Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,663
- 8,795
Rais Magufuli leo yupo mkoani Kagera akitokea Chato kuendelea na kampeni za kuwania Urais kwa muhula wa pili. Hizi ni baadhi ya picha za Rais Magufuli akiwa anaongea na Wananchi alipokuwa njiani katika mkoa Kagera.
Picha zikimuonesha Rais Magufuli akiwa katika gari akizungumza na Wananchi Mkoani Kagera
Zaidi ya hayo, Rais Magufuli akiwa njiani alisimama Muleba, lililokuwa jimbo la mama Anna Tibaijuka upande wa Muleba Kusini
Anna Tibaijuka: Nashukuru sana mheshimiwa Rais kuniruhusu na mimi nikapumzike. Ninapopumzika, hapa tunaacha ni mahali salama. Kuna mtu mwenye mashaka na baba huyu? Kuna mtu mwenye wasiwasi? (Wananchi: Hamna).
Nyinyi wanangu wa Muleba, walio wengi hapa ni wanangu na wewe mheshimiwa Rais ukiwa mdogo wangu. Hapa Muleba, jirani yetu ni Chato, wembe ni uleule. Wazungu wanasema kama huyu Rais Magufuli ana mshikaji wake, wanasema natural allie ni Muleba Kusini, Muleba kwa ujumla.
Kwa hio kura hapa zitaendelea kuwa za heshima mheshimiwa Rais kama ilivyokuwa 2015. Hapa usiwe na shaka na mimi hapa mstaafu na dada yako, nashukuru sana.
BASHIRU: Hapa mimi ndiko ulikonitoa jalalani(Bukoba) maana kuna lugha ya jalalani, ukiwa Kagera sisi wasaidizi wako umetutoa jalalani na mimi niko kwenye jalala langu na jana nimekuona ukiwa kwenye jalala lako Chato, sasa ni zamu yangu, acha nijidai kwenye jalala langu la Kagera.
MAGUFULI: Miaka mitano iliyopita tulipita hapa kuomba kura na tuliwaomba kwa heshima kubwa, mgombea wa ubunge wakati huo alikuwa Prof. Tibaijuka. Mimi Prof. Tibaijuka ni dada yangu na nataka niwaeleze hata marehemu mume wake alipokuwa balozi kule Sweden, mimi nikiwa naibu waziri wa ujenzi na mbunge kwenye miaka ya 95 nilienda mpaka huko kwa hio Prof. Tibaijuka ninamfahamu.
Baada ya wakati ule, mheshimiwa Masilingi, aliyekuwa mbunge wa hapa kabla ya mama Tibaijuka nae ni rafiki yangu, tulihangaika nae wote kwenye barabara ya kwenda mpaka Kyamyora mpaka kuelekea Kimwali. Ndio maana alipomaliza kumuachia Pro. Tibaijuka, Masilingi nikamteua kuwa balozi na hata mpaka leo ni balozi kule Marekani, ndiyo faida ya kumteua unayefahamu.
Hata mama Tibaijuka amesema amestaafu lakini kwangu mimi hajastaafu.
Huyu Bashiru, hakuna mtu alitegemea atakuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania nzima, alikuwa muuza ndizi pale Kemondo, baadae akaenda chuo kikuu akafundisha lakini leo ndio katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania nzima, Muleba Oyee.
Serikali hii ina mavyeo mengi na ndio maana nimemwambia hata Prof. Tibaijuka, ameniambia hapa, mdogo wangu nimestaafu. Mimi nakwambia hapa, Prof. hujastaafu. Hauwezi tukamuacha Profesa akakaa tu hapa wakati kuna maeneo mengi ya kwenda kufanya.
Muachane na propaganda ambazo zinafanyika, kwamba mkituchagua sisi tutafuta kodi. Utafutaje kodi wakati kwenye mikutano yako unachangisha kodi?
Unasema utafuta kodi, ukienda kwenye mkutano, naomba mtuchangie, sasa wakiingia zile tulizozikusanya si watazitumia vibaya, zile tulizopanga kununua meli ambayo inatengenezwa pale, zitapotea.
Msichague watu wasioaminika, msichague watu watakaokuja kutawala kwa matakwa ya watu wengine. Na si ajabu zikarudishwa hapa lockdown wakati Mungu ameshaimaliza.