Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,035
164,306
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.

Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.

========

Hussein Mwinyi amesema kuwa yupo tayari kutoa ufafanuzi kwa yale yote yaliyokuwa yanasemwa na alikataa kuongea kabla ya uchaguzi kwa kuwa huenda kauli yake ingetafsiriwa tofauti.

Mahojiano yao yalikuwa:

Swali, Katika hatua mbalimbali za mchakato ambao umemfikisha hapo alipofikia ni hatua gani ilikuwa inamtia wasiwasi ambayo alikuwa anadhani akiivuka mambo yake yatakuwa mazuri.

Jibu, Katika utaratibu wa chama kutoka kwa wale wote waliochukua fomu huchujwa na kupata watano, na kutoka watano kwenda tatu bora, hatua zote ni ngumu na hazitabiriki kuwa kuna moja ni rahisi zaidi ya nyingine bali zinataka kuwa makini na yeye alikuwa anasubiri baada ya hatua hizo nani atashinda na anashukuru alifanikiwa kushinda.

Swali Unadhani katika mchakato huo kuna watu ambao ulikuwa unahofia kuwa iwapo wataingia huenda mpambano utakuwa mzito zaidi huenda wana ushawishi zaidi Zanzibar au vipi au nao waliingia katika hao watu 32 ?.

Jibu Katika uchaguzi huwezi umdharau mtu yoyote na aliona katika wote waliochukua fomu wana nafasi ya kushindahususani wale waliokuwa katika serikali au chama walikuwa na nafasi kama ambavyo alikuwa nayo yeye.

Swali Kwenye hotuba yako ulisema kuwa mtihani wa kutafuta nafasi ya kuwania urais ulisema ulikuwa mgumu, wewe ni daktari na mitihani ya madaktari kwa kawaida huwa ni migumu zaidi lakini umesema huu wa kuwania urais wa Zanzizibar ulikuwa mgumu zaidi ?.

Jibu Mtihani ulikuwa mgumu kuliko yote kwakuwa haukuwa mwepesi na hautabiriki kwa hiyo mpaka kuumaliza kwa ushindi anamshukuru Mungu.

Swali Sasa Dr.Hussein Tayari yameshabaki majina matano na tayari mmeshafika Dodoma ulijisikiaje kufika katika hatua hii? Lakini je,uliona mtihani ulizidi kuwa mgumu zaidi kwakuwa miongoni mwa wale watano yoyote anaweza kuchaguliwa?

Jibu Kutoka kwenye watu wote mpaka kufika watano maamuzi hayo yalifanywa na kamati kuu Zanzibar na unaweza kusema kuwa wale ambao hawakuwa na nguvu sana walikuwa wameshatoka na kubaki wale ambao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wengine hivy mtihani ulizidi kuwa mgumu zaidi.

Swali Je, ulipofika Dodoma ulikuwa tayari una tetesi ya kuwa nani unakutana nao kwenye kinyang'anyiro hicho au mpaka unafika Dodoma hukua unajua chochote.

Jibu Kwakweli taarifa zilitoka kwenye mitandao ila hawakuwa na uthibishi ila yeye aliamini hivyo hivyo walipofika Dodoma walikuwa wanasubiri kuthibisha kama ni hivyo.

Swali Sasa baada ya hapo mkabaki watatu na wenzako wawili walikuwa na hali ya kufahamika zaidi, wao wana shughuli zao Zanzibar hivyo kufahamika zaidi japo na wewe unafahamika ila ni maneno yalikuwa yanesemwa.

Jibu Yeye hakuliona katika mtazamo huo alikuwa anaona ni maneno ya watu ambao hawakuwa upande wake kwa sabau yeye amekuwa mbunge wa Kwahani kwa miaka 15 na miaka hiyo ni mingi na alikuwa anajiona ni mmoja ya watu wanaofahamika zaidi Zanzibar hivyo kusema alikuwa hafamiki haikuwa sahihi.

Swali Kwa mshangao wa wengi na sijui kwa upande wako wewe ulilichukuliaje suala la Mh. Rais na mwenyekiti wa chama kusema kikao cha halmashauri kuu kitakuwa cha wazi hata kwenye "television" kioneshwe, ulifurahia uamzi huo au ulipata mshangao na kuona suala hilo hakutakuwa na cha siri tena?

Jibu Kwa kweli nichukue fursa hii kumshuru rais kwa kuwa kila mmoja aliondoka pale akiwa ameridhika na kuona kulikuwa na haki hakuna kuibiwa wala kuonewa.

Swali Baada ya kuitwa kwenda kushikwa kurazenu na kuona wewe unakuwa na rundo kubwa la kura ulijisikiaje kuona kuwa unaelekea kushinda?

Jibu,kwa kweli nilijisikia vizuri sana kwa kuwa kila mgombea ana mategemeo ya kushinda na nilimshukuru Mungu kwa kuwa niliona naelekea kushinda.

Swali kuna maneno yanasemwa kuwa nafasi yako umeipata kwa msaada wa wajumbe kutoka Tanzania bara na sio kutoka wajumbe wa Zanzibar.

Jibu Ni maneno potofu ila ukweli utabaki palepale na ni ukweli wa kitakwimu kuwa, wajumbe wanaopiga kura ni 68 na ukichukuwa kura za wenzangu ambo jumla 35 na hivyo 33 zilipiga kwangu na mimi nimepata karibu nusu ya kura na hivyo mimi nimepata karibu nusu ya kura za Zanzibar.

Swali Maneno kama haya ya watu wanapiga kwenye mitandao yanakupa tabu gani hasa wakati huu unapoelekea kwenye kampeni.

Jibu Hazinipi changamoto yoyote kwa kuwa maneno ya sikupata kura za watu wa Zanzibar sio kweli.

Swali Je, wazanzibari wategemee utabadilika na kuwa mkali kama Rais Magufuli maana unaonekana ni mtu mpole na mtaratibu kiasi.

Jibu Sio rahisi kunielewa vizuri kwa kuwa sikuwa na wizara ambayo nilikuwa naonekana ila nimejifunza kutoka kwa watangulizi wangu kama JK Kikwete na Rais Magufuli ukali wake wa kupinga ubadhilifu na rushwa nimejifunza na nitapenda kuwa kama yeye katika kuhakikisha ubadhilifu, rushwa havipati nafasi.

Swali Inasemekana wewe ni kweli umezaliwa na wazazi ambao ni wazanzibari ila hukuzaliwa Zanzibar na hukukulia wala kusoma Zanzibar hivyo huna ukaribu zaidi Na Zanzibar kuliko sehemu nyingine za Tanzania bara.

Jibu Mimi nimezaliwa Zanzibar japo sikusoma Zanziba ila hii hainiondolei sifa ya kugombea nafasi ya kuwa Rais wa Zanzibar.

Swali Wengine wanakwenda mbali zaidi kwakusema kuwa nguzo yako kubwa ni kuwa wewe ni mtoto wa rais mstaafu na hiyo ndio nguzo yako kubwa katika kuwania nafasi hii.

Jibu Yeye ni daktari na ana uzoefu katika serikali kwa muda mrefu na haina mahusiano yoyote na nafasi ya uongozi uliopita wa mzazi wake.

Swali unajisikiaje kupambana na mtu ambae ameshakuwa na uzoefu Maalim Self Hamad hii ni mara ya sita na tayari ameshakuwa na uzoefu.

Jibu Uchaguzi ni kampeni na sera wananchi watachagua sera nzuri na pia wananchi wengi ni vijana na watapenda damu changa na sera nzuri na hii kwao ni faida.

Swali Ni kipi unaweza kuiga kutoka kwa mzazi wako ambae ni rais mstaafu, ambae alikalia kiti ambacho wewe nawe unataka kwenda kukalia.

Jibu Mimi sijawahi kufanya kazi na Mzee Mwinyi ila kwenye historia kuna mambo mazuri ambayo ameyafanya kama kuruhusu biashara za aina zote zifanyike na mimi naweza fanya hivyo ila kwa utaratibu wa sasa.

Swali Katika kipindi cha hivi karibuni uchumi wa Zanzibar umekuwa ukiendeshwa na utalii ila sio biasharaya kutemgea sana kama kipindi hiki kuna corona na zao la karafuu limezorota, wewe unajipanga vipi kuleta maendeleo Zanzibar.

JibuUchumi wa visiwa unafanana na Zanzibar lazima iige mbinu za Visiwa vinavyofanya vizuri badala ya kutegemea watalii lakini pia kuendeleza bandari na uvuvi ili kuongeza pato kwa ujumla na yapo ambayo tutaboresha ili kuongeza kipato zaidi.

SwaliKwenye utalii kumekuwa na kelel kwamba Si kwakiasi kikubwa Zanzibar imekuwa ikifaidi na hivyo wageni kufaidi zaidi una mpango gani ili kiasi kikubwa cha mapato kiifaidishe zaidi Zanzibar ?

Jibu Biashara au shughuli yoyote inayofanyika Zanzibar ni lazima iwafaidishe wananchi hivyo ni vyema kuangalia upaya sera na kuona jinsi ya kufanya wananchi wa Zanzibar waweze kupata mafufaa, lakini pia Kodi sera za kodi kwa kiwango gani tunapata manufaa na kuboresha ili kuleta mafuaa.

Swali Hakuna shaka kama utapata nafasi basi muungano utakuwa katika mikono salama lakini pia umejipangaje kuhusu malalamiko au kero za muungano kama wanavyoziita ili yasiwepo

Jibu Ni kweli lakini si kero bali ni changamoto ila tutaangalia jinsi ya kuyatua yale machache ambayo bado yapo ili kila mmoja apate manufaa ya muungano huu.

Swali Ni nini kauli mbiu au ahadi yako kwa wazanzibari na kuwaonesh akuwa wewe ndie unaefaa kuchukua kijiti cha nafasi ya rais ajaye.

Jibu Dhamira yangu ni njema nia yangu ni kuweza kuongeza kipato cha Mzanzibari na kufanya kazi kwa maslahi ya Mzanzibari na kusimamia serikali nitakayoiunda ili kuongeza kipato na kuboresha huduma za kijamii Zanzibar.

Swali Mwishi kabisa unawaambia nini au una ushauri gani kwa Wazanzibari

Jibu Nawaambia kuwa tunakwenda kwenye uchaguzi na vyama vingine na mimi nawaambia wana CCM na Wazanzibar kuwa tudumishe amani tuliyonayo atakaeshindwa akubali matokeo na sisi tunaimani kama tutashinda na atakaeshinda akfanye kazi kwa nguvu sana ili kuleta maendeleo Zanzibar.
 
Ameshafeli kama ameanza mapema kuingia kwenye huu mtego, CCM wanafanya makosa sana kuacha kura za visiwani zipigwe bara na wabara pia..

Kura za Urais Zenji zilipashwa zipigwe na wazenji tena wakiwa kisiwandui pale au bwawani hoteli, kura za wazenji kupigwa dom tena wapiga kura wengi wakiwa wabara ni dhahiri kunathibitisha wazenji hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe na kila kitu lazima kifanywe bara..

Wazanzibar simameni pamoja kuwaonyesha wabara nyie ni wazenji na Rais wenu lazima atoke zenji kwa kura za wazenji..

Rais wa Tanzania ni wa wote kwa maana ya Bara na Zenji hivyo kura lazima zipigwe na wote labda tulete serikali tatu, Zenji rais wao, bara rais wao na Tanganyika rais wake au zenji na bara ziwe na Mawaziri wakuu na Rais awe mmoja, au makamu wa Rais awe Rais wazenji na huku bara kuwe na waziri mkuu tu....
 
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.

Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.

Source Swahili times

Maendeleo hayana vyama!
Kazi imesha anza sasa kuivuruga ccm, namuona mzee wetu Seif Sharif akitoboa kirahisi
 
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.

Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.

Source Swahili times

Maendeleo hayana vyama!

Nimejari kutafuta source ya hii habari sijaona,watu wanachangia habari ya mtunzi.
 
Kwa hiyo rais mtarajiwa wa Zanzibar kashaanza kuwagawa Watanzania kwa mafungu ya bara na Zanzibar?

Kura za watu wa bara na za wa Zanzibar zipo sawa au hazina usawa?

Kama zipo sawa, mjadala huu si muhimu, kwa nini anauendekeza?

Kama hazipo sawa, kwa nini zinapigwa pamoja kama ziko sawa?
 
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Mwinyi amesema wajumbe wa Zanzibar waliowapigia kura walikuwa 68 na siyo 35 kama inavyovumishwa.

Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amewataka watanzania wawe wakweli badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija yoyote.

Source Swahili times

Maendeleo hayana vyama!
Dkt Mwinyi anapaswa kuwa makini mno kwa sasa kwa kauli zake, anapaswa kuwa na timu kabambe sana ya kampeni tena yenye kujumuisha watu waliokuwa kambi tofauti naye. Ili pale zitolewapo kauli za mitego kama hizo, wawe ndiyo wa kwanza kuzitolea majibu ya kuzikanusha.

Nyufa zipo kubwa sana kwa upande wa CCM Zanzibar, akumbuke matokeo yaliyompatia yeye ushindi yameaacha si makovu tu mioyoni mwa waliokuwa wajumbe na kambi zao bali vidonda halisi. Matokeo yale yaliliza baadhi ya wajumbe, kwa hiyo kitu muhimu sasa ni kutumia kila njia awezayo ili kuleta maafiakiano na kujenga umoja ndani ya chama chake. Ili kufanya pale anapokwenda kukabiliana na Maalim Seif, awe amejizatiti kweli kweli.
 
Ameshafeli kama ameanza mapema kuingia kwenye huu mtego, CCM wanafanya makosa sana kuacha kura za visiwani zipigwe bara na wabara pia..

Kura za Urais Zenji zilipashwa zipigwe na wazenji tena wakiwa kisiwandui pale au bwawani hoteli, kura za wazenji kupigwa dom tena wapiga kura wengi wakiwa wabara ni dhahiri kunathibitisha wazenji hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe na kila kitu lazima kifanywe bara..

Wazanzibar simameni pamoja kuwaonyesha wabara nyie ni wazenji na Rais wenu lazima atoke zenji kwa kura za wazenji..

Rais wa Tanzania ni wa wote kwa maana ya Bara na Zenji hivyo kura lazima zipigwe na wote labda tulete serikali tatu, Zenji rais wao, bara rais wao na Tanganyika rais wake au zenji na bara ziwe na Mawaziri wakuu na Rais awe mmoja, au makamu wa Rais awe Rais wazenji na huku bara kuwe na waziri mkuu tu....
Mkuu mbona kwa idadi ya kura za zanzibar amepata kura 33 karibu sawa na nusu ya kura zote za Zanzibar hivyo wangepiga wanzibar tupu bado angeshinda maana wenzie wamegawana kura zilizo baki.

Kwahivyo wanzanzibar wameonesha wanamkubali.
 
Back
Top Bottom