BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 485
- 1,174
Nipo nawasikiliza Wachambuzi wa masuala ya Sias wakijadili Katiba Mpya.
Baadhi ya washiriki wa mjadala ni:
Dkt. Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji, LHRC
Dkt. Willibrod Peter Slaa, Mbunge Mstaafu
Zitto Kabwe, Kiongozi Mstaafu , ACT-Wazalendo
Salma Said, Mwandishi wa Habari, DW (Deutsche Welle)
Marry Ndaro, Mwendesha Mjadala.
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Dr. Wilbroad Slaa amesema kuwa hakubaliani na kauli ya Serikali ya kutoa elimu ya Katiba kwa miaka mitatu kabla ya kupata Katiba mpya.
Akizungumza leo April 3, 2024 kwenye mjadala ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) kupitia Mtandao wa X-Space zamani ikitambulika kama Twitter, kuwa wananchi hawahutaji elimu hiyo hata kwa sekunde moja, ambapo amedai kuwa wananchi wanapodai Katiba wanaelewa nini wanataka.
"Mimi bahati nzuri nilishiriki kukusanya maoni wakati wa Warioba tukiwa kwenye Tume, lakini Mimi kama Katibu Mkuu wa Chama nilizunguka Nchi nzima kukusanya maoni pamoja na wenzangu ndani ya Chama wananchi wanajua wanahitaji nini ndio maana ukienda kwenye rasimu ya Katiba aliyoiandaa Warioba yale yote yaliyoko kwenye rasimu ni maoni kutoka kwa wananchi wenyewe"
Akiendelea kuchangia mjadala huo ambao ulikuwa na mada isemayo "Madai ya Katiba mpya: Je Wananchi wanahitaji elimu ya miaka mitatu ?", Mwanasiasa huyo ambaye amewai kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, pamoja na kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema kwenye uchaguzi Mkuu 2010 amesema kuwa Serikali inatakiwa kurejesha rasmi mchakato wa Katiba mpya.
Ambapo amesema kuwa inaweza ikaletwa Sheria nyingine ya kuendeleza mchakato huo au kutumia Sheria ya mabadiliko ya Katiba ambayo amedai bado ipo hai licha ya kudaiwa kuondolewa Bungeni.
"Utaratibu rahisi ni kurudisha mchakato wa Katiba kwa kupitia Sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyokuwepo bungeni ikaondolewa kwa taratibu zisizo halali, Wanasheria tunakubaliana wengi, najua wapo wanaobisha kwamba hile Sheria bado ipo hai kwa sababu hiyo Sheria kuna kipengele inataja kwamba itaisha muda wake pale yote yanayotakiwa kwenye Katiba na utekelezaji wa Katiba hiyo yatakapokuwa yamekamilika."amesema Dr. Slaa
Ambapo amedai kuwa kumekuwepo na hofu kwa watawala kuhofia wapoka mamlaka waliyonayo, licha ya yeye kudai kuwa Katiba mpya inalenga kuweka mgawanyo wa madaraka unasaidia utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika Nchi.
Hata hivyo mmoja kati ya wachangiaji amesema kuwa kama kuna mchakato wa kutoa elimu ni bora ukafanyika baada ya kupatikana kwa Katiba, ambapo amesema kuwa kusema wananchi wasubiri kwanza wapewe elimu ya miaka mitatu ni 'janja janja' za kutaka uchaguzi Mkuu ufanyike bila kuwepo kwa Katiba mpya.
Zitto: Hata Wakoloni Hawakuweka Masharti ya Namna Hii Kwenye Kupata Katiba Mpya
Zitto Kabwe amesema wananchi wamepewa mamlaka ambayo yanaweza kuishinikiza Serikali kuwajibika kwenye mambo wanayoyataka hususani suala la Katiba Mpya.
Akichangia hoja ya madau aliyeshiriki mjadala huo iliyohoji kama wananchi wanayonafasi ya kuishinikiza Serikali kuendelea na mchakato wa Katiba mpya,Zitto amesema kuwa kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa mamlaka makubwa ambayo yanawafanya viongozi kuwajibika kwa wananchi.
Amesema Serikali inaweza kushinikizwa kuwajibika na vyombo ambavyo vimepewa nguvu ya uwakilishi kama wabunge, pamoja na Mahakama ambayo ipo kwa ajili ya kuitafsiri Sheria.
Hivyo amedai kuwa kulingana na mazingira mbalimbali wananchi wanaweza kuishinikiza Serikali kwa utaratibu huo au mwingine kwa kuzingatia taratibu.
Mdau mwingine ambaye amechangia mjadala huo ; amesema kuwa kumekuwepo na hofu ya watawala kuififisha jitihada za kupata Katiba mpya kwa kudhania kuwa Katiba ni kwa ajili ya madaraka.
Amedai kuwa mtazamo huo ni hasi kwa kuwa Katiba inaweka mwelekeo wa Nchi kwenye mambo mengi muhimu ambayo yanaweza kuifanya Nchi kupiga hatua zaidi kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo maendeleo.
Carol Ndossi: Elimu na Mchakato wa Kupata Katiba Mpya Viende Pamoja