Dkt. Nyambura Moremi ateuliwa tena kuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa. Aliondolewa baada ya sampuli za mimea kukutwa na UVIKO-19

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
65,819
75,143
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemrejesha kwenye nafasi yake aliyekuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii (NPHL), Dk Nyambura Moremi aliyesimamishwa kazi Mei 4, 2020 kupisha uchunguzi.

Dk Moremi amerejeshwa ikiwa ni miaka minne, baada ya kuondolewa katika nafasi hiyo na Waziri wa Afya, baada ya Rais wa wakati huo, hayati John Magufuli kutia shaka usahihi wa vipimo vya Maabara ya Taifa vilivyothibitisha kuwapo Uviko-19 katika sampuli za wanyama na mimea.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Englibert Kayombo, Dk Moremi ameteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa maabara hiyo, Medard Beyanga.

“Kwa kipindi chote Dk Moremi alikuwa Mkuu wa Idara ya Tafiti katika Maabara Kuu ya Taifa,” amesema Kayombo.

Dk Moremi ni miongoni mwa wabobezi katika fani ya maabara na ni mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza.

Pia, soma=> Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

20240411_144137.jpg



View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1778374400317767778?t=07CH9V1X6z4RR1t8Zfq5rw&s=19

My Take
Walinda Ligacy mnaitwa huku 🤣🤣🤣
 
Ni Dkt.Moremi Marwa ambae alitimuliwa na Mwendazake Kwa kuthibitisha Uwepo wa uviko 19 Kupitia ushahidi wa maabara.

Ikumbukwe hata Marehemu Dr.Mwele Malecela alitimuliwa na Mwendazake kisa Kusimamia Maadili ya kazi.

Shirika la Afya Duniani Huwa linamuenzi Dr Mwele Kwa kuanzisha tuzo ya Sayansi ya Magonjwa ambukizi ya Mwele Malecela inayotolewa Kwa watafiti Kila mwaka.

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1778374400317767778?t=07CH9V1X6z4RR1t8Zfq5rw&s=19

My Take
Walinda Ligacy mnaitwa huku 🤣🤣🤣

Magufuli alikuwa bwege sana halafu covid-19 hiyo hiyo ikaja kumpitia dadeq
 
Back
Top Bottom