Deficeit) kwa guarantee ya Dunia nzima\

Nchi kama India na China sarafu zao kuwa chini ya dollar huoni kwamba ni advantages kwa hizo nchi?

Hivi nyie wenzetu mna ABC za uchumi?

Ungesema mwamba GDP ya India au China imeshuka hapo ningekuelewa. Au export zao zimeshuka hapo ningekuelewa.

Hivi unakumbuka kipindi kile Trump ni president alikuwa analalamika kwa kitendo cha China kushusha curency yake na kusema inaondoa trade competitiveness.. unakumbuka?

Embu jifunze kwanza elementary economics.
Watu wanadhani currency yako ikiwa na thamani kubwa kuliko dola then na uchumi wako uko hohehahe, kujua vitu nusu nusu ni sawa na kuramba sumu tu. Kama hutegemea ku import zaidi na una export sana then currency valve is issue ki vile. India na China wanauza zaidi kuliko kununua, viwanda vikubwa duniani vinawekeza kwao and hence Wahindi na Wachina wana nunua bidhaa kwa currency zao, huwezi kulinganisha na nchi kama za kwetu ambazo hadi chupi, toothpick, pamba za kutolea nta masikio tunaagiza kutoka nje; poor us
 
Mimi nimeleta taarifa iliyoandikwa na jarida hilo hapo sasa kunikosoa kwamba sijui ABC ya uchumi ni kuonyesha jinsi watu mlivyo na upeo mdogo na hii yote ni kwa sababu kuna watu humu wakiona habari yoyote wanayoona inaelekea kuifagilia Marekani basi wenyewe huchangia kwa misingi ya kidini wakilenga kuiponda hiyo taarifa.

Hizi imani za kidini zinakuwa na mwitikio mbovu sana kwa jamii ya kitanzania kwani huwafanya wasidadavue mambo kwa uhalisia wake.
Wewe acha kujifyatua akili hapa,hakuna aliyejadili hii mada kwa misingi ya udini,bila shaka wewe ndio umeileta hii thd kwa misingi hiyo ndio maana unajishtukia,nyuzi zako nyingi hapa JF zina maudhui ya chuki ya udini,

Pambana na hali yako hapo Tegeta kwa ndevu,hao US wanaweza hata wasikupe Visa japo ukatembee tu.
 
Back
Top Bottom