BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,812
DODOMA: Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amelitaka Jeshi la Polisi kukamilisha mchakato wa matumizi ya Kamera zitakazokuwa zikivaliwa na Askari wakiwemo wa Usalama Barabarani kwa lengo la kudhibiti Vitendo vya Rushwa
Dkt. Mpango ameeleza hayo wakati akizindua Kituo cha Polisi Daraja A, Mtumba Jijini Dodoma ambapo amesema "Waziri wa Mambo ya Ndani amenihakikishia mchakato wa ufungaji Kamera za Barabarani Kamera za Mavazi (Body Cam Jacket za Askari umeanza ili kuongeza weledi kwa Trafiki na usalama Barabarani"
Ameongeza "Askari Polisi anapokuwa anaongea na Madereva huko Barabarani kila kitu kinakuwa kinaonekana na kwa hiyo nafasi ya Rushwa inakuwa imepungua sana"