Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
5,580
60,883
Mtoto wa miaka minne jinsi ya kiume amekutwa ametekelezwa nyuma ya nyumba kwenye makazi ya watu Kisasa majumba 300 baada ya kukatwa mkono wa kulia na sehemu za siri na watu wasiojulikana na kutokomea navyo kusikofahamika.

Siku kadhaa hapo nyuma yameshatukia matukio kama haya mawili ambayo nimeyasikia.

Hii taarifa nimeipata kwa moja wa jirani wa wazazi wa mtoto aliyetendewa kitendo hicho cha kikatili na kupelekea umauti wa mtoto huyo.

Swali ni; upo wapi usalama wa raia?

=====

Dodoma.
Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio la mwili mtoto, Telesphore Mwakalinga (4) aliyeokotwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Julai 18, 2024 eneo la nyumba 300, Kisasa jijini Dodoma akiwa hana mkono na sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya amesema tukio hilo lilitokea jana Jumatano usiku kwenye nyumba 300 zilizopo Kisasa jijini Dodoma.

“Jana askari polisi akiwa katika eneo hilo aliona mbwa akiwa na kitu, jambo ambalo lilimfanya kusogelea karibu na kumuona mtoto huyo. Alitoa taarifa polisi ambao walikwenda kwenye tukio na kumpeleka hospitali,” amesema.

Amesema kwa sasa hivi hawawezi kusema mtoto huyo aliuawa ama vinginevyo hadi hapo watakapopata uhalisi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.

“Siwezi kusema ameuawa hadi tutakapokamilisha uchunguzi wa tukio hilo yakiwemo mazingira ya tukio lenyewe ikiwa aliondokaje nyumbani,” amesema kamanda huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka katika eneo hilo, mtoto huyo alipotea jana jioni saa 12.00 jioni lakini alipatikana saa 4.00 usiku, akiwa hana mkono mmoja na sehemu za siri katika eneo hilo la nyumba 300 za Kisasa jijini Dodoma.

Kamanda Theopista amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

©Mwananchi
 
Mtoto wa miaka minne jinsi ya kiume amekutwa ametekelezwa nyuma ya nyumba kwenye makazi ya watu Kisasa majumba 300 baada ya kukatwa mkono wa kulia na sehemu za siri na watu wasiojulikana na akutokomea navyo kusikofahamika.

Siku kadhaa hapo nyuma yameshatukia matukio kama haya mawili ambayo nimeyasikia.

Hii taarifa nimeipata kwa moja wa jirani wa wazazi wa mtoto aliyetendewa kitendo hicho cha kikatili na kupelekea umauti wa mtoto huyo.

Swali ni; upo wapi usalama wa raia?

Kwa nini uchaguzi ukikaribia matukio kama haya yanafanyika sana? Je tuhusishe haya yanayoendelea na uchaguzi/wanasiasa? Watoto wana haki ya kusihi na kupata haki za msingi( UNICEF ilisema na kusikika kwa sauti kubwa )
 
Viongozi wenu wachawi wakijiandaa na uchaguzi. Haijalishi hizi taarifa ni za kweli au uongo.
Fungia mtoto wako ndani mpaka hiki kipindi kiishe. Otherwise, usishangae ukija kuta kabaki kiwiliwili kichakani.

Hasa kwa wale wazazi wapuuzi wasemao "Mtoto ni mali ya jamii." Huku wakikimbia responsibility.
 
Leo nimesikiliza Clouds tv habari ya asubuhi
Mkuu wa polisi kakanusha taarifa za watoto kuuwawa kasema ni watu wanazusha hata ile ya Temeke, Mbagala ni uongo🤔
Dah! My God! Kwa hiyo sasa wasiojulika waendelee tuuu?? Ni ruksa?
Kama hao tuliotegemea ndo kazi yao na wanawalipwa kwa kodi zetu majibu yao ndo hayo, basi tumekwisha. Wazazi fungieni watoto ndani au mlale nao chumba kimoja mkiwa na rungu, panga au mkuki.
 
Back
Top Bottom