Dk.Philip Mpango aagiza NEMC kuangalia mapungufu ya kisheria yanayosababisha kukosa nguvu katika usimamizi wa usafi wa mazingira

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
534
754

images.jpeg

MAKAMU wa Rais, Dk.Philip Mpango amezindua chapisho la utafiti wa hali ya mazingira ya Pwani na Bahari Tanzania Bara huku akiagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuangalia mapungufu ya kisheria yanayosababisha kukosa nguvu katika usimamizi wa usafi wa mazingira ili kufanyiwa marekebisho.

Akizungumza jana kwenye Kongamano la wadau wa mazingira lililoandaliwa na NEMC, Dk.Mpango alisema miji mingi taka zimejaa kila kona na NEMC hawana meno kisheria.

"Tumepiga kelele za kutosha kuhusu usimamizi, utunzaji na usafi wa mazingira na Sheria ni kikwazo basi zitazamwe taratibu zipo, NEMC nendeni mkaangalie Sheria zenu na Taasisi zingine, mnipe mrejesho nijue tatizo ni nini,"alisema.

Alisema kwasasa athari za mabadiliko ya tabianchi zinachangia upotevu wa asilimia moja ya pato la Taifa na inakadiriwa ifikapo Mwaka 2030 kuna uwezekano wa kupoteza asilimia Tatu ya pato la Taifa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Immaculate Sware Semesi, alisema kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira kwa lengo la kujadiliana namna Bora ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingiraili kutoka na mikakati ya pamoja ya kuzitambua na kushughulikia kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

"Nchi yetu na Dunia kwa ujumla inakabiliwa na changamoto za kimazingira, mfano mabadiliko ya hali ya hewa, tabianchi, upotevu wa bioanuai, uchafuzi na uharibifu wa mazingira, upungufu wa maliasili, ni ukweli unaoathiri maisha yetu ya kila siku Afya, makuzi, mahusiano, uchumi na madhara haya yatakwenda hadi vizazi vijavyo tusiposhughulikia sasa."
"Makubaliano ya kisayansi yapo wazi kwamba hatua za haraka na madhubuti zinahitajika ili kulinda mazingira yetu,"alisema

"Baraza lina jukumu la kulinda na kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na limepewa jukumu la kusimamia athari za mazingira nchini zinazotokana na shughuli za kibinadamu nchini,"alisema.

Alisema usimamizi wa mazingira umeendelea kuhitaji mbinu mpya na za kimkakati kutokana na mabadiliko yanayoendelea kuwepo katika mifumo ya ikolojia na mbinu na teknolojia za uvunaji na uzalishaji.
Alifafanua kuwa katika kuelekea siku ya mazingira duniani Baraza hilo limeona ni muhimu wadau kupata elimu ya mazingira.

"Tunategemea kongamano hili litakuja na njia ya kupunguza changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na upotevu wa bioanuai,"alisema.
Kadhalika, alisema katika kongamano hilo wadau watajadili matumizi ya nishati safi kwa Maendeleo ya nchi na jamii.

"Pia tutajadili uthibiti wa taka ngumu, plastiki na ushiriki wa sekta binafsi katika kuhifadhi mazingira, jambo jingine kupitia kongamano hili ni kuwa na jukwaa mahsusi la wadau wa mazingira nchini ili kukutana kila mwaka kuwa na mikakati yenye tija katika usimamizi wa mazingira nchini,"alisema
"NEMC inathibitisha katika kujitathmini, kujiboresha na kujiimarisha katika kushauri serikali kwenye usimamizi wa mazingira nchini. Leo kutazinduliwa chapisho la hali ya mazingira ya Pwani na Bahari Tanzania Bara ambapo kazi hiyo ilifanyika NEMC kwa kushirikiana na Taasisi zingine,"alisema.
large-1717165825-nnnnnnnnnn.jpg

Akiwasilisha maelezo kuhusu chapisho hilo, Dk. Julius Francis kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM alisema ni chapisho la pili kuzinduliwa katika kipindi cha mwezi mmoja na kwamba chapisho la kwanza lilihusu upande wa Zanzibar.

"Chapisho hili limeandaliwa kwa kufuata matakwa ya mkakati wa Taifa wa usimamizi wa rasilimali za Pwani na Bahari, unatoa mchango katika uandaaji wa taarifa ya mazingira na kutimiza matakwa ya mkataba wa kimataifa wa Nairobi katika usimamizi na uendelezaji wa mazingira Bahari na ukanda wa Pwani katika eneo la Bahari ya Hindi kama inavyotakiwa vyombo vingine vya kimataifa kuandaliwa taarifa kila baada ya miaka mitano au 10,"alisema.

Alisema chapisho hilo limeandaliwa na wataalamu 18 kutoka Taasisi za Serikali na limegawanyika katika sehemu kuu sita na mandhari yake ni kuelekea uchumi wa Buluu na mchango wa rasilimali za Pwani na Bahari.

"Chapisho limebeba ujumbe mahsusi katika maeneo manne kuna viashiria vinaonesha baadhi ya makazi ya viumbe yameathirika na yapo hatarini kutoweka iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa ili kurejeshwa katika mazingira ya awali,"alisema
Mtaalamu huyo alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi maeneo ya Pwani na Bahari zinazotoa fursa ya kujenga uchumi wa Buluu mkubwa na endelevu kw kuunganisha mikakati ya sekta mbalimbali.

"Chapisho hili limekuja wakati muafaka ambapo nchi yetu ipo kwenye uandaaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na utekelezaji wa sera na mkakati wa uchumi wa Buluu hivyo chapisho hili ni chanzo kizuri cha taarifa za hali ya mazingira na rasilimali za Pwani na Bahari,"alisema
Alisema katika kujenga uchumi wa Buluu kunahitaji mageuzi ya kimkakati katika kusimamia rasilimali za Pwani na Bahari kwa Kila sekta na mageuzi yanahitaji kufanyika na yatachukua muda matokeo kuonekana
 
Huyu Makamu wa Rais ameshindwa kupanda miti Dodoma kuunga mkono jitihada za kuifanya Dodoma ya kijani, na mapesa yote yaliyojaa duniani ya kuunga mkono mambo ya mazingira.

Katika makamu wa Rais ambaye haijulikani anafanya nini ni huyu, anakula hela za bure tu.

Basi achukue hata UDOM kama mfano akapande miti, sijui kama kweli ni muha, waha ni wachapa kazi
 
Bora hata RC wa Dar, imebidi awaambie ukweli kuwa haiwezekani wakimbilie kupiga kelele kwa wenye bar kuwa wanachafua mazingira(air pollution) wakati dar nzima maviwanda yanatiririsha chemikali kwenye vyanzo vya maji!! Wanamwambia apige marufuku utumiaji wa mkas wakazi wa dar, wakati wameshindwa kudhibiti huko inapotoka!! "Hiyo kazi hafanyi"
 
Huyu Makamu wa Rais ameshindwa kupanda miti Dodoma kuunga mkono jitihada za kuifanya Dodoma ya kijani, na mapesa yote yaliyojaa duniani ya kuunga mkono mambo ya mazingira.

Katika makamu wa Rais ambaye haijulikani anafanya nini ni huyu, anakula hela za bure tu.

Basi achukue hata UDOM kama mfano akapande miti, sijui kama kweli ni muha, waha ni wachapa kazi
jamani hebu wacheni lawama kwa kila kitu. Hivi hii taasisi ya misitu inafanya nini nayo inakusanya mapato kede kede kutoka kwenye mazao ya misitu?
 
Bora hata RC wa Dar, imebidi awaambie ukweli kuwa haiwezekani wakimbilie kupiga kelele kwa wenye bar kuwa wanachafua mazingira(air pollution) wakati dar nzima maviwanda yanatiririsha chemikali kwenye vyanzo vya maji!! Wanamwambia apige marufuku utumiaji wa mkas wakazi wa dar, wakati wameshindwa kudhibiti huko inapotoka!! "Hiyo kazi hafanyi"
RC hakuwa sahihi kwani malalamiko makubwa yanayohusu kelele yanatoka kwa wananchi. Yeye anaona ni sawa kwa wananchi kupigiwa makelele wakati wengine ni wazee na wagonjwa, lakini anakumbuka mapato tu. Na ni huyu huyu ndiyo nilimuona analalamika hivi majuzi kuhusu kelele karibu na nyumbani kwake Oyster Bay, au anaona sawa kwa kelele zipigwe maeneo ya uswahilini lakini kwao uzunguni wabaki kimya?

Na kama wanaona hawawezi kutekeleza basi wafute hiyo sheria na kanuni zake zote ili kila mmoja afanye analopenda mwenyewe.
 
Very interesting .Kuona no.2 analamikia wingi wa NEMC hadi mikoani na kazi zao zisizolidhisha.
1.Tumewahi kusema kuna mapungufu makubwa na uelewa mdogo wa maafisa wa NEMC katika utendaji kazi yao.
Mifano midogo ya kupima akili zao ni ukusanyaji wa taka kutoka majumbani.
Wao ukimbilia kuhamasisha taka taka za aina zote kuzipeleka kwenye dampo.Lakini wanasahau ukilundika takataka hizo nyingi bila kuzichakata ili kuzalisha by products nyingine ni kutengeza bomu kubwa ambayo nikujenga uchafusi mkubwa wa mazingira.
Wakati mwingine kama mazingira yanaruhusu hizi food waste waruhusu wananchi kwenye maeneo yao,
wakazifukia au kutengeneza compost,inayoweza kutumika katika kukuza kilimo cha mazao mbali mbali.

2.Nyerere alijenga umeme kutoka mabwawa ya Kidatu ,Mtera,Kihansi n.k kuzalisha umeme wa bei nafuu ,akatengeneza kiwanda TANELEC Arusha cha kuzalisha majiko ya kupikia yaliyo imara na nafuu tukapikia umeme.
Sasa ninyi mnatuambia tupikie gesi kutoka nje LPG badala ya kuweka nguvu kubwa tukatumia gesi asilia iliyo nafuu na ninyingu,na huku mkitukataza kutumia kuni na mkaa.Tanzania ina wakazi over 60 million na almost 98% hawawezi kumudu bei ya LPG.

Zipo nchi zinatumia majiko ya umeme kwa wingi.Umeme wa Bwawa la Nyerere unaweza kutusaidia kupata umeme wa bei poa kwa nchi nzima.

3.Upandaji wa miti nacho ni kitendawili,nchi jirani yetu Uganda wao wanahamasisha kupanda miti kama sisi LAKINI wao wamezifanyia utafiti wa kupanda miche bora na inayokuwa kutoa mazao kama matunda,kuni au mbao kwa muda mfupi sana.
Tanzania hakuna utashi wa taasisi zetu kupeleka tekinologia yao kwa wakulima wadogo wadogo.
 
Anzeni kupanga miji kwanza, mitaa ilyopangika haiwezi kuwa michafu.
Mwenzako anasema eti ''wapiga kelele weee, lakini tatizo haliishi''. Hivi mji unakuwa msafi kwa kupiga kelele? Wanakimbilia kutibu dalili za ugonjwa wanaacha ugonjwa wenyewe.
 
 
Back
Top Bottom