Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 29,869
- 21,075
Ndugu zangu Watanzania,
Kama kuna mtu mnapaswa kumpuuza ,kutokumsikiliza na kumkemea vikali wakati huu ni Dkt Slaa. Huyu Mzee ni Muongo sana ,Mchonganishi sana ,kigeugeu sana na anayebadilika kama kinyonga.
Embu jaribuni kufuatilia kauli zake za siku ya nyuma ndio muelewe nayoyazungumza hii leo. Huyu Mzee bila ushahidi amewahi kuudanganya Umma hadharani kuwa kuna Kontena linaingiza maboksi ya kura Feki Nchini . Mwisho wa siku baada ya uchunguzi ilikuja kubainika ni uongo na Mzee alikuwa ameudanganya Umma.
Huyu Mzee Kwa Mdomo wake Si mnakumbuka yale aliyoyazungumza wakati Mbowe amekamatwa kwa kesi ya Ugaidi? Je mnakumbuka yale aliandika kuihusu CHADEMA kwa kile alichoita Nyuma ya Pazia? Je amewahi kukanusha au kuomba msamaha? Je mnakumbuka kile alizungumza kuhusu kupigwa Risasi kwa Lissu?
Mnaanzia wapi kumuamini na kumsikiliza huyu mzee enyi watu? Ninyi mnafikiri ni kwanini watanzania wengi kwa sasa wamempuuza na kupelekea kukosa kabisa ushawishi na nguvu kwa watanzania? Jibu ni kuwa watanzania wamegundua kuwa huyu mzee ni muongo, kigeugeu, Mchonganishi na kinyonga asiye na msimamo zaidi ya kutapatapa tu na kupigania maslahi yake binafsi. Ndio sababu alipopewa Ubalozi alitulia tulii kama Maji mtungini.
Dkt Slaa ni lazima atambue ya kuwa heshima huwa hairudi mara mbili. Aliheshimika na kusikilizwa awali kwa sababu watu walikuwa gizani juu yake. Lakini sasa watu wanajua rangi yake halisi kuwa ni mtu msaliti,muongo, kigeugeu na kinyonga. Hivyo hakuna anayeweza kusikiliza uzushi wake na kumuunga mkono.hakuna wa kumsikiliza wala kupoteza muda wake kutega sikio kusikiliza uongo wake. Kwa sasa yeye atulie tu na kuendelea kujutia makosa yake na kuomba msamaha kwa Mungu wake. Uongo na uzushi hauwezi kumrejeshea heshima aliyoipoteza Mwenyewe.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.