Dkt. Wilbroad Slaa, Mwanachama na kiongozi mstaafu wa CHADEMA amedai kuna hali ya sintofahamu ndani ya chama chake cha zamani.
Ameamua kusema kuwa CHADEMA inatamka mambo makubwa, lakini vitendo vyao vinaonyesha picha tofauti kabisa.
Ameeleza wazi jinsi anavyokerwa na ukimya wa CHADEMA juu ya tuhuma za rushwa zilizotolewa na Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.
Katika nafasi yake, Lissu angeweza kutumia madaraka yake kuhakikisha tuhuma hizo zinajadiliwa ndani ya chama na kufanyiwa kazi ili ukweli ujulikane.
Lakini kinyume chake, Lissu amenyamaza huku akiwalaghai Watanzania na kauli za uongo dhidi ya CCM na serikali.