Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,715
- 4,455
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.
Shauri Na.993 la mwaka 2025 lilidai Dkt. Slaa ameshtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter).
Leo February 27,2025, Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga .
Wakili Mrema ameieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.
Source: Millard Ayo, TBC