Dkt Mollel achafua hali ya hewa kwa kauli ya Fedha za Maendeleo hazitokani na kodi bali za CCM

Ndagullachrles

Senior Member
Jun 20, 2023
130
141
KAULI ya Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Jimbo la Siha,Dkt .Godwin Molllel kwamba fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali hazitokani na Kodi za wananchi bali ni fedha za chama Cha Mapinduzi (CCM), imeonekana kuwachefua wananchi wengi.

Mollel anasikika kwenye video inayozunguka mitandaoni akiwaeleza wananchi wa Jimbo la Siha kuwa fedha za maendeleo hazitokani na Kodi zao.

Kuhusu kauli soma LGE2024 - Dkt. Mollel: Hii sio kodi yenu, ni CCM ndio imeleta hela

Alikuwa akihutubia kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi A
za uenyekiti wa vijiji na vitongoji kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mapema jumatano wiki hii .

"Sasa ngoja niwaeleze,eti watu wanasema hii ni Kodi yenu, eti wanasema ni hela ya serikali,hakuna cha Hela ya serikali hapa"

"Ni mbunge wa Chama cha Mapinduzi, Rais wa Chama Cha Mapinduzi, madiwani wa Chama cha mapinduzi na wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi tumeenda kutafuta Hela tukazipata tukazileta",amesikika Mollel.

Baada ya video hiyo kusambaa ,wananchi wamepaza sauti na kuitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi hayo wakidai yanaichafua serikali .

"Hivi hii kauli ilistahili kutolewa na mtu mwenye hadhi kama Naibu Waziri kwamba Kodi zinazotolewa na wananchi haziendi kufanya shughuli za maendeleo kweli ?"amehoji Mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mwananchi huyo amesema kuwa kwa uelewa wake chama Cha Mapinduzi (ccm) na vyama vingine vya siasa vyenye wabunge hupata ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya uendshaji wa shughuli za vyama vyao na si vinginevyo.

"Mimi kwa uelewa wangu mdogo,fedha za maendeleo zinapitishwa na bunge wakati wa kikao cha bunge la bajeti na si vinginevyo"amesema Mwananchi huyo .
 
Huyo asamehewe bure alidhani anamfurahisha mheshimiwa Rais kumbe anamchafua. Sasa hivi nadhani akili imesha mrudi. Hicho kichwa chake ni kama mtu mwenye " Downis Syndromes".
 
Hivyo kweli Ukimuangalia Vizuri Yule Dr Mollel kile kichwa Chake na Komwe lile, kweli Yuko Sawasawa YULE? Ile ni Type ya Wale kina Shedede
Huyo Mollel atakuwa ni mwendawazimu anayetakiwa awekwe kwenye kumbukbu ya Dunia, kuwa ndite mwendawazimu pekee alitefanikiwa kuwa kiongozi, akiwaongoza wendawazimu wenzake na watu wenye akili timamu, huku wente akili timamu wakiwawametulia na kukubali kuongozwa na mwendawazimu.
 
Enzi Za Mzilankende Angeshamfyatua Zamani
Yeye mwenyewe ndiye muasisi wa huo ujinga,ni wakati wake ndiyo hela ya serikali iliitwa hela yake na kusemwa yeye ndiye alikuwa akitoa hela ya miradi ya maendeleo wakati ni fedha za wananchi wenyewe kupitia kodi wanazo tozwa.
 
KAULI ya Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Jimbo la Siha,Dkt .Godwin Molllel kwamba fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali hazitokani na Kodi za wananchi bali ni fedha za chama Cha Mapinduzi (CCM), imeonekana kuwachefua wananchi wengi.

Mollel anasikika kwenye video inayozunguka mitandaoni akiwaeleza wananchi wa Jimbo la Siha kuwa fedha za maendeleo hazitokani na Kodi zao.

Kuhusu kauli soma LGE2024 - Dkt. Mollel: Hii sio kodi yenu, ni CCM ndio imeleta hela

Alikuwa akihutubia kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi A
za uenyekiti wa vijiji na vitongoji kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mapema jumatano wiki hii .

"Sasa ngoja niwaeleze,eti watu wanasema hii ni Kodi yenu, eti wanasema ni hela ya serikali,hakuna cha Hela ya serikali hapa"

"Ni mbunge wa Chama cha Mapinduzi, Rais wa Chama Cha Mapinduzi, madiwani wa Chama cha mapinduzi na wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi tumeenda kutafuta Hela tukazipata tukazileta",amesikika Mollel.

Baada ya video hiyo kusambaa ,wananchi wamepaza sauti na kuitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi hayo wakidai yanaichafua serikali .

"Hivi hii kauli ilistahili kutolewa na mtu mwenye hadhi kama Naibu Waziri kwamba Kodi zinazotolewa na wananchi haziendi kufanya shughuli za maendeleo kweli ?"amehoji Mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mwananchi huyo amesema kuwa kwa uelewa wake chama Cha Mapinduzi (ccm) na vyama vingine vya siasa vyenye wabunge hupata ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya uendshaji wa shughuli za vyama vyao na si vinginevyo.

"Mimi kwa uelewa wangu mdogo,fedha za maendeleo zinapitishwa na bunge wakati wa kikao cha bunge la bajeti na si vinginevyo"amesema Mwananchi huyo .
Anaiabisha hiyo nafasi huyo hafai na kumdhalilisha aliyempa nafasi hiyo.
 
Back
Top Bottom