mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Nafuatilia kampeni za Uchaguzi Mkuu, sina shaka yoyote kuwa upinzani haujawa tayari kupewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi hii. Kwa sababu kuu zifuatazo, Bunge la kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu, lipitishe kwa kauli moja, pasiwe na uchaguzi wa Rais hadi 2030. Kwa maana hii Rais Magufuli aendelee kutawala hadi muda huo.
1) Wakati CCM ina Katiba yenye kuiagiza Serikali yake kujenga uchumi wa kujitegemea utakaomkomboa mwananchi mmoja mmoja kuondokana na umaskini, hakuna chama kingine cha siasa chenye mwelekeo huo. Rejea Ilani ya CCM ya uchaguzi, 2020, Sura ya 2 (naambatanisha).
2) Rais Magufuli amethubutu na kutekeleza yaliyoelekezwa na CCM kwenye Ilani ya Uchaguzi, 2015. Viongozi wa upinzani wamebaki kushangaa na ili kuendelea kuwa kwenye ramani ya siasa wamekuwa wakiendesha siasa za kupinga kila kitu. Hili linaendelea kujitokeza kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
3) Miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za jamii, faida yake itaonekana baada ya miaka kama 5 na kunufaisha kizazi cha Watanzania wa kesho. Ni busara msimamizi wa miradi hiyo aendelee kuwepo kuhakikisha haihujumiwi.
4) Rais Magufuli amekuwa kinara wa kuendesha vita ya kiuchumi ili nchi iwe huru kiuchumi. Vita hii si lelemama kwa jinsi ile ile Baba wa Taifa alivyoweza kuleta Uhuru wa Bendera. Kufanikisha kwake uhuru wa Uchumi utakomboa nchi nyingine za Afrika kiuchumi kama alivyofanikisha Baba wa Taifa uhuru wa bendera.
4) Tanzania na bara la Afrika linamhitaji sana Magufuli kwa kipindi kirefu ili utajiri wa nchi hizi ulete maendeleo ya kushangaza dunia. Kwa kipindi kifupi cha miaka 5 ya utawala wake, Tanzania imepiga hatua kubwa kimaendeleo. Kwa kauli yake, muda si mrefu Tanzania itakuwa nchi ya kutoa misaada kwa nchi nyingine kujiendeIeza.
5) Utawala wa Magufuli umesaidia vyama vya upinzani kujijenga kisiasa. Ushahidi ni jinsi wapiga kura wanavyokusanyika kwenye kampeni zao. Bahati mbaya, kwa uchanga wa kisiasa, viongozi wa upinzani hawatumii fursa hiyo kujiimarisha kisiasa bali kuchochea vurugu. Katika hali hiyo ni busara waendelee kujifunza kuendesha siasa hadi 2030 ambapo watakuwa wamekomaa kisiasa.
NAWASILISHA
PIA SOMA
- Hashim Rungwe: Kama tatizo ni muda, Rais Samia aongezewe muda ili tupate Katiba Mpya ndio tufanye Uchaguzi
- Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka
- Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono
- Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani
- Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?
- Uchaguzi 2020 - Dkt. Magufuli aongezewe muda wa kutawala
- Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala