Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,609
Picha: Prof. Mkumbo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema suala la viwanda 100 kila mkoa siyo mpango wake na halipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo amesema kazi kubwa ni kusimamia ujenzi wa viwanda kila mtaa na kuanzisha ukanda maalumu wa viwanda.
Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo leo Novemba 17, 2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari uhusu miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Amesema hilo halimo kwenye usimamizi wake ambao unaongozwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ambayo alishiriki kuiandika.
"Suala la viwanda 100 hilo siwezi kulisemea kwa sababu halinihusu na halipo katika mwongozo wa mambo manne ninayoyasimamia chini ya Ilani ya Uchaguzi," amesema Profesa Mkumbo.
Waziri huyo amesema hadi kufikia Julai 2021 Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 80,696 vyenye uwezo wa kuajiri kati ya watu 1 kuendelea na mtaji unaoanzia Sh1 milioni.
Amesema sekta binafsi bado inaendelea kupewa nafasi kubwa ili kuwavutia wawekezaji kufurahia uwekezaji wao.
Mwananchi