Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,454
- 149,357
Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu Nchemba , tunaomba kujua huyu mtu ni nani hasa na je, BOT walimpa leseni ya kufanya hii biashara kihalali hapa nchini?
Na kama ana leseni, basi Waziri Mwigulu hebu chunguza leseni ya huyu bwana kama imetolewa kwa njia halali hasa kutokana na riba wanazochaji, muda wa kurejesha na kama anatimiza masharit menginei ya BOT pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.
Kuna App mbilli tofauti ambazo ndani yake kuna products kadhaa zinazotoa mikopo lakini malipo yote kupitia lipa namba ya mitandao ya simu jina lililosajiliwa linasoma Mr. Finance.
Pia, chunguza mikataba ya kazi ya hao vijana anaowaajiri na ikibidi muwahoji wanafanya kazi katika mazingira gani(wanalipwaje, n.k).
Tetesi ni kuwa hawa ni Wachina na kama ni kweli, inabidi tujiulize hivi mtanzania unaweza ukaenda china na kufanya biashara ya kuumiza wachina kwa riba kubwa na ukabaki salama?Nchi yetu imekuwa shamba la bibi?
Na je, unaweza kwenda nchi za watu na ukadhalilisha/kutishia kudhalilisha watu kama wanavyofanya wakopeshaji wa mitandaoni hapa nchini?
Na kwa riba wanazotoza, tunaomba serikali itueleze ni kodi kiasi gani wanalipa serikalini kwani hii biashara hawaifanyi kwa kificho bali hutumia mitandao ya simu kufanya transcations zao za kukopesha na kupokea marejesho.
Mr. Finance ni mmoja tu wa hawa wenye hizi biashara hapa nchini, hivyo mna kazi kubwa ya kufanya.