Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,299
- 6,314
Wanavyuo kutoka mkoa wa Dodoma wameazimia kwa kauli moja kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Azimio hilo limetangazwa katika mkutano mkubwa uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Ndg. Geofrey Kiliba.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika mkutano huo, wanavyuo hao wamesisitiza dhamira yao ya kumlinda na kumtetea Rais Samia dhidi ya upotoshaji wowote, wakieleza kuwa uongozi wake umeleta mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali za maendeleo, hususan elimu, uchumi, na miundombinu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ndg. Kiliba amewapongeza wanavyuo kwa mshikamano wao na kuwahimiza kuendelea kuwa mabalozi wa maendeleo na ukweli kuhusu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.