JOYOPAPASI
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 250
- 409
Ubunifu, weledi, msimamo, uzalendo, uadilifu na kasi kubwa anayokuwa nayo katika kufanya maendeleo, ndivyo vinavyomtofautisha Rais .Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Marais wengine barani Afrika. Maneno na vitendo vyake vya kizalendo ni ngumu kuvificha “Tumeongeza bajeti ya maendeleo ili kuondoa kero nyingi zinazowakabili wananchi na pia kuleta maendeleo ya haraka kwa nchi yetu….”. Kazi ya kufukuza umasikini nchini ni vita kubwa kama zilivyo vita nyingine duniani.
Wakati ukihimiza wananchi wako kufanya kazi ili kuwa na maisha mazuri, wapo baadhi yao wanaotaka kuwanyonya wanyonge usiku na mchana “Kazi yoyote ya mabadiliko lazima wapo watakaoumia kwasababu hawataki kubadilika” Hizo ni baadhi ya kauli za Rais Magufuli. Kwa hakika huyo ni Rais bora barani Afrika.
Wakati fulani mwanzoni mwa mwaka 2016 watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari barani Afrika walianza kutabiri kwamba kuna Rais yuko Tanzania anaitwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Rais huyo wa Tanzania ni aina ya Rais mzalendo, mchapakazi ambaye hajaonekana barani Afrika kwa muda mrefu sasa. Miaka michache baadae msomi nguri na mchambuzi wa masuala ya kisiasa mwenye weledi usiofichika Prof. Patrick L. O. Lumumba kutoka Kenya alivunja ukimya akasema, Rais Dkt John Magufuli ni Rais bora Afrika Mashariki na Barani Afrika.
Aliendelea kusisitiza kuwa Mwalimu J.K. Nyerere yuko hai anaishi ndani ya Rais Dkt John Magufuli. Na kama haitoshi alianzisha kitu kinachoitwa MAGUFULIFICATION. Mwaka 2016 gazeti la New African Magazine lilimuandika Rais Dkt John Magufuli kama mtu maalumu na mashuhuri wa kuigwa barani Afrika wakimpongeza kama *AFRICAN OF THE YEAR 2016*.
Tumeongeza bajeti ya maendeleo ili kuondoa kero nyingi zinazowakabili wananchi na pia kuleta maendeleo ya haraka kwa nchi yetu…” Ni maneno aliyosema Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli akihitaji Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa kiuchumi.
Lengo kuu la Rais Dkt John Magufuli alijua kuwa uchumi wa Tanzania unapaswa kujengwa na Watanzania wenyewe na wanaweza kufanya hivyo. Maneno ya Mwalimu J.K. Nyerere yanawakumbusha Waafrika kujitegemea, aliwahi kusema *Independent can not be real if a nation depends upon gift* Akimaanisha *Nchi ambayo bado inategemea misaada haina uhuru thabiti* tafsiri.
Wakati wa taharuki kubwa ya ugonjwa wa CORONA (COVID 19) nchi zenye uwezo mkubwa kiuchumi zilitaka kukopesha nchi za Afrika, ili fedha hizo zitumike kupambana na ugonjwa huo. Rais Dkt John Magufuli alitofautiana na viongozi wengine wengi wa bara la afrika kimtazamo. Yeye alisisitiza kwamba, wakati wa ugonjwa si wakati sahihi kwa nchi za Afrika kukopeshwa fedha bali ni muda wa kusamehewa madeni ili fedha ambazo zingetumika kulipa madeni ndizo zitumike kushughulikia matatizo ya magonjwa.
Akili ya hali ya juu ya Magufuli ilinikumbusha, Thomas Isdore Noel Sankara (Rais wa Burkina Faso mwaka 1983 mpaka 1987) aliwahi kusema *Debt is a cleverly managed reconquest of Africa, It is a reconquest that turns each one of us into a financial slave* Speaking at OAU summit, 1987. Alimaanisha *Madeni ni mbinu ya kuitawala tena Afrika na ni kwa mbinu hiyo kila mmoja wetu imemgeuza kuwa mtumwa wa madeni* Tafsiri.
Rais bora Afrika anajulikana kwa mawazo na vitendo vyake Aliposema kuleta maendeleo ya haraka kwa nchi yetu, Rais Magufuli alimaanisha wakati nchi nyingine zinatembea juu ya suala la maendeleo, Tanzania inapaswa kukimbia mbio kali za mita mia moja. Na kama kuna haja ya kupaa kwenye suala la maendeleo basi ni vema kufanya hivyo. Kufumba na kufumbua miradi mikubwa ikaanzishwa, Rais mwenye uthubutu alihitaji aone ndege zikinunuliwa ili kuboresha usafiri wa anga na kuimalisha sekta ya utalii nchini, hilo limefanyika.
Ukitaka kuona fly over siyo mpaka uende ulaya, kama uko nje ya jiji la Dar siku umeamua kwenda kumsalimia shangazi yako Dar utashuhudia kwa macho yako mwenyewe. Suala la umeme anzia vijijini uangalie kazi iliyofanyika, kisha nenda ukaone bwawa la mto rufiji ili uelewe nchi hii inaelekea wapi katika suala la nishati ya umeme. Kwenye suala la Nishati Kuna Mradi wa Umeme almaarufu *Mradi wa Umeme Wa Dege Megawatts 54, Unakamilika mwezi wa Kumi* Hakika JPM bado Ni Rais Bora Bara la Afrika 2015-2020.
Mambo ya shule kila kitu kiko wazi, kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha nne ni elimu bure. Habari za afya takribani hospitali 98, vituo vya afya 433 na zahanati zaidi ya 1,000 zimejengwa.
Kuna mapinduzi makubwa upande wa madini unaweza kwenda melerani kujifunza.
Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mpaka june 30 zaidi ya bilioni 520 zilikuwa zimekusanywa upande wa madini tu.
Kuchapa kazi na kulipa kodi ni mambo ambayo yamesisitizwa sana katika serikali ya awamu ya tano. Baada ya mambo hayo kueleweka vizuri kwa Watanzania, makusanyo ya kodi yameongezeka kiasi cha kukusanya zaidi ya shilingi trioni moja kwa mwezi a.k.a CONTROL NUMBER.
Baadhi ya vitu vilivyodhaniwa kuwa ni ndoto kufanyika Tanzania sasa inawezekana. Mtani wangu mmoja alinitania juzi akisema, Treni ya umeme siyo mpaka ukaipande Ubeligiji au Ujerumani. Treni ya umeme inatoka Dar mpaka Mwanza na Kigoma. Wakulima na wavuvi wanaisubiri treni hii ili wasafirishe mazao yao kwa haraka.
Tanzania kuwa kama Ulaya inawezekana chini ya kiongozi mzalendo Rais Dkt John Magufuli.
Hakuna rais barani Afrika ambaye amejipambanua kuwa bora zaidi ya Rasi Magufuli kwa miaka mitano iliyopita na hasa ukiangagalia katika mambo kama Ubunifu, weledi, msimamo, uzalendo, uadilifu na kasi kubwa ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.
Hakuna maajabu kwa watu wa nchi nyingine barani Afrika kumhitaji Rais Dkt John Magufuli kuwa Rais katika nchi zao. Lengo lao ni moja tu, haya maendeleo chanya na ya kutisha yaliyofikiwa hapa nchini Tanzania hata kuiwezesha nchi yetu kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kipato Cha kati kwa muda mfupi, basi yafanyike pia katika nchi zao.
Rais Dr. John Pombe Jeseph Magufuli ni Rais bora wa wakati wote, na ni MOST INFLUENTIAL AFRICAN OF THE YEARS 2016 TO 2020.