Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Wakuu, Balozi mstaafu Dkt. Willbrod Peter Slaa anazungumza live kwenye Medani za Siasa Star TV.
Sababu ya kuondoka CHADEMA ilikuwa ni kumpokea Edward Lowassa kuwa mgombea Urais wa chama hicho. Dkt. Slaa amesema alizunguka nchi nzima akiutangazia umma kuwa Lowassa ni fisadi, na alimtangaza Mwembeyanga kwenye orodha ya mafisadi nchini (The list of shame). Asingeweza tena kumsafisha kwa namna yoyote ile.
Amesema Hayati Magufuli aliwahi pia kuwa na makosa ya ufisadi wakati wa kuuza nyumba za serikali, na miongoni mwake ni makosa mwili ambayo yeye Dkt. Slaa anayafahamu ikiwemo kugawa nyumba ya Serikali kwa “girlfriend wake”.
Anasema Balozi ana njia za kuwasiliana na Raisi Moja kwa moja ili kupeleka ushauri wake, ivyo hawezi kusema ni kitu gani alikuwa akiishauri serikali na Hayati Magufuli wakati akiwa balozi, pia amesema hata Mawaziri wana njia zao za kupeleka mawazo na ushauri wao huwezi kuwasikia wakipiga kelele kama wabunge maana wao wana njia zao.
Pia si kila kitu kipingwe hadharani, balozi ana njia zake na ivyo kama vipo alivyompinga Rais Magufuli basi alimpinga kwa kutumia njia hizo.
Pia amesema Magufuli hakupiga marufuku vyama vya siasa kwa kuwa ili Rais aseme inabidi aandike kama hakuandika ivyo hakusema na vyama vya upinzani viliogopa kwa kuwa na woga na yeye aliona udhaifu huo na ili kuotoka mtegeni ndio maana alitamka na si kuandika.
Amesema Rostam, hana hadhi ya kujibiwa na mtu wa hadhi yake, ameshampunguza kama punge ya shanga au haradali, hana hoja hivyo amempuuza. Amesema Rostam anaweza kutamka upuuzi tu wa anachotaka.
Dkt. Slaa Amesema Mwalimu Nyerere aliwahi kusema tusibinafsishe maendeo muhimu ya nchi yetu ambayo ni Bandari, Uwanja wa ndege, na mengine jumla yalikuwa 5, amesema ni nchi ya wapumbavu pekee ndio wanaweza kubinafsisha maeneo muhimu ya nchi.
Anasema bandari ni sehemu muhimu, ni kama geti kwenye nyumba na bandari ndio geti la nchi, sasa unachukua geti unamkabidhi mtu hapo utakuwa huru kweli?
Aliweka swali kidogo kimaanisha hakuta kuwa na uhuru. Anasema hayo yanayosemwa na Serikali juu ya mkataba kuwa si mkataba bali ni makubaliano ni propaganda za Serikali ili kuwafanya watu wakubali na hajui kwa nini wanafanya ivyo.
Anasema waandishi Mnaambiwa huo si mkataba ni makubaliano na nyie mnakubali, ina maana waandishi hamkusoma, kiingereza hamjui au hata kama hamjui hamna kamusi, mkataba umeandikwa agreement maana yake mkataba, sasa kwanini mnaambiwa na Msigwa nanyi mnakubali, mnamsikiliza Msigwa ambaye yupo kufanya propaganda tu na si kueleza kisheria.