Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewaasa Wakristo kuliombea Taifa amani, utulivu, umoja na mshikamano uendelee katika kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu imeeleza, Dk Biteko amesema hayo leo Jumapili, Aprili 20, 2025 jijini Mwanza wakati aliposhiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la African Inland Church (AIC) - Makongoro.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Mwaka huu ni wa uchaguzi na una michakato mbalimbali ya kujiandikisha, kugombea, kupiga kura na kutangaza matokeo. Kwa niaba ya Serikali napenda kuwaomba waumini wa AICT na wale ambao tunadhani tuna uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali tujitokeze kwa wingi tugombee, wale tu wenye nia ya kweli tuhakikishe tunawasaidia watu katika hali zao,” amesema Dk Biteko.
Sambamba na kugombea amewahimiza waumini kuliombea Taifa kuelekea wakati na baada ya uchaguzi: “Tujitokeze ili tuweze kugombea kwa ajili ya kuhudumia nchi yetu na wakati wa kampeni utakapofika naomba tuendelee kuliombea Taifa.”